Mahakama yatengua hukumu ya kina Mwana-FA, AY na Kampuni ya tiGO

Jamaa he
Halafu kuna milamba matako humu ilisema hawa mafala walishapewa hiyo hela...

Masikini wale
Jamaa hela walishapewa. Tigo hawakukata rufaa ndani ya muda wa rufaa, wakalipa baada ya account zao kukamatwa. Wakaomba kibali cha kukata rufaa nje ya muda wa rufaa. Wakapata ndipo wakakata rufaa.
 
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Kwani wao walilipwa kidogokidogo? Tena walizuia akaunti. Ngoma ngumu hii mkuu.
Lakini tukumbuke kwamba pamoja na yote haya, haiondoi ukweli kwamba tigo iliwaibia jamaa kwasababu mpaka sahizi hawana hoja/ushaidi kwamba walizitumia zile nyimbo kihalali ila wana hoja moja tu ya kiutendaji ya mahakama/sheria ambayo haiingilii kwenye kesi yenyewe hasa!
 
Tigo kanunua kwa dalali aseee.
 
Mwana FA ashaenda Sana OLD Trafford kucheki game za MAN UTD πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚!

Kimsingi Tigo wakaushe tu wajue walishapigwa tu mapema.
🀣🀣
...Na ukimpa kazi ya kukuchambulia kikosi cha Ole Gunnar...Edo Kumwembe na George Ambangile hawatii miguu...
 
Huyo hakimu ni marehemu kwa Sasa.

Na kilichomtokea ni kuvuta mpunga kwa wadaawa (wanaoshtakiana) halafu hakutoa maamuzi yanayowafurahisha.

Jamaa kumfuata na kumuuliza kwanini katoa hukumu ya aina hiyo, akawajibu mbovu.

Wakamtengeneza, baada ya siku kadhaa jamaa kaugua, ikawa safari.
 
Sasa hapo hasara itakuwa Kwa hao vijana, maana waliopewa mgao kama mawakili na wadau hawawawezi kurudisha pesa. Hapo mwana FA na AY inabidi wahangaike wenyewe ikiwemo kuwalipa mawakili upya. Nilichogundua mawakili wengi ni watoto WA mjini
Msando ndo alikuwa wakili wao.
 
Unaumia jamaa kupiga hela ka wamekuibia mke. Umasikini mbaya sana.

Kama mbingu ipo naamaini watajaa matajiri tu.
Cha msingi tuangalie namna gani tunaweza wafungulia kesi za wizi wa zile cent wanazojimegeaga ukiacha salio bila kujiunga kifurushi. Fidia yangu wakinilipa hata Mil. 100 tu inantosha. Nilegeze vyuma tu.
 
Lakin kumbuka walichelewa kukata tufaa(obviously walikubali kulipa) then akatokea mtu akawapanga wakakata rufaa nje ya muda wa rufaa.
 
Mwana FA ashaenda Sana OLD Trafford kucheki game za MAN UTD πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚!

Kimsingi Tigo wakaushe tu wajue walishapigwa tu mapema.
Mashabiki wenzie 500 ya kibanda umiza kwa Ujugu Arena hawana,wanasubiri matokeo,yeye anaenda muona Lingaard akitoa boko Old Trafford.
 
Mkuu deni linafunga kwa mtindo ule ule AY na FA waliotumia kukamata akaunti za tigo. Muhimu hukumu iwe imetoka kwa faida yako wewe unayedai. Wanaita civil prisoner, lengo ni kukutia presha ulipe deni la watu.

Ndo itabidi washike mali zenye thamani ya 2B za hao jamaa napo ni kama wanazo hizo mali kwa majina yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…