Mahakama yamwamuru Lissu kufika mahakamani

Mahakama yamwamuru Lissu kufika mahakamani

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemwamuru kufika mahakamani mbunge wa zamani wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na wenzake watatu, wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi, Septemba 14, mwaka huu, baada ya jana kushindwa kufika kusikiliza kesi yake.

Amri hiyo ilitolewa jana na mahakama hiyo iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, kesi hiyo ilipopangwa kwa ajili ya kutajwa.

Awali, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, alidai shauri lilipangwa kwa kutajwa na kwamba mshtakiwa Lissu, hakufika kusikiliza kesi yake.

Mdhamini wa Lissu, Robert Katula, alidai mshtakiwa aliwasiliana naye juzi asubuhi na kumueleza kwamba yuko mkoani anatafuta wadhamini kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka huu.

Hakimu Simba, alimtaka mdhamini huyo kuhakikisha mshtakiwa anafika mahakamani na sio kutoa sababu ambazo sio za kisheria.

"Mdhamini hizo sababu hazikubaliki kisheria tusiikosee sheria, sisi ni watekelezaji wa sheria ambapo tunatoa amri. Ukisema unaiachia mahakama tunaweza kusema ulipe dhamana na ukishindwa unakwenda jela hatutaki kufika huko, wewe hakikisha unamleta mshtakiwa tarehe ijayo," alisema.

Hata hivyo, wadhamini wa Lissu waliomba mahakama kujitoa katika udhamini kwasababu wanayemdhamini hana ushirikiano mzuri na wadhamini wake na mahakama iliwaeleza kuwa kisheria mdhamini akitaka kujitoa lazima kwanza anamleta mshtakiwa halafu ndiyo aweze kujitoa.

Kwa upande wa mshtakiwa wa tatu ambaye hakufika mahakamani Mehbooh, ilidaiwa na mdhamini wake kuwa ni mgonjwa na kuwasilisha fomu mahakamani hapo.

Hakimu Simba baada ya kusema hayo, alimtaka mdhamini wa Lissu ahakikishe mshtakiwa huyo anafika mahakamani hapo tarehe ijayo na sio vinginevyo.

Mbali na Lissu washtakiwa wengine ni, Wahariri Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh.

Katika kesi ya msingi kwa pamoja washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matano ikiwamo kuandika habari za uchochezi kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.

Ilidaiwa kuwa kati ya Januari 12 hadi 14, 2016 jijini Dar es Salaam, washtakiwa Jabir, Mkina na Lissu, waliandika na kuchapisha taarifa za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar.’

Katika shtaka la pili wanadaiwa kuwa Januari 14, 2016 walichapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa wananchi wa Zanzibar.

Mshtakiwa Mehboob anadaiwa kuwa Januari 13 ,2016 katika jengo la Jamana lililopo Manispaa ya Ilala, alichapisha gazeti la Mawio lililokuwa na taarifa za uchochezi.

Ilidaiwa kuwa mshtakiwa huyo pia alichapisha gazeti hilo bila ya kuwasilisha hati ya sheria ya kiapo kwa Msajili wa Magazeti.
 
Mahakama ndio tuseme hawaoni kuwa anatafuta wadhamini kitendo ambacho kina time limit? Mbona hizo kesi zilizokuwepo hawazisikilizi wanawapiga watuhumiwa tarehe tu na kuwarejesha Segerea.

Upinzani ukichukuwa nchi mwaka wowote, hakuna kuwasamehe wale wote waliotumia madaraka yao vibaya. Wanafanya hivyo kwa utashi wao binafsi na kinyume cha kiapo cha maadili. Piga chini mahakimu na majaji wote watakaonekana wamekiuka kufata sheria ya maadili ya umma.
 
Hoja za utetezi zinazokwenda mahakamani zinakosa mashiko, inamaana Mh Lissu hajui hizi Sheria au kuna kitu cha ziada anakitafuta.

