Mahakama yaamuru kupigwa mnada nyumba ya mjane ili kumfidia aliyeumia mguu kwa ajali ya bodaboda

Yani kwakifupi huyo mjane hatopata chochote aisee.. Hee! Nyie dunia hii ina mitihani
 
Najua inauma ,also nimeumia ila daaah. Naomba niwajibu ndugu zangu hili kisheria, Mama kakosa kila kitu wala asikate rufaa. Ila apambane hiyo nyumba iuzwe gharama zaidi mbona nyumba nzuri.

Katika hali kama hii, kuna mambo kadhaa ya kisheria yanayoweza kutokea kulingana na mazingira ya kesi:
1. Kesi ya Jinai (Kama Ipo) – Ikiwa dereva wa gari alikuwa anashtakiwa kwa kosa la jinai, kama vile uzembe au kuendesha gari kwa hatari, kesi hiyo itafutwa kwa sababu mshitakiwa amefariki. Katika sheria za jinai, mtu hawezi kuhukumiwa baada ya kufariki.

2. Kesi ya Madai (Kama Ipo) – Ikiwa aliyepata majeraha alikuwa amewasilisha kesi ya madai ya fidia dhidi ya mtuhumiwa, kesi inaweza kuendelea lakini italenga mali ya marehemu. Familia ya mwathiriwa au aliyepata majeraha anaweza kuwasilisha madai dhidi ya mali ya marehemu (estate) ikiwa alikuwa na bima au mali nyingine inayoweza kufidia hasara iliyotokea.

3. Bima ya Gari – Ikiwa gari lilikuwa na bima, mwathiriwa anaweza kupata fidia kutoka kwa kampuni ya bima ya gari lililosababisha ajali, bila kujali kama dereva aliyesababisha ajali amefariki.

4. Hatima ya Kesi Mahakamani – Mahakama itapokea taarifa ya kifo cha mtuhumiwa na inaweza kuifuta kesi ya jinai, lakini ikiwa kuna upande wa madai wa kifedha, basi watazamwa waliokuwa warithi wa marehemu na mali zake.

Kwa hiyo, hatma ya kesi inategemea kama ni ya jinai au madai, na pia uwepo wa bima na mali za mtuhumiwa.
Daaah namuonea huruma sana dada yangu huyu ila daaah.
 
Mjane mmoja aliyejulikana kwa jina la Beatrice Lyimo, mkazi wa Mbezi Makabe, jijini Dar es Salaam, yupo kwenye maumivu makali baada ya mahakama kutoa uamuzi kuwa nyumba yake ipigwe mnada mnamo Machi 10, mwaka huu, ili alipwe fidia abiria aliyekuwa amebebwa na bodaboda kugongwa na gari lililokuwa likiendeshwa na marehemu mumewe, na kusababisha abiria huyo kuvunjika mguu.

Akizungumza na Global TV Online, mjane huyo alisema kuwa baada ya ajali hiyo kutokea maeneo ya Mbezi Magufuli, mumewe alijitolea kuwapeleka hospitali dereva wa bodaboda na abiria, lakini abiria huyo alikataa na kusema kuwa atapelekwa na ndugu zake.

Hata hivyo, mumewe aliendelea kumhudumia dereva wa bodaboda hadi akapona.

Baadaye, walipokea wito kutoka kwa abiria aliyekuwa kwenye bodaboda, na alipokwenda kumuona alimlaumu kwa kutomfuatilia tena.

Mumewe alimueleza kuwa alimwomba kumtibu lakini alikataa, hivyo alidhani kuwa hakuhitaji msaada wake.

Abiria huyo akaomba alipwe shilingi milioni tano, lakini mumewe alikataa na badala yake alipokea barua kutoka kwa mwanasheria wa abiria huyo, akimtaka kulipa fidia ya shilingi milioni 200.

Mumewe aliomba suala hilo liende mahakamani. Shauri lilipofikishwa mahakamani, washtaki hawakufika siku ya kwanza, lakini mumewe alienda.

Kwa bahati mbaya, alipokuwa akirudi nyumbani, alipata ajali mbaya maeneo ya Mbezi Kibanda cha Mkaa na kufariki dunia.

Hivyo, walimuomba mjane huyo kuendelea na kesi, na hatimaye ikaamuliwa kuwa nyumba yake iuzwe kwa thamani ya shilingi milioni 35 ili alipwe fidia ya shilingi milioni 24 kwa abiria aliyekuja kuvunjika mguu, pamoja na shilingi milioni 10 za usumbufu.

