Mahakama yaamuru kupigwa mnada nyumba ya mjane ili kumfidia aliyeumia mguu kwa ajali ya bodaboda

Huyo Majeruhi ni mchawi sana alisha mchulia marehemu. Eti alidai hataki kutibiwa na aliyemgonga anataka atibiwe na ndugu zake...
 
Kama gari au bodaboda ya matehemu ilikuwa na bima hata third party inatakiwa iwalipe wahusika (third parties) fidia na si kuuza mali zake. Hapa inawezekana chombo cha marehemu hakikuwa na bima.
Inawezekana kabisa mkuu
 
Kwenye sheria zetu za makosa ya barabarani hakunaga adhabu ya kumhudumia majeruhi.
Hakimu amekuwa na mihemuko mingi mno.
 
kuna uwezekano gari haikuwa na BIMA
kuna NDUGU yangu WAZAZI wake wlilipwa pesa nyingi na MTOTO KIONGOZI MKUBWA awamu ya tatu 7bu alikuwa anaendesha gari haina BIMA akamgonga na kufariki
kesi walichukukia poa kutokana na huyo kiongozi alikuwa ndio TOP awamu hiyo ila km unavyojua wapale wakikomalia lao
ikabidi hilo jambo limalozwe nje ya mahakama kwa kuwalipa FIDIA milioni 35 baba na milioni 35 mama
kuendesha chombo cha moto Bila BIMA kunaweza kukusababishaia hasara kubwa epuka sana hilo jambo
michezo ya mahakamani kulipana FIDIA sijui nini wanawezaga BIMA wenyewe
wewe likikukuta jambo na ukawa huna BIMA inabidi uwe mpole sana
 
Story haijabalance kabisa
Natamani tupate upande wa abiria pia aeleze tukio pia hapo tunaweza kuelewa vizuri kuliko kulaumu maamuzi ya mahakama.
 
Mdaiwa yupo wap hapo?
Mdaiwa anasimama msimamizi wa mirathi na ikibidi kuuza mali basi inayouzwa ni mali ya marehemu na siyo mali ya msimamizi wa mirathi pia kumbuka jukumu kubwa la msimamizi wa mirathi ni kukusanya mali za marehemu ikiwa ni pamoja na madeni anayodai kisha kulipa madeni ya marehemu kama anadaiwa na kilichobaki ndiyo ugaiwa kwa warithi,kesi zinazofutwa za marehemu ni kesi za jinai tu lakini za madai zinaendelea hadi kieleweke.
Ebu jiulize ikiwa marehemu ndiye mdai ina maana mdaiwa hastahili kulipa tena kwa sababu anayemdai amefariki? Ngoja siku likitokea kwa mtu wako wa karibu ndiyo utaelewa.
 
Ujinga huo, sheria gani na mwanasheria gani? Halafu wabongo sisi tabu sana inpotokea ajali nini maana ya bima!?!? Makimbiliaga kutibu kama nani na kivipi? Kila ikitokea ajali ya boda na ndiga assumptions ni kuwa ndiga ndio chombo cha moto kikubwa so kina makosa.

Njoo akate rufaaa. Halafu mume kafa mshtakiwa mke anaingiaje?!?!?!

Ni hayo tu.
 
Unaonekana unajibu kwa nadhalia na kama hujibu hvyo shusha vifungu viinavyosema hvyo
 
aombe appeal .......
 
Mimi ndio maana siamini kama haki inatolewa mahakamani....haki siku zote naipigania mwenyewe kwa njia zangu
 
Kuna watu matatizo yao wanaamini ndo fursa ya kutokea Kama huyo Abiria
 
Hii imekaa kisiasa na hizi sheria hazina utu ndani yake kabisa .

Very sad 😥😥
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…