Mahakama ya Wilaya ya Temeke yavunja ndoa baada ya Bwana harusi kushindwa kushiriki tendo la ndoa kwa miaka 5. Bibi harusi kapotezewa fertility age

So kwa miaka 5 alikua anamridhishaje mkewe? Mm siamini huo upuuzi! Kuna kitu hapo. Au mwanamke aliangalia mali na kumvumilia jamaa ili aje achukue mali?

Wanaume mmeona hawa viumbe walivyokaa kitapeli?
Mahakama inaamua kesi kwa mujibu wa sheria na ushahidi yaani evidence,kila mtu anasikilizwa kwa misingi ya natural justice. Pretex haiwezi kuiongoza mahakama kutoa hukumu.Hata kitendo cha kukojoa nje kinaweza kuvunja ndoa.Coitus interruptus kinaweza kutafsiriwa kama ukatili ikiwa wahusika hawakukubaliana.
 
Kwenda mahakamani ni muhimu hata kama hakuna mali.
Ndoa za kikatoliki hubatilishwa na mahakama ya kanisa lakini lazima iende mahakama ya serikali ili wapate kibali cha kuwa huru ili waweze kuoa/kuolewa tena.
 
Dheheby gani walifungia Ndoa? Sijaona mahali mwanamke amethiditisha miaka mitano. Hata hivyo ingekuwa jamaa anapiga miti vizuri na mwanamke Hana uwezo wa kuzaa Ndoa ingevumiliwa.
Ndoa ingeweza kuvumiliwa lakini mwanaume asingevumilia kuishi bila kupata mtoto angeenda kuzaa nje ya ndoa.
 
Mtoa post moderator muwe mnaficha majina ya hayo wa husika , Sio sawa kbsa privacy za watu kuw waz
 
Sasa mbona mwamba kaaibishwa asee hii dunia ni ngumu sana
 
Kwenda mahakamani ni muhimu hata kama hakuna mali.
Ndoa za kikatoliki hubatilishwa na mahakama ya kanisa lakini lazima iende mahakama ya serikali ili wapate kibali cha kuwa huru ili waweze kuoa/kuolewa tena.
Kanisa lina Mahakama ?
 
Ndoa imefungwa mwaka june 2019 na ndoa hiyo imevunjwa na mahakama April 2024.

Piga hesabu mwenyewe utajua ndoa ilikuwa hai kwa miaka mingapi
Inawezekaa kesi ndo imechukua miaka hiyo ila ndoa ilivunjika siku hiyo hiyo au mwezi mmoja baadae...
 
Wakati wa uchumba hakuona hilo? Au mashine ilizimika baada ya ndoa?

Soma nakala ya hukumu utaona majibu ya swali lako.

Kwa ufupi hawakufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa. Walifata kanuni za kidini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…