Mahakama yaamuru kupigwa mnada nyumba ya mjane ili kumfidia aliyeumia mguu kwa ajali ya bodaboda

Siku zote ukipata shida inayohusiana na sheria ,wewe tafuta mwana sheria akusaidie vinginevyo utapewa hukumu hata ya mtu mwingine, tatizo ni kutokujua sheria ,kazi ya bima ni kudeal na ajali sio mtu binafsi
Mzee unajua hata Bima imefanyaje kazi? Unafahamu kitu kinaitwa 3rd party? Yaani huyo abiria aliyepata ajali kuna bima ya pikipiki hiyo inamhusu lakini pia kuna bima ya huyo mwenye gari nayo inamhusu. Sasa unabisha nini kusema BIMA haihusiki na chochote.
Huyo abiria alitakiwa apelekwe hospital na mwenye gari yeye na boda boda then wapewe huduma ya kwanza kisha matibabu watagharamikiwa kila kitu, kuanzia chakula, madawa na usimamizi wa madaktari hsadi siku wanapotoka hospital.
 
1.inaonekana gari haikuwa na bima, kama ingekuwa nayo wangedai bima

2.Sijajua vizuri hapo kisheria ila kama mali bado ni ya marehemu inatumika kulipa liability zake ambazo anadaiwa.

3.Kusaidiwa ni ubinadamu wa muhusika tu ila kisheria ni anadai fidia kwa maumivu(loss suffered) hivo huwezi kumlaumu kwa kudai
 
Hakuna sheria ya hivyo duniani,mdaiwa ameshakufa na kesi closed
No kama hakuna makando makando na marehemu alikuwa na makosa ya kulipa fidia huwa wanafuata mali zake kupitia msimamizi wa mirathi.
Ni busara ya anaedai tu kuamua kupotezea na kusamehe marehemu ila mabandidu huwa wanakazia hukumu hadi wanalipwa fidia
 
Hili swala liko serious sana katika hali ya utapeli ni lini na wap katika sheria inaposema kesi inarithiwa?aliyefanya hilo tukio ni marehem na vithibitisho kama vilikuwepo ilikuwaje mahakama ikampa mjane kesi aendelee nayo kama yeye ndie alikuwa mtuhumiwa wa hilo tukio?na kuhukumu kuwa nyumba iuzwe ilipwe kwa niaba ya marehem kumgonga huyo mtuhumiwa? Maswali tata

1.vyeti vya kuthibitisha marehem amefatiki vipo?
2.Mjane ameingia kuendelea na hiyo kesi?
3.je kesi zipo katika ulithi hasa kwa mtu aliyefariki?
4.hao wanasheria wamepata wapi hizo sheria za hvyo na pia hakimu kuendeleza kesi hyo kwa kuingizwa mtu ambaye hakuwa anaendedha hyo gari?
5.bima kama ipo wamechangia nn hapo juu ya kesi hyo?
Nb:Hakim na wanasheria waliotoa uamuzi huo wajuwe maisha ni mzunguko na hyo laana itawatafuna wao na familia zao iwe direct au indirect mana huyu mungu ni wetu sote na wanajisikiaje sasa baada ya hukumu kutoka na robbing waliofanya
 
Sasa huo m-picha wa Samia wanaweuweka hapo wa nini? Nchi ina wanafiki sana. Watu wanashindwa kujua shuruba za maisha wanazopata zinasababishwa na uongozi wa CCM?
 
nunueni bima ya vyombo vyenu. mtanishukuru.
 
1.inaonekana gari haikuwa na bima, kama ingekuwa nayo wangedai bima
Kuna jambo nina suspect,marehemu ndie aliyekuwa na mkataba na kampuni ya bima akifa then the contract is avoidable.

Hii ni kama vile mimi nikikuuzia gari yangu ikiwa na bima niliyokata. Ukapata ajali nayo bima niliyokata haitakufidia maana hawana mkataba na wewe. So nina suspect hata hapa bima wake decline kufidia sababu waliyeingia nae contract ameshafariki.
2.Sijajua vizuri hapo kisheria ila kama mali bado ni ya marehemu inatumika kulipa liability zake ambazo anadaiwa.
Sio mtaalam wa sheria ila kwa nijuavyo mali ya familia yaani ya mke na mume haiwezi taifishwa bila consent ya mke.

Sasa mke yupo mume kafa automatically ile mali ni ya mke ,why waje kuiclaim kwa mke na wanaedaiana nae yupo kaburini.
3.Kusaidiwa ni ubinadamu wa muhusika tu ila kisheria ni anadai fidia kwa maumivu(loss suffered) hivo huwezi kumlaumu kwa kudai
 
Walicheka na huyo kima? Huyo anatakiwa atafutwe na kufungwa.
 
Chombo lilikuwa na bima?
Dereva alikuwa na leseni?
Kosa la Nani?
Unajua kuna kesi mmiliki basi la abiria kutakiwa kulipa fidia abiria walio pata ajali kwenye basi husika?
 
Serikali ikishakuwa legelege mambo kama haya yanakuwa mengi sana

Gali Ina bima na bodaboda Ina bima kwanini asilipwe na bima

Alafu na huyo mke alifuata Nini mahakani kwani kesi inarithiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…