GE2025 Mahakama yatoa Siku Saba CCM kujieleza, uteuzi wa Samia kugombea Urais

GE2025 Mahakama yatoa Siku Saba CCM kujieleza, uteuzi wa Samia kugombea Urais

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Akitoa maelezo ya kesi hiyo, Jaji Mbosso wa Jux alisema '' Madai ya mlalamikaji kuhusu kukiukwa kwa katiba ya Chama ni ya kweli. Jaji amesema hoja za Walalamikiwa kuhusu mwenendo wa kesi zimezingatiwa, na kwamba aliyepaswa kushtakiwa si Chama bali bodi ya Wadhamini. Kwa kufuata katiba ya Chama, Ibara ya 700, fasili (i) (a ) ikisomwa pamoja na Ibara 900 kifungu kidogo C fasili (f), Chama kinaweza kufanya taratibu zake za ndani bila kuingiliwa. Kwamba, mkutano umeteua wagombea si tatizo kwasababu Wazee wa Chama walielekeza Emma na wenzie watengeneze taratibu''

Baada ya maelezo hayo Jaji Mbosso alitupilia mbali maombi ya mlalamikaji



Mshana Jr JokaKuu
 
Kumbe ni mchungaji sasa tumemulewa kwanini anapinga lkn kitaeleweka October tano tena
 
Baada ya siku saba hizo in shahuri litatupiliwa mbali kwa kukosa sifa
Nitunzieni hii comment
 
Hiyo kesi itafutwa katika hatua ya mapingamizi ya kisheria (Notice of preliminary objection). Yatasukwa mapingamizi ambayo dunia hii haijawahi kuyaona, kesi yote itapondwapondwa, kitu pekee ambacho kitabaki sahihi ni majina ya mshitaki na mshitakiwa, na jina la mahakama
Kati ya watu wenye roho mbaya na isiyo na hadhi ya uwepo kwenye chumba ni wewe...period
 
Mahakama ya haki iko ubongoni kwako na jeshi halali ni mikono yako, kama mtubuna mmudu hamna haja ya kupoteza raslimali na muda. Ishi nae.
 
Mahakama Kuu ya Dodoma ilipofunguliwa kesi ya kikatiba na kada wa Chama cha Mapinduzi Mch. Dkt. Godfrey Malisa imesikiliza kwa mara ya kwanza kesi hiyo Agosti 5,2025. Akiongea na waandishi wa habari Dkt. Malissa amesema hakimu anayesimamia kesi hiyo amesema kuna umuhimu wa kesi hiyo kusikilizwa baada ya kupitia shauri zima kama lilivyowasilishwa mbele yake.

Shauri hili linalosimamiwa na jopo la mawakili watatu linalenga kuiomba mahakama kutoa tafasri na uamuzi wa usahihi katika mchakato wa kumpata mgombea wa CCM, Samia Suluhu Hassan na mgombea mwenza Dr Emmanuel Nchimbi.

Mahakama imeutaka upande wa wawalamikiwa ambao ni CCM kutoa maelezo ya utetezi ndani ya siku saba kabla mahakama haijatoa uamuzi wa shauri hilo. Ikumbukwe kuwa shauri hilo limewasilishwa mbele ya mahakama kuu kwa hati ya dharula.

Mchungaji Malisa alindwe pia hakimu anayesikiliza shauri hili alindwe kwa hali ya juu, team msoga wanaweza 💉💉💉
 
Back
Top Bottom