Mahakama yaamuru kupigwa mnada nyumba ya mjane ili kumfidia aliyeumia mguu kwa ajali ya bodaboda

Mahakama yaamuru kupigwa mnada nyumba ya mjane ili kumfidia aliyeumia mguu kwa ajali ya bodaboda

Hii kesi na maamuzi yake ni ya kimagumashi sana.

1. Gari haikuwa na bima ?
2. Deni la marehemu linakwendaje kufidiwa na mjane?
3. Kwanini huyo mhanga alikataa kusaidiwa na marehemu kwa gharama za marehemu akiwa hai then aje kumfungulia mashitaka baadae akidai fidia?
Hakimu ameshaahidiwa mgao hapo. Hakuna namna nyingine ya kuepukana na huo uhuni.
 
Unaonekana unajibu kwa nadhalia na kama hujibu hvyo shusha vifungu viinavyosema hvyo
Mimi sijibu kinadharia najua kwa sababu mashauri kama hayo nimeshawahi kushughulika nayo,hata hivyo katika kuchangia hoja kama hizi lengo ni kuelimishana kwa kadri ya ufahamu wa mtu mmoja mmoja katika mada husika hapa siyo mahakamani na wala mimi siyo Advocate hadi sijui nikariri vifungu vya sheria kichwani.
Mimi naeleza kwa uzoefu wangu kutokana na yaliyowahi kutokea kwangu kama msimamizi wa mirathi hivyo naomba tuishie hapa kwa leo.
 
Naona watu neno MJANE limewafanya aonekane haki haijatendeka. Kimsingi madai ya "tort" hayaishi kisa mdaiwa kufa. Bali yataendelezwa na ikiwa kuna malipo yatalipwa kutoka kwenye mali za marehemu.

Madai yanayofika mwisho ni jinai tu. Na talaka maana mmoja wa wanandoa akifa madai ya talaka hayana msingi tena.

P.s. Naelewa hisia na sheria ni tofauti. Cha kufanya huyo mama mzee alipofariki angebadili jina la nyumba chap kwa haraka.
 
Huyo mama aanzie TAKUKURU ili hilo faili la hiyo kesi lipitiwe na wanasheria mahiri wa TAKKUKURU. Pili huyo mama aende akatafute usaidizi wa kisheria kwa haya mashirika yanayojitolea ili hao wanasheria waangalie kama yupo ndani ya muda akate rufaa mapema vinginevyo itakula kwake. Kutoa taarifa kwenye vyombo vya habari ni jambo zuri kwani bado kuna watu wema wachache serikalini wanaweza kumsaidia lakini la muhimu zaidi awahi kwa wataalamu wa sheria wamsaidie kukata rufaa na kweka zuio kama yupo ndani ya muda.

Pia kama kuna mwanasheria wa kujitolea humu ndani amtafute ajue msingi wa hiyo kesi na kama anasaidika asaidiwe jamani. Na sio lazima amsaidie kumwakilisha mahakamani bali anaweza akamsaidia hata njia za kufuata ili apte haki yake.
 
Mama aache kulia ajifunge kibwebwe ama sivyo wahuni wataiuza hiyo nyumba. Cha kufanya mama kimbia nenda pale Tanzania Human Rights Commission (THRC) wapo pale Kijitonyama ubavuni mwa chuo cha Usiitawi wa Jamii, wanatoa msaada wa kisheria. Au nenda TAWLA (Tanzania women's Lawyers association) wapo Ilala karibu kabisa na hospitali ya Amana nao pia wanatoa msaada wa kisheria hasa hasa kwa wanawake kama yeye. Mwisho kimbilia mkoani ambako team ya Kisheria ya Mama Samia kwa sasa mkoa wa karibu na yeye mama wako Kilimanjaro. Inatakiwa iwekwe 'Injunction order'. Hili ni zuio la Kisheria kisifanyike chochote kuhusu hiyo nyumba mpaka hatua nyingine za Kisheria ziendelee na kufikia tamati. Fanya hivyo mama kama uko humu JF. Au wewe mwandishi wa habari uliye muhoji mfikishie habari. Ama sivyo wahuni wata 'kula' hiyo nyumba.
 
