Mahakama yatengua hukumu ya kina Mwana-FA, AY na Kampuni ya tiGO

Deni halifungi hizo jambajamba tu tena sasa FA mbunge ndo haguswi kabisa.
Mkuu deni linafunga kwa mtindo ule ule AY na FA waliotumia kukamata akaunti za tigo. Muhimu hukumu iwe imetoka kwa faida yako wewe unayedai. Wanaita civil prisoner, lengo ni kukutia presha ulipe deni la watu.
 
Tuache ushabiki kwenye sheria, sheria ndiyo iliwapa ushindi lakini ni sheria hiyohiyo imesema mahakama wamekosea.
Maadamu wote wana wanasheria ni jukumu lao kupambana kisheria badala ya sisi kuendelea kutoa mapovu.
 
Wale ambao huwa tunasikia hawakutakiwa kujibu chochote kwakuwa mahakama hio haina mamlaka ya kusikiliza shauri lao huwa wanaambiwa na nani wasijibu?

Ina maana hakimu yeye anatwanga tu hata kama anajua mahakama yake haina mamlaka
 
"Tigo katika utetezi wake kupitia kwa mkuu wa kitengo cha burudani na miradi David Zakaria, alidai kuwa MIC ilipelekewa nyimbo hizo na kampuni ya Cellulant Tanzania Limited, waliyoingia nayo mkataba wa kisheria kwa huduma hiyo na kwamba ndio inapaswa kuwalipa wasanii husika"

Kwahiyo wasanii hao walilipwa na tigo ama cellulant?
 
Aisee! Kina MwanaFA hela zao si walilipwa kwa hukumu ya Mahakama? Sasa wao kosa lao nini hapo mpaka kusema mali zao zitakamatwa?

Wataalamu wa sheria mje hapa kutusaidia kuelewa hili jambo.
Ila ni kweli hapa kuna "law controversy" wasanii wamelipwa kutokana na maamuzi ya hakimu (legal personnel) sasa wakifirisiwa au kufungwa watakuwa wanaonewa from the law basis.
 
Mahakama iliyosikiliza hiyo kesi haikupaswa kusikiliza kesi inayozidi madai ya kiwango cha million 300 kisheria au haujapitia bandiko vyema mkuu !?
Ishu ni kwamba, kosa sio la waliolipwa, kosa ni la hakimu(mahakama) jamaa wanaonewa, jamaa hawana kosa lolote ni kama wanaonewa kutokana na uzembe wa hiyo mahakama ya wilaya, got it?
 

Nakumbuka mahakama iliwaambia wanaruhusiwa kukamata mali za Tigo. Nadhan kwa sababu kesi ilikua inaendelea tokea 2011, Tigo wakaona hawa jamaa wanaweza kukamata mali zao!
 
Wale ambao huwa tunasikia hawakutakiwa kujibu chochote kwakuwa mahakama hio haina mamlaka ya kusikiliza shauri lao huwa wanaambiwa na nani wasijibu?

Ina maana hakimu yeye anatwanga tu hata kama anajua mahakama yake haina mamlaka?
Zile ni kesi za mauaji mara nyingi huwa wanaambiwa vile ile baadhi ya vitu fulani mahakama kuu iwe ime vikamilisha na kujiridhisha.
Pia ni wajibu wa mtuh kufikishwa mahakamani baada ya masaa kadhaa.
Upande wa kesi ya Tigo atawaachia mawakili upande wapili waje kupiga P.O, au wakate rufaa.
 
Mahakani sio jengo la kanisa au msikiti useme kuna huruma.

Lakini kumbuka hoja ya huyo hakimu ni moja tu na ambayo haina mashiko, ambapo haibaidilishi ukweli kwamba tigo waliwaibia hao jamaa (this is unchanged) kwahiyo jamaa wakiamua kuendelea na madai kwamba walipwe watalipwa tena kwa kiwango cha 4bills wakisimama kidete
 
So you hate em?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…