Mahakama yatupilia mbali mapingamizi ya utetezi, maelezo ya Mohamed Lingw'enya yapokelewa na Mahakama. Kesi kuu kuendelea Des. 15, 2021

Amani ya Nchi ni muhimu zaidi kuliko mwanasiasa yeyote yule.

Kamwe tusijaribu kuchezea au kufanya mchezo na Amani ya Nchi.

Mbowe sio MALAIKA.................................
Narudia tena na tena wewe ni MBWA koko unahitaji kipigo!
 
Lema anatoa huo ushauri wa kipumbavu akiwa amefichwa kwenye mbawa za mwanaume Canada

Anaogopa nini kurudi Tanzania
Lema akirudi baadae angepewa kesi ya ugaidi wewe ungekuja tena hapa jf na kuuliza ili kuwaje lema alirudi tanzania
 
Tuliaminishwa humu kibatala ndiye wakili bora kabisa hapa nchini kwa sasa?
Mbona anagaragazwa hivi sasa na wakina Wa kili Kidando?

Unaweza kuwa na timu nzuri yenye wachezaji bora lakini refa akiamua kuwabania mfungwe hashindwi. Anachofanya Jaji Tiganga ni kuwapendelea upande was serikali. Jaji akiamua kupendelea hashindwi. Lakini hukumu hii inaeza ikazaa Jambo ambalo hatukulitegemea. Kama vile uchaguzi mkuu ulivyozua msiba mkubwa. Jaji anapingana na nature, na nature huwezi kupigana nayo utashinda. Refer kwa polepole kwa sasa anavyoangahika.
 

Kula tano mwanangu, hilo la kushindana na nature huwa nalisema sana humu. Hata sasa CCM inalazimisha kukaa madarakani lakini nature inakataa. Wanaiba kura ili wakae madarakani, matokeo yake wapinzani wamesusia hizo chaguzi, wapiga kura nao hawajitokezi tena! Huyo Jaji anapoteza muda tu. Hapo mawakili wa utetezi wakijitoa na kusema hawana imani na mahakama, basi mahakama itazidi kupoteza imani kwa umma. Na impact yake itakuwa kubwa.
 
Kweli mawakili wa Gaidi Mbowe na wenzake ni bure kabisa. Wanafanya court battle kwa kutegemea huruma ya akina Mmawia na tindo! Nafikiri ni wakati wa kuanzisha ashtag

#KIBATALA SIO ADVOCATE!!!!

Yaani mnadhani tuna imani na hizi mahakama, hivyo mnaamini tuna ujinga huo kuwa mawakili wa utetezi wanashindwa huko mahakamani. Ni kama box la kura hivi sasa, unaona kabisa wapiga kura hawajafika hata 100, kisha matokeo yakitoka unasikia CCM wamepata kura 500. Tulishaamka muda mrefu, upuuzi uliopo kwenye taasisi nyingi za umma, upo mahakamani pia. Hizo ndio dalili za mwisho za chama kupoteza uhalali wa utawala.

Kinachoendelea mahakamani kwasasa kwa sisi wasoma alama za nyakati, tunajua nini kitaenda kutokea kwenye utawala huu wa CCM.
 
Vipi ile kesi ambayo Mbowe alirudishiwa hela yake? Subiri rufaa,hawa majaji wa michongo na uvccm kuna muda wao
Majaji wanaosikiliza rufaa awachaguliwi na Rais au wao awasikilizi maelekezo toka juu?
 

Sheria zetu ni za kikoloni. Katika nchi zilizoendelea, recanting (retracting a statement by a defendant) au hata withdrawing a guilty plea sio big deal. Prosecutors wanapaswa kuwa na uwezo wa kuthibitisha mashitaka yao dhidi ya defendant hata bila confession ya defendant. Faida pekee ya defendant’s confession ni kuokoa muda wa mahakama na wa pande zote zinazohusika.

All in all, mawakili wanaounda jopo la defense wanapoteza muda mwingi kwenye POs ambazo zina zero-chance ya kufanikiwa (au hata zikifanikiwa, zina impact kiduchu sana kwenye kesi ya msingi). That’s nonsense. Wanapaswa watumie muda mwingi kunoa mikakati yao ya utetezi katika kesi ya msingi!
 
Si ndio hivyo wanavyonoa?

Amandla...
 
Mkuu Tuliambiwa 'Wenzie Mbowe'' wanatumikia kifungo tayari
Tuliambiwa 'mtuhumiwa' alikimbia huku rejea zikionyesha akiwa nchini
Tukasikia Jaji anatoa maoni na si kwa mujibu wa sheria . '' kwa maoni yangu'
Mahakama ilipowasihi waendesha mashata wakaweke uzuri mashataka yao
Jaji kiongozi akiapishwa '' kwamba hukumu zizingatie hali ya nchi '!

