Tumia fuvu lako vyema, abuse and misuse of your tiny brain trying to pull some stinky trolls won't doKwahiyo huyo jamaa unamfahamu vizuri?
Yeye pikipiki ya marehemu aliitoa wapi ndani ya masaa yasiyozidi 12?
Majaji watatu wakiongozwa na Jaji Mkuu.....Mahakama ya Rufani Morogoro, imetupilia mbali rufani ya Justine Chamashine aliyehukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kumuua dereva wa bodaboda, Joseph Frorence 'Msimbe'.
Uamuzi huo ulitolewa wiki iliyopita na Jopo la Majaji watatu likiongozwa na Jaji Mkuu Profesa Ibrahimu Juma. Majaji wengine ni Augustine Mwarija na Othman Makungu.
Chamashine alikata rufani kupinga hatia na adhabu aliyopewa na Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam. Majaji hao walisema baada ya kupitia hoja za pande zote mbili wamebaini hoja za rufani hazina mashiko
na Mahakama Kuu ilimhukumu mrufani kwa usahihi. Walibainisha miongoni mwa hoja za mrufani kupinga adhabu hiyo ilikuwa ni kwamba Mahakama Kuu ilikosea kumhukumu kwa kutumia ushahidi wa kukutwa na vitu vya marehemu huku kukiwa hakuna ushahidi iwapo wakati Msimbe anauawa alikuwa akitumia pikipiki aliyokutwa nayo yeye.
Pia, alidai hakuna ushahidi wa malalamiko unaomuunganisha mrufani na pikipiki iliyoibwa kwasababu upande wa Jamhuri umeshindwa kumuita Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuthibitisha umiliki wake.
Wakizichambua hoja hizo, Majaji walisema Jaji wa Mahakama Kuu alikuwa sahihi kusema mrufani ndiye aliyemuua Msimbe. Aidha, walisema ushahidi unaonyesha mrufani alikamatwa na polisi akiwa anamiliki pikipiki hiyo ilithibitishwa na mmiliki wake halali ambaye alimkabidhi Msimbe kufanya biashara ya kubeba abiria Januari 6, mwaka 2017.
Ilielezwa Januari 9, mwaka 2017, Msimbe aliuawa na siku iliyofuata saa 7:30 mchana askari walimkamata mrufani akiwa anaendesha pikipiki hiyo, ndipo walipomfungulia shtaka la mauaji kwasababu alikutwa na pikipiki iliyokuwa inaendeshwa na Msimbe.
Majaji hao walisema kwa ushahidi huo, hawaoni hitimisho lingine isipokuwa kama Jaji wa mahakama ya chini alivyoeleza kwamba mrufani alihusika na mauaji ya Msimbe na kuiba pikipiki.
Majaji hao walisema kutokana na hali hiyo wameona hoja za mrufani hazina mashiko, hivyo wanaitupa rufani kama ilivyokatwa. Chamashine alitenda kosa hilo, Januari 9, mwaka 2017, eneo la Kikwaraza, Kata ya Mikumi, Wilaya ya Kilosa, Morogoro.
Sahihi kabisa.Kuna kitu cha kujifunza hapa.
Unadhani aliyeua ni mpumbavu kiasi cha kuendesha pikipiki ya marehemu kesho yake?Yan Leo pikipiki ipotee kesho ukutwe nayo wewe, mnataka kusema nin nyie huko juu mnaotetea, huyu ni muuaji,kama sio basi kahusika na anawajua wauaji awataje wakapumzike wote huko.
Nyumban kwetu sisi ni njian kuna siku usiku tunakula tukawatunasikia watu wanabishana hiv ila tunasikia kwa mbali yan tunakuja kushtuka yule boda anapiga kelele za msaada tunafika pale kashakatwa katwaapanga, kichwan, mabegan na mikononi, wezi wabayaa saaana
Kwamba aliipataje? hilo swali Mahakama haikuliuliza na zaidi hata Mahakama ilipoombwa TRA waitwe kuthibitisha umiliki haikutoa nafasi hiyo.Aliiipataje pikipiki ya marehemu ,masaa 24 baada ya kuwawa?
Pikipiki aibe leo kwa kumuua mtu halafu kesho atembee nayo mitaani ! Hii nayo imekaa sawa?, ni mwizi gani anaweza kufanya kosa la namna hiyo?Yan Leo pikipiki ipotee kesho ukutwe nayo wewe, mnataka kusema nin nyie huko juu mnaotetea, huyu ni muuaji,kama sio basi kahusika na anawajua wauaji awataje wakapumzike wote huko.
Nyumban kwetu sisi ni njian kuna siku usiku tunakula tukawatunasikia watu wanabishana hiv ila tunasikia kwa mbali yan tunakuja kushtuka yule boda anapiga kelele za msaada tunafika pale kashakatwa katwaapanga, kichwan, mabegan na mikononi, wezi wabayaa saaana
Unaishi Tanzania ipi mkuu?? Ukipeleka polisi ushaidi wewe ndo unakuwa mtuhumiwa ,Piki piki inaokotwaje?
Kama aliiokota angeipeleka polisi
Acha apigwe kutanzi
Halafu watu ni maajabu sana, unamwua mtu kwa ajiri ya kumpora pikipiki tu.Piki piki inaokotwaje?
Kama aliiokota angeipeleka polisi
Acha apigwe kutanzi
Kuna series of misfortunes zikikuandama unaweza jikuta umeingia kwenye matatizo makubwa kwa bahati mbaya , kuna uwezekano kuwa jamaa ni mnunuzi maarufu wa vitu vya mazabe, akaletewa pikipiki hiyo akanunua kwa bei chee bila kujua msala wake.Aliiipataje pikipiki ya marehemu ,masaa 24 baada ya kuwawa?
Sina shida na hukumu kama ni kweli aliyekamatwa ni muuaji halisi.Halafu watu ni maajabu sana, unamwua mtu kwa ajiri ya kumpora pikipiki tu.
Toka hapo unaanza kuishi maisha ya wasiwasi tele.
Ndio maana wanahukumiwa adhabu kali
Rough justice, sio wote waliopo jela ni wahalifu , kuna innocents pia .Acha tu, nimejiuliza maswali mengi sana
Hiyo ni common sense !! Bahati mbaya sana watanzania hatuna uwezo wa kutumia common sense , akili ya mwanzo kabisa ambayo mwanadamu kapewa bure kabisa bila ya kwenda darasani.Muuaji hawezi UA, akachukua pikipiki afu kesho aiendeshe maeneo hayo hayo
Matukio yote ya uporaji kitu kikiibiwa,hakiuzwi mtaa huo wala hakitatumika mtaa huo.Hiyo ni common sense !! Bahati mbaya sana watanzania hatuna uwezo wa kutumia common sense , akili ya mwanzo kabisa ambayo mwanadamu kapewa bure kabisa bila ya kwenda darasani.
Unaona hata kwenye huu mjadala baadhi ya watu hawajaitumia common sense , wanahukumu tu .bila kuhoji
Awataje basi waliomuuzia pikipikiMuuaji hawezi UA, akachukua pikipiki afu kesho aiendeshe maeneo hayo hayo
Yeye aliomba TRA waje thibitisha umiliki wa pikipiki, TRA hawajatokeaAwataje basi waliomuulizia pikipiki
Mmmhh, aisee🤔Yeye aliomba TRA waje thibitisha umiliki wa pikipiki, TRA hawajatokea