Mahakama yaamuru kupigwa mnada nyumba ya mjane ili kumfidia aliyeumia mguu kwa ajali ya bodaboda

Mahakama yaamuru kupigwa mnada nyumba ya mjane ili kumfidia aliyeumia mguu kwa ajali ya bodaboda

Hii kesi na maamuzi yake ni ya kimagumashi sana.

1. Gari haikuwa na bima ?
2. Deni la marehemu linakwendaje kufidiwa na mjane?
3. Kwanini huyo mhanga alikataa kusaidiwa na marehemu kwa gharama za marehemu akiwa hai then aje kumfungulia mashitaka baadae akidai fidia?
Inaonekana gari haikuwa na bima.
Deni linalipwa na mali ya marehemu ambayo ndiyo hiyo nyumba.
Na kuhusu madai kwamba aliyejeruhiwa kakataa kuhudumiwa hayo yatakuwa ni maelezo ya utetezi tu.
 
Hakuna Sheria ya hivi duniani kote.

Hata kama gari halikuwa na bima bado hakuna hukumu ya hivi, gari kukosa bima hiyo ni kesi nyingine na ina hukumu yake.

Mwenye makosa alishakufa na kesi imeishia hapo hata kama ingekuwa kesi ya madai.
 
Kesi ya madai inaendelea kama kawaida msimamizi wa mirathi ataendelea nayo kwa niaba ya marehemu na ikitokea upande wa marehemu umeshindwa na kuamuliwa kulipa fidia na ikashikana basi mali za marehemu zitanadiwa

Mlipaji deni ambaye ni marehemu na bank au taasisi ya mkopo imemkopesha marehemu, deni harilithiwi, urithi ni haki ya warithi kisheria na sio deni.

Mikopo ina insurance kwenye dharula kama hizi ambazo ziko nje ya uwezo wa kila mtu.
 
Kama huyo mtu alikatwa mguu, basi apewe hela zake kama fidia.
Kinachosikitisha hapo ni neno 'mjane' lakini haki imetendeka.
Alipwe fidia na nani aliemgonga kafariki vipi MKE abebe adhabu ya kosa la marehemu??
 
Kesi ya madai inaendelea kama kawaida msimamizi wa mirathi ataendelea nayo kwa niaba ya marehemu na ikitokea upande wa marehemu umeshindwa na kuamuliwa kulipa fidia na ikashikana basi mali za marehemu zitanadiwa
Je kama marehem asingekuwa na nyumba ama hilo gari nalo lingekuwa haliwez tengenezeka mahakama na walalamikaji wangeendelea na kesi kwa huyo mjane?ama wangemuhukum vipi huyo mjane ili kulipia hiyo fidia wanayoitaka?
 
Hii kesi na maamuzi yake ni ya kimagumashi sana.

1. Gari haikuwa na bima ?
2. Deni la marehemu linakwendaje kufidiwa na mjane?
3. Kwanini huyo mhanga alikataa kusaidiwa na marehemu kwa gharama za marehemu akiwa hai then aje kumfungulia mashitaka baadae akidai fidia?
Shida ndio hapo, marehemu kafariki, why mjane aendelee na kesi,? Wangetemana nayo
 
Sio mjuzi wa sheria kabisa, lakini, Pana hujuma hapo, malipo ya ajali hufanywa na bima ambayo huwepo kwenye chombo cha moto, kibaya nadhani huyo aliyegongwa ni mchawi mbaya Sana, hilo ni game!, inachezwa na mahakama, na wapuuzi katika kudhulumu.
Serekali izuie ujinga huu.
Hiyo ni uhakika pikipiki haina Bima au walichagua kumalizana kinyemela bila kesi kurepotiwa polisi, na investigation report pamoja na Claims ziende Bima, asilimia kubwa ya pikipiki hazina Bima baada ya kumaliza Bima ya kwanza ya Bure kwenye kununua pikipiki. Lakini wanavyovimba barabarani kama vile wanamkataba na Mungu wakuishi milele.
 
Aisee kumbe ndo maana watu wakigonga usiku wanatembea tu, tena nilikuwa naskia kuwa kuna madereva wakiona ajali inaenda kutokea mbele wanahakikisha haponi.
Hapo Hakimu, mwanasheria na aliyegongwa wote moto utawatafuna - dhuluma kabisa.
 