Kuna uwezekano mkubwa hii ajali haikuhusisha hata traffic kupima ni walimalizana kishkaji wenyewe barabarani.
 
Lakini ni bora tungesikiliza upande wa mahakama pia nao wanasemaje kabla ya kuhukumu kwamba mama kaonewa.

Ila mahakama na nyie mna roho mbaya aseee! Nyumba iuzwe 35, mdai apewe 24, usumbufu 10.

35 - 24 = 11.
11 - 10 = 1.

Hii ni ubaya ubwela, yaani mjane na watoto warithi million moja tu.

Uzeni hata million 40 mzee.
 
Kuna uwezekano mkubwa hii ajali haikuhusisha hata traffic kupima ni walimalizana kishkaji wenyewe barabarani.
Kuna boya mmoja hivi hivi aligongwa na gari tena zebra crossing.

Yule dada aliegonga akawa amepanic sababu anajua amegonga mtu zebra. Akawa anambembeleza jamaa ampeleke hospitali.

Lile jamaa lililogongwa badala ya kutaka hata lipelekwe hospitali, likadai hela laki moja taslimu.

Yule dada chap kazama kwenye gari, kachukua kipochi, kahesabu chwa chwaa chwaaa akalipa bila hata kubisha.

Jamaa linakenua meno, linajiona limewin, dada kawasha chombo kaondoka(bila hata kutoa walakuchukua namba)

Yule boya akawaita walevi wengie wakaanza kuvipiga visungura mpaka usiku kalala.

Kesho yake kaamka guuuu limevimba kama la tembo, linauma kama mapenzi, hapo ndio akili ilimkaa sawa.
 
Hakuna sheria ya hivyo duniani,mdaiwa ameshakufa na kesi closed
Kesi ya madai hii siyo jinai kwa uelewa wangu mdogo wa sheria. Kwa maana hiyo warithi au msimamizi wa mirathi walitambue hilo.

Kwenye kukusanya mali ya marehemu si nyumba wala viwanja bali kama marehemu alikuwa anadai au kudaiwa.
 
Mjane mmoja aliyejulikana kwa jina la Beatrice Lyimo, mkazi wa Mbezi Makabe, jijini Dar es Salaam, yupo kwenye maumivu makali baada ya mahakama kutoa uamuzi kuwa nyumba yake ipigwe mnada mnamo Machi 10, mwaka huu, ili alipwe fidia abiria aliyekuwa amebebwa na bodaboda kugongwa na gari lililokuwa likiendeshwa na marehemu mumewe, na kusababisha abiria huyo kuvunjika mguu.
Bima ina kazi gani
 
Kesi ya madai hii siyo jinai kwa uelewa wangu mdogo wa sheria. Kwa maana hiyo warithi au msimamizi wa mirathi walitambue hilo.

Kwenye kukusanya mali ya marehemu si nyumba wala viwanja bali kama marehemu alikuwa anadai au kudaiwa.
Kesi haikuwa imefika mwisho hivyo marehemu labda alikuwa na utetezi kuhusu hiyo kesi sasa hayupo
 
Kesi inafikirisha sana. Kesi iliendeshwaje ilihali mshitakiwa kashafariki? Hukumu kasomewa nani wakati mshitakiwa kashafariki? Mahakama imeridhikaje kuwa ni marehemu ndiye hasa alimgonga? Mjane kaingiaje kwenye kesi isiyomhusu?
 
Siku zote ukipata shida inayohusiana na sheria ,wewe tafuta mwana sheria akusaidie vinginevyo utapewa hukumu hata ya mtu mwingine, tatizo ni kutokujua sheria ,kazi ya bima ni kudeal na ajali sio mtu binafsi
Wewe ndio haujui.
 
Kesi haikuwa imefika mwisho hivyo marehemu labda alikuwa na utetezi kuhusu hiyo kesi sasa hayupo
Ndio familia wakate rufaa kutia huruma kama mjane haitowasaidia,msimamizi wa mirathi asimamie kesi
 
Back
Top Bottom