Jambo hili linamuumiza sana mjane huyo kwani hana kazi, mumewe amefariki, na pia ana watoto wadogo.

View attachment 3252053
Avumilie.

Awaombe wasamaria wema wamlipie deni hilo.

Sheria ni msumeno!
 
Hakuna kitu kama hicho mkuu
Wabongo wengi hawajui chochote kuhusu sheria na isitoshe mtu mwingine hajasoma hata hiyo habari yenyewe lakini anakazana kubishana tu! Utasikia mtu anasema eti inakuwaje aliyegonga ni marehemu halafu ashitakiwe mjane yaani hata hajui hiyo kesi imeanzaje! Mara mwingine utasikia mdaiwa akifariki kesi ndiyo imeisha na deni limekufa! Sasa utajitahidi kueleza lakini wapi mtu haelewi anajifanya yeye ni mjuaji kumbe boya tu.
 
Waelez
 
Hata habari yenyewe imeandikwa kinazi! Eti "Mahakama yaamuru nyumba ya mjane kupigwa mnada................!
Hakuna mahakama inaweza kufanya ujinga wa namna hiyo kwamba iamuru nyumba ya mtu mmoja ipigwe mnada kufidia deni la mtu mwingine hata kama wana uhusiano wa namna gani.
Habari sahihi ni Mahakama imeamuru nyumba ya Marehemu kuuzwa kulipa deni analodaiwa.
Watu watambue msimamizi wa mirathi anawajibika kulipa madeni yote ya marehemu na kilichobaki ndiyo anakigawa kwa warithi na ndiyo maana mirathi ikienda kufunguliwa mahakamani inatakiwa itangazwe kwa siku 90 ili yeyote mwenye pingamizi au maslahi kwenye mali ya marehemu ajitokeze lakini hata kama ndani ya muda huo hakuna aliyejitokeza haina maana kwamba baada ya hapo mtu anayemdai marehemu haruhusiwi tena kujitokeza.
 
Siku zote ukipata shida inayohusiana na sheria ,wewe tafuta mwana sheria akusaidie vinginevyo utapewa hukumu hata ya mtu mwingine, tatizo ni kutokujua sheria ,kazi ya bima ni kudeal na ajali sio mtu binafsi
Pamoja na kutokujua Sheria lakini mahakama inatakiwa kutenda haki kama taratibu zinavyotaka.
 
Sio mjuzi wa sheria kabisa, lakini, Pana hujuma hapo, malipo ya ajali hufanywa na bima ambayo huwepo kwenye chombo cha moto, kibaya nadhani huyo aliyegongwa ni mchawi mbaya Sana, hilo ni game!, inachezwa na mahakama, na wapuuzi katika kudhulumu.
Serekali izuie ujinga huu.
Kabisa naona hapo kuna kitu hakipo sawa, uchawi na ushirikina plus sheria kupindishwa
 
Kama huyo mtu alikatwa mguu, basi apewe hela zake kama fidia.
Kinachosikitisha hapo ni neno 'mjane' lakini haki imetendeka.
Umekula maharage ya wapi leo
Vipi huyu mjane Angekua amepanga chumba cha elfu 30 si ungetaka na yeye avunjwe miguu yote au auawe?
 
For what is worth, kesi ya madai inakosa nguvu pale mdai au mdaiwa anapofariki.
 
Mjane mmoja aliyejulikana kwa jina la Beatrice Lyimo, mkazi wa Mbezi Makabe, jijini Dar es Salaam, yupo kwenye maumivu makali baada ya mahakama kutoa uamuzi kuwa nyumba yake ipigwe mnada mnamo Machi 10, mwaka huu, ili alipwe fidia abiria aliyekuwa amebebwa na bodaboda kugongwa na gari lililokuwa likiendeshwa na marehemu mumewe, na kusababisha abiria huyo kuvunjika mguu.

Akizungumza na Global TV Online, mjane huyo alisema kuwa baada ya ajali hiyo kutokea maeneo ya Mbezi Magufuli, mumewe alijitolea kuwapeleka hospitali dereva wa bodaboda na abiria, lakini abiria huyo alikataa na kusema kuwa atapelekwa na ndugu zake.

Hata hivyo, mumewe aliendelea kumhudumia dereva wa bodaboda hadi akapona.

