Mwalimu wa tuisheni
JF-Expert Member
- Oct 19, 2019
- 6,602
- 10,801
Wauze gari walipe fidia
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mzee unajua hata Bima imefanyaje kazi? Unafahamu kitu kinaitwa 3rd party? Yaani huyo abiria aliyepata ajali kuna bima ya pikipiki hiyo inamhusu lakini pia kuna bima ya huyo mwenye gari nayo inamhusu. Sasa unabisha nini kusema BIMA haihusiki na chochote.Siku zote ukipata shida inayohusiana na sheria ,wewe tafuta mwana sheria akusaidie vinginevyo utapewa hukumu hata ya mtu mwingine, tatizo ni kutokujua sheria ,kazi ya bima ni kudeal na ajali sio mtu binafsi
Kabisa. Labda kama marehemu hakuwa na BIMA kwenye chombo chake.Kama gari au bodaboda ya matehemu ilikuwa na bima hata third party inatakiwa iwalipe wahusika (third parties) fidia na si kuuza mali zake. Hapa inawezekana chombo cha marehemu hakikuwa na bima.
1.inaonekana gari haikuwa na bima, kama ingekuwa nayo wangedai bimaHii kesi na maamuzi yake ni ya kimagumashi sana.
1. Gari haikuwa na bima ?
2. Deni la marehemu linakwendaje kufidiwa na mjane?
3. Kwanini huyo mhanga alikataa kusaidiwa na marehemu kwa gharama za marehemu akiwa hai then aje kumfungulia mashitaka baadae akidai fidia?
No kama hakuna makando makando na marehemu alikuwa na makosa ya kulipa fidia huwa wanafuata mali zake kupitia msimamizi wa mirathi.Hakuna sheria ya hivyo duniani,mdaiwa ameshakufa na kesi closed
Sasa huo m-picha wa Samia wanaweuweka hapo wa nini? Nchi ina wanafiki sana. Watu wanashindwa kujua shuruba za maisha wanazopata zinasababishwa na uongozi wa CCM?Mjane mmoja aliyejulikana kwa jina la Beatrice Lyimo, mkazi wa Mbezi Makabe, jijini Dar es Salaam, yupo kwenye maumivu makali baada ya mahakama kutoa uamuzi kuwa nyumba yake ipigwe mnada mnamo Machi 10, mwaka huu, ili alipwe fidia abiria aliyekuwa amebebwa na bodaboda kugongwa na gari lililokuwa likiendeshwa na marehemu mumewe, na kusababisha abiria huyo kuvunjika mguu.
Akizungumza na Global TV Online, mjane huyo alisema kuwa baada ya ajali hiyo kutokea maeneo ya Mbezi Magufuli, mumewe alijitolea kuwapeleka hospitali dereva wa bodaboda na abiria, lakini abiria huyo alikataa na kusema kuwa atapelekwa na ndugu zake.
Hata hivyo, mumewe aliendelea kumhudumia dereva wa bodaboda hadi akapona.
Baadaye, walipokea wito kutoka kwa abiria aliyekuwa kwenye bodaboda, na alipokwenda kumuona alimlaumu kwa kutomfuatilia tena.
Mumewe alimueleza kuwa alimwomba kumtibu lakini alikataa, hivyo alidhani kuwa hakuhitaji msaada wake.
Abiria huyo akaomba alipwe shilingi milioni tano, lakini mumewe alikataa na badala yake alipokea barua kutoka kwa mwanasheria wa abiria huyo, akimtaka kulipa fidia ya shilingi milioni 200.
Mumewe aliomba suala hilo liende mahakamani. Shauri lilipofikishwa mahakamani, washtaki hawakufika siku ya kwanza, lakini mumewe alienda.
Kwa bahati mbaya, alipokuwa akirudi nyumbani, alipata ajali mbaya maeneo ya Mbezi Kibanda cha Mkaa na kufariki dunia.
Hivyo, walimuomba mjane huyo kuendelea na kesi, na hatimaye ikaamuliwa kuwa nyumba yake iuzwe kwa thamani ya shilingi milioni 35 ili alipwe fidia ya shilingi milioni 24 kwa abiria aliyekuja kuvunjika mguu, pamoja na shilingi milioni 10 za usumbufu.
Jambo hili linamuumiza sana mjane huyo kwani hana kazi, mumewe amefariki, na pia ana watoto wadogo.