Mahakama itakapokuja kutoa kibali cha kukamatwa wasije wanaharakati wakasema kuwa anaonewa na kile kinachodaiwa kuwa ni mbinu chafu za CCM wakati ni dhahiri kabisa mh Lissu anadharau mahakama bila kificho.

=====

News Alert: - Mahakama yamwamuru Lissu kufika mahakamani
 
Magufuli kama Magufuli hawezi siasa za ushindani, na kwa muundo wa katiba yetu rais ndio anaagiza mahakama ifanye vipi kazi. Kwa vyovyote vile Magufuli hawezi kukubali ushindani toka kwa Lisu, wakati ana uwezo kabisa wa kuitumia mahakama kumzuia mshindani wake. Kwa sasa hivi hiyo mahakama iko kwenye mbinyo mkubwa ili itumike kumdhibiti Lisu. Na kwa uhakika hata hukumu imeshapangwa iwe vipi.
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemwamuru kufika mahakamani mbunge wa zamani wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na wenzake watatu, wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi, Septemba 14, mwaka huu, baada ya jana kushindwa kufika kusikiliza kesi yake.

Amri hiyo ilitolewa jana na mahakama hiyo iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, kesi hiyo ilipopangwa kwa ajili ya kutajwa...
kWA KILA kinachotaka kufanyika na CCM na hawa watawala Tanzania kuna dalili ya Zimbabwe ijayo, na wanajua kabisa, wanajidanganya sana. Zimbabwe ilkuwa strong, ila hii Tanzania iwekewe hivyo vikwazo mnawezi kurudi ule wakati kupanga foleni kunua sukari na unga wenye muhogo. POLENI SANA
 
Hoja za utetezi zinazokwenda mahakamani zinakosa mashiko, inamaana Mh Lissu hajui hizi Sheria au kuna kitu cha ziada anakitafuta.

Mahakama itakapokuja kutoa kibali cha kukamatwa wasije wanaharakati wakasema kuwa anaonewa na kile kinachodaiwa kuwa ni mbinu chafu za CCM wakati ni dhahiri kabisa mh Lissu anadharau mahakama bila kificho.

=====

News Alert: - Mahakama yamwamuru Lissu kufika mahakamani
Kwa hili la kutokwenda mahakamani hata mimi sikubaliani nalo kabisa, tuwe mfano kuheshimu mahakama tusibaki kulalamika serikali haiheshimu mahakama na wakati na sisi ni walewale.
 
Najua Tundu hawezi na hana sifa ya kuwa no. 1 wetu. Lkn kwa matendo haya dhidi ya mahakama ni mfano hai wa nchi kusadikika atakayoiongoza bwana huyu. Mbinafsi, mbishi, mwenye dharau na asiye na chembe ya staha kwa wenzake.

Naishangaa mahakama nayo kwa kufumbia macho hii contempt of court anayofanya msomi huyu wa kufikirika tena kwenye kesi ya jinai. Kwa nn hakimu asisikilize mashauri ya Lissu expatre?

Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app
 
Magufuli kama Magufuli hawezi siasa za ushindani, na kwa muundo wa katiba yetu rais ndio anaagiza mahakama ifanye vipi kazi. Kwa vyovyote vile Magufuli hawezi kukubali ushindani toka kwa Lisu, wakati ana uwezo kabisa wa kuitumia mahakama kumzuia mshindani wake. Kwa sasa hivi hiyo mahakama iko kwenye mbinyo mkubwa ili itumike kumdhibiti Lisu. Na kwa uhakika hata hukumu imeshapangwa iwe vipi.
hiyo hukumu iweke hapa tuisome!
 
Kwa hili la kutokwenda mahakamani hata mimi sikubaliani nalo kabisa, tuwe mfano kuheshimu mahakama tusibaki kulalamika serikali haiheshimu mahakama na wakati na sisi ni walewale.
Ni tatizo kubwa sana hili
 
Back
Top Bottom