Baadaye, walipokea wito kutoka kwa abiria aliyekuwa kwenye bodaboda, na alipokwenda kumuona alimlaumu kwa kutomfuatilia tena.

Mumewe alimueleza kuwa alimwomba kumtibu lakini alikataa, hivyo alidhani kuwa hakuhitaji msaada wake.

Abiria huyo akaomba alipwe shilingi milioni tano, lakini mumewe alikataa na badala yake alipokea barua kutoka kwa mwanasheria wa abiria huyo, akimtaka kulipa fidia ya shilingi milioni 200.

Mumewe aliomba suala hilo liende mahakamani. Shauri lilipofikishwa mahakamani, washtaki hawakufika siku ya kwanza, lakini mumewe alienda.

Kwa bahati mbaya, alipokuwa akirudi nyumbani, alipata ajali mbaya maeneo ya Mbezi Kibanda cha Mkaa na kufariki dunia.

Hivyo, walimuomba mjane huyo kuendelea na kesi, na hatimaye ikaamuliwa kuwa nyumba yake iuzwe kwa thamani ya shilingi milioni 35 ili alipwe fidia ya shilingi milioni 24 kwa abiria aliyekuja kuvunjika mguu, pamoja na shilingi milioni 10 za usumbufu.

Jambo hili linamuumiza sana mjane huyo kwani hana kazi, mumewe amefariki, na pia ana watoto wadogo.

View attachment 3252053
Atafute wana sheria wa stay execution afu afanye revision kwenye kesi ya msingi, katika hali ya kawaida madai yatokansyo na Sheria ya madhara tort hayarisishwi kama ilivyo kwa makosa ya jinai, mtuhumiwa akifa anakua na makosa yake
 
Mjane mmoja aliyejulikana kwa jina la Beatrice Lyimo, mkazi wa Mbezi Makabe, jijini Dar es Salaam, yupo kwenye maumivu makali baada ya mahakama kutoa uamuzi kuwa nyumba yake ipigwe mnada mnamo Machi 10, mwaka huu, ili alipwe fidia abiria aliyekuwa amebebwa na bodaboda kugongwa na gari lililokuwa likiendeshwa na marehemu mumewe, na kusababisha abiria huyo kuvunjika mguu.

Akizungumza na Global TV Online, mjane huyo alisema kuwa baada ya ajali hiyo kutokea maeneo ya Mbezi Magufuli, mumewe alijitolea kuwapeleka hospitali dereva wa bodaboda na abiria, lakini abiria huyo alikataa na kusema kuwa atapelekwa na ndugu zake.

Hata hivyo, mumewe aliendelea kumhudumia dereva wa bodaboda hadi akapona.

Baadaye, walipokea wito kutoka kwa abiria aliyekuwa kwenye bodaboda, na alipokwenda kumuona alimlaumu kwa kutomfuatilia tena.

Mumewe alimueleza kuwa alimwomba kumtibu lakini alikataa, hivyo alidhani kuwa hakuhitaji msaada wake.

Abiria huyo akaomba alipwe shilingi milioni tano, lakini mumewe alikataa na badala yake alipokea barua kutoka kwa mwanasheria wa abiria huyo, akimtaka kulipa fidia ya shilingi milioni 200.

Mumewe aliomba suala hilo liende mahakamani. Shauri lilipofikishwa mahakamani, washtaki hawakufika siku ya kwanza, lakini mumewe alienda.

Kwa bahati mbaya, alipokuwa akirudi nyumbani, alipata ajali mbaya maeneo ya Mbezi Kibanda cha Mkaa na kufariki dunia.

Hivyo, walimuomba mjane huyo kuendelea na kesi, na hatimaye ikaamuliwa kuwa nyumba yake iuzwe kwa thamani ya shilingi milioni 35 ili alipwe fidia ya shilingi milioni 24 kwa abiria aliyekuja kuvunjika mguu, pamoja na shilingi milioni 10 za usumbufu.

Jambo hili linamuumiza sana mjane huyo kwani hana kazi, mumewe amefariki, na pia ana watoto wadogo.

View attachment 3252053
 
Kuna mahala hapako sawa kisheria hapo Mjane akate rufaa, wakowapi wale mawakili wakujitolea wamsaidie huyu Mjane? Tamwa wapo wapi wamsaidie mjane? ikiachwa hivyo mengi yataibuka zaidi ya hilo na kwa wengine hasa wale amabao hawaja weza kufikiwa na vyombo vya habari na mambo yakaisha.
 
Back
Top Bottom