Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mahakama Kuu ya Dodoma ilipofunguliwa kesi ya kikatiba na kada wa Chama cha Mapinduzi Mch. Dkt. Godfrey Malisa imesikiliza kwa mara ya kwanza kesi hiyo Agosti 5,2025. Akiongea na waandishi wa habari Dkt. Malissa amesema hakimu anayesimamia kesi hiyo amesema kuna umuhimu wa kesi hiyo kusikilizwa baada ya kupitia shauri zima kama lilivyowasilishwa mbele yake.
Shauri hili linalosimamiwa na jopo la mawakili watatu linalenga kuiomba mahakama kutoa tafasri na uamuzi wa usahihi katika mchakato wa kumpata mgombea wa CCM, Samia Suluhu Hassan na mgombea mwenza Dr Emmanuel Nchimbi.
Mahakama imeutaka upande wa wawalamikiwa ambao ni CCM kutoa maelezo ya utetezi ndani ya siku saba kabla mahakama haijatoa uamuzi wa shauri hilo. Ikumbukwe kuwa shauri hilo limewasilishwa mbele ya mahakama kuu kwa hati ya dharula.