Aramun
JF-Expert Member
- Nov 8, 2023
- 461
- 2,213
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam, imeamuru Uongozi wa Club ya Yanga ukiongozwa na Rais wa Yanga Injinia Hersi Saidi na wenzake, kuachia ngazi na kuondoka kwenye Club hiyo kwakuwa Katiba ya Yanga haitambui uwepo wao.
Imedaiwa kuwa uamuzi huu wa Mahakama umekuja baada ya Kundi la Wazee wachache waliowahi kuwa Wazee wa Yanga kipindi cha nyuma, kushitaki Mahakamani likidai uwepo wa Viongozi wa sasa wa Yanga (Injinia Hersi na wenzake) ni batili na haujafuata Katiba ya Club hiyo.
Kutokana na Wazee hao kushinda kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, inamaana kuwa Rais wa Yanga Injinia Hersi na Viongozi wenzake wanatakiwa kuachia ngazi na kukabidhi Ofisi kuanzia sasa.
Injinia Hersi alianza kuiongoza Yanga kama Rais miaka miwili iliyopita baada ya kushinda nafasi hiyo akiwa ni Mgombea pekee July 2022 na kumfanya kuwa Rais wa kwanza wa Yanga SC toka kuanza kwa mfumo mpya wa mabadiliko ambapo alitangazwa kuwa atakuwa madarakani kwa miaka minne ( hadi 2026 ) kwa mujibu wa Katiba ya Club hiyo.
Source: #MillardAyoUPDATES
- Yanga: Mkutano na wanahabari tar 17.07.204
====
Source nyingine:
Walipinga kutumika kwa katiba ya mwaka 2020 ambayo ilitumika kwenye uchaguzi Mkuu uliouweka uongozi uliopo madarakani wakisema katiba hiyo sio halali. Inasemekana RITA waliitwa kutoa ushahidi na wakasema wanaifahamu katiba ya mwaka 2011 ambayo ipo ofisini kwao na hiyo ya mwaka 2020 hawaitambui.
Baada ya kupata hukumu yao mwezi Agosti mwaka 2023 JUMA MAGOMA NA GEOFREY MWAIPOPO wameona hakuna utekelezaji wa hukumu hiyo hata baada ya kuwasilisha kwa wahusika wakaamua kufungua kesi ya kukazia hukumu ambapo itatolewa maamuzi mwezi Agosti tarehe 5 mwaka 2024, ili hukumu hiyo ianze kufanya kazi. Ambapo inategemewa Mkutano Mkuu wa Yanga kuitwa ambao utajumuisha WANACHAMA WOTE HAI sio wawakilishi wa matawi pekee (kama ilivyo sasa) na kwenda kwenye uchaguzi mkuu wa uchaguzi wa viongozi wa klabu kwa kufuata katiba ya mwaka 2011.
Kama hili litatokea manake Eng Hersi na timu yake watakuwa wameondoshwa madarakani kwakuwa watakuwa wameingia isivyo halali.
Pia soma==>> Je, Mahakama Ina Mamlaka ya Kumwondoa Rais wa Yanga Hersi?