Je kama marehem asingekuwa na nyumba ama hilo gari nalo lingekuwa haliwez tengenezeka mahakama na walalamikaji wangeendelea na kesi kwa huyo mjane?ama wangemuhukum vipi huyo mjane ili kulipia hiyo fidia wanayoitaka?
Kesi ingeendelea na hukumu ingetolewa,mahakama isingeweza kuacha kuendelea kuisikiliza hiyo kesi kwa sababu yenyewe haiwezi kujua kama mdaiwa anaweza kulipa au la.
 
1). Mimi nikajua kuwa gari yenye bima inapotokea ajali bima ndio inayo cover.

2). Mimi najua dereva ndie anae shtakiwa sasa abiria(mke/mjane) ameshtakiwa kwa kosa gani hapa na mahakama?.
 
Hii kesi na maamuzi yake ni ya kimagumashi sana.

1. Gari haikuwa na bima ?
2. Deni la marehemu linakwendaje kufidiwa na mjane?
3. Kwanini huyo mhanga alikataa kusaidiwa na marehemu kwa gharama za marehemu akiwa hai then aje kumfungulia mashitaka baadae akidai fidia?
Ni tatizo
Na hio ni mahakama ya mwanzo

Iende mahakama kuu hadi rufaa
Pia mkiipata hio hukumu tusome
 
Mlipaji deni ambaye ni marehemu na bank au taasisi ya mkopo imemkopesha marehemu, deni harilithiwi, urithi ni haki ya warithi kisheria na sio deni.

Mikopo ina insurance kwenye dharula kama hizi ambazo ziko nje ya uwezo wa kila mtu.
Kwani wapi hapo umezungumzwa mkopo! Lakini nataka nikufahamishe pia kuhusu shauri la mkopo ni vipi linaweza kuendelea hata pale mdaiwa anapofariki.
Ni kwamba kama mtu anakopa kwenye taasisi ya fedha mkopo unakuwa katika muda maalumu mfano mkopo unatakiwa ulipwe ndani ya miezi 24 basi bima itaulipa mkopo huo pale itapotokea dharura ndani ya muda huo wa mkopo lakini iwapo muda wa mkopo umekwisha na deni halijalipwa basi bima haitahusika na lolote litakalotokea.
Na inapofikia hatua hiyo mara nyingi wakopeshaji wataanza taratibu za kukamata na kuuza mali iliyowekwa kama dhamana lakini kwa upande wa mdaiwa uwa wanapenda kukimbilia mahakamani kuweka pingamizi na kutoa sababu hizi na zile sasa katika hatua hiyo mdaiwa akifariki kabla hajamaliza deni ina maana kesi itaendelea kusikilizwa(msimamizi wa mirathi atahusika) na mali ya mdaiwa itapigwa mnada kulipa deni lake na gharama nyingine za kesi kadri mahakama itakavyoamua,hapo bima haitahusika kwa sababu muda wa mkataba wao ulikuwa umeshakwisha.
 
Hiyo ni uhakika pikipiki haina Bima au walichagua kumalizana kinyemela bila kesi kurepotiwa polisi, na investigation report pamoja na Claims ziende Bima, asilimia kubwa ya pikipiki hazina Bima baada ya kumaliza Bima ya kwanza ya Bure kwenye kununua pikipiki. Lakini wanavyovimba barabarani kama vile wanamkataba na Mungu wakuishi milele.
Lakini ajali husika mwenye gari ndiye aligonga pikipiki na kumjeruhi abiria wa pikipiki na wala siyo pikipiki ndiyo iliyosababisha ajali.
 
Hukumu za Mahakama ni public record aseme hiyo kesi namba Ngapi ilikuwa Mahakama gani watu waisome ila Nina maswali haya:-
1. Baada ya kesi ya traffic kuisha mume alikata Rufaa?
2. Mume alikuwa anaendesha Gari ilikuwa na bima? Yeye Marehemu alikuwa na leseni?
3. Kwenye kesi ya Madai baada ya Uamuzi kutoka walikata Rufaa?
4. Hapa kuna Mirathi tayari msimamizi Wa Mirathi kapokea document zozote za kukamata Mali kutoka Mahakamani ili kukazia Hukumu?!
 
Back
Top Bottom