View attachment 3252053
Una utaalam wa sheria? Sheria siyo hisia.Hakuna sheria ya hivyo duniani,mdaiwa ameshakufa na kesi closed
nunueni bima ya vyombo vyenu. mtanishukuru.Mjane mmoja aliyejulikana kwa jina la Beatrice Lyimo, mkazi wa Mbezi Makabe, jijini Dar es Salaam, yupo kwenye maumivu makali baada ya mahakama kutoa uamuzi kuwa nyumba yake ipigwe mnada mnamo Machi 10, mwaka huu, ili alipwe fidia abiria aliyekuwa amebebwa na bodaboda kugongwa na gari lililokuwa likiendeshwa na marehemu mumewe, na kusababisha abiria huyo kuvunjika mguu.
Akizungumza na Global TV Online, mjane huyo alisema kuwa baada ya ajali hiyo kutokea maeneo ya Mbezi Magufuli, mumewe alijitolea kuwapeleka hospitali dereva wa bodaboda na abiria, lakini abiria huyo alikataa na kusema kuwa atapelekwa na ndugu zake.
Hata hivyo, mumewe aliendelea kumhudumia dereva wa bodaboda hadi akapona.
Baadaye, walipokea wito kutoka kwa abiria aliyekuwa kwenye bodaboda, na alipokwenda kumuona alimlaumu kwa kutomfuatilia tena.
Mumewe alimueleza kuwa alimwomba kumtibu lakini alikataa, hivyo alidhani kuwa hakuhitaji msaada wake.
Abiria huyo akaomba alipwe shilingi milioni tano, lakini mumewe alikataa na badala yake alipokea barua kutoka kwa mwanasheria wa abiria huyo, akimtaka kulipa fidia ya shilingi milioni 200.
Mumewe aliomba suala hilo liende mahakamani. Shauri lilipofikishwa mahakamani, washtaki hawakufika siku ya kwanza, lakini mumewe alienda.
Kwa bahati mbaya, alipokuwa akirudi nyumbani, alipata ajali mbaya maeneo ya Mbezi Kibanda cha Mkaa na kufariki dunia.
Hivyo, walimuomba mjane huyo kuendelea na kesi, na hatimaye ikaamuliwa kuwa nyumba yake iuzwe kwa thamani ya shilingi milioni 35 ili alipwe fidia ya shilingi milioni 24 kwa abiria aliyekuja kuvunjika mguu, pamoja na shilingi milioni 10 za usumbufu.
Jambo hili linamuumiza sana mjane huyo kwani hana kazi, mumewe amefariki, na pia ana watoto wadogo.
View attachment 3252053
Kuna jambo nina suspect,marehemu ndie aliyekuwa na mkataba na kampuni ya bima akifa then the contract is avoidable.1.inaonekana gari haikuwa na bima, kama ingekuwa nayo wangedai bima
Sio mtaalam wa sheria ila kwa nijuavyo mali ya familia yaani ya mke na mume haiwezi taifishwa bila consent ya mke.2.Sijajua vizuri hapo kisheria ila kama mali bado ni ya marehemu inatumika kulipa liability zake ambazo anadaiwa.
3.Kusaidiwa ni ubinadamu wa muhusika tu ila kisheria ni anadai fidia kwa maumivu(loss suffered) hivo huwezi kumlaumu kwa kudai
Walicheka na huyo kima? Huyo anatakiwa atafutwe na kufungwa.Kuna boda amegonga mtoto mtaani kwetu. Kamvunja mfupa wa kiungi flani muhimu.
Boda katoa 35,000 tu.
Kasusa kuchangia matibabu mengine, kabadili namba ya simu, hhasivyo na akili anaendelea kufanya kazi jirani na nyumbani kwa mgonjwa.
Angeona hii angekimbia mji.
Pikipiki haina bima, dereva hakuwa na leseni.
Sio mjuzi wa sheria kabisa, lakini, Pana hujuma hapo, malipo ya ajali hufanywa na bima ambayo huwepo kwenye chombo cha moto, kibaya nadhani huyo aliyegongwa ni mchawi mbaya Sana, hilo ni game!, inachezwa na mahakama, na wapuuzi katika kudhulumu.
Serekali izuie ujinga huu.
Naongea kwa kujiamini kama parallegal court clerkUna utaalam wa sheria? Sheria siyo hisia.