Kesi ya Mbowe pamoja na wengi kusema inatia doa Taifa na nchi kwa ujumla , kwa upande mwingine imesaidia sana na pengine kupitia kesi hii kuna kudhihiri kwa baadhi ya mambo

1. Kwamba, wasiojulikana wapo na wengine wamejulikana na haijulikani kwanini hawajulikani
2. Imetoa ushuhuda kwanini ilikuwa kupoteza muda kupeleka kesi za uchaguzi
3. Imeondoa shaka kuhusu 'Mhimili uliojichimbia chini zaidi' na hii mingine ikielea na kupepesuka

Kesi imeonyesha nafasi ya mahakama katika jamii na imeacha maswali mengi sana ikiwa kuna mahali mbadala pa kupata haki.

Imeonyesha matundu katika mhimili wa haki kuliko wakati mwingine wowote ule wa uhai wa Taifa.

Maana yake ni moja, haki isipopatikana mahakamani itapatikana wapi?

Wanaodhani tuna tatizo la Tume ya uchaguzi wafikirie tena.

Tatizo ni kubwa sana, kesi ya Mbowe iwafungue macho.
Mifumo ya Taasisi zetu haifanyi kazi kama ilivyotarajiwa.

Wanasaikolojia wanasema ukitaka kumshinda mpinzani wako kwanza mfanye dhalili ili kumuondolea ''confidence'' halafu mkabili. Mkuu unakumbuka ''probation' ?

Hakuna njia ya mkato, katiba mpya itakayojenga mifumo imara ya taasisi zetu ni jibu

Hii kesi iendelee inafunua macho , nadhani ni moja ya vitu muhimu sana vinavyolizindua Taifa
 
yaani Tanzania ni nchi ya amani sana. imagine, kesi ni ya upinzani, lakini wazungu ambao siku zote wamelalia upande wa upinzani, wanahudhuria kesi bila shida. sasa wewe nenda nchi za watu, kaonyeshe brassiness upande mmoja uone kama utakubaliwa na nchi hiyo. wajerumani na wazungu wengine wote wameonyesha kulalia upande mmoja bila hata aibu, hata kwa mambo ambayo yana ushahidi. hao mawakili wa serikali wanafanya kazi ngumu kwasababu wanashindana sio tu na mawakili wa mbowe, wanashindana na nchi za EU zote pia. na wanawashinda.
 

..Ujerumani wametupa fedha kuboresha mifumo yetu ya sheria. Pia wamekuwa wafadhili wakubwa wa kitivo cha sheria Udsm. Kwa hiyo lazima wafuatilie kinachoendelea.
 

Watu mna obsession na katiba mpya utadhani katiba mpya itakuwa na uwezo wa kujilinda yenyewe. Kama haki zilizomo kwenye katiba ya sasa hatuwezi kuzisimamia, kuna sababu gani ya kuamini kuwa tutaweza kuisimamia katiba mpya? FYI, zipo nchi zingine zilizoandika upya katiba zao, lakini shida zao zimebaki palepale!
 

You’re right, hiyo sio kazi ya diplomatic missions. Ni interference ya wazi kwenye internal affairs za host country!
 
Tanzania sio nchi ya amani..ni nchi ya watu waoga.tunaojiridhisha uoga wetu kwa kujificha kwenye kivuli cha amani..if you are in your right senses haya yote yanayoendelea kwa ujumla wake yanaonyesha ni watu waoga waliopumbazwa na siasa za ujamaa..kumbuka amani hupewi bali unaitafuta na haiji hadi kwa ncha ya upanga..amani huja baada ya kuushinda uoga.
 
Kwanza, nitajibu hoja zako kwa kuanzia na hii ya katiba iliyopo ya 1977.

Haki ndani ya katiba ya sasa haziwezi kusimamiwa ni hoja mfu potofu inayotumiwa na watu wasioweza kutazama mambo kwa upana wake.Ni hoja primitive na silaha rahisi kwa 'ignorant'

Katiba ya sasa ni sawa na mgonjwa aliyepo ''ICU'' kwamba mgonjwa hajiwezi wala kujitambua bado unamatumaini anaweza kwenda uani, kujiwekea Oxygen na hata kukusaidia wewe ulikwenda kumsalimu.

Nyerere alisema '' katiba inampa madaraka ya kuwa Dikteta''. Kwa bahati nzuri uadilifu na maadili ya viongozi waliomfuata yaliitetetea katiba. Miaka 5 iliyopita tumethibitisha alichosema Nyerere ni kweli. Katiba haikuweza kujitetea nani angeweza kuitumia kujitetea

Katiba Mpya si suluhisho la matatizo lakini ni hatua muhimu sana. Hakuna katiba iliyokamili duniani lakini zipo zilizo na hali nzuri. Kenya ya leo ni tofauti na sisi kwa haki na uwajibikaji

Kenya CJ anagombea hateuliwi na hafungwi na mtu. Yupo huru kutetea masilahi ya Umma

Majaji wana muda ili kuondoa conflict of interest. Kwamba hawategemewi kuwa katika bodi au taasisi nyingine na hilo linawaweka huru. Fuatilia yanayotokea Kenya

Katiba mpya si kwa ajili ya uchaguzi au tume, bali kurekebisha mifumo dhaifu iliyotakiwa kujisimamia na kusimamia umma zikiwemo taasisi kama Bunge na Mahakama

Vyombo kama DPP, DCI Takukuru ni vya umma kwa ajili ya Umma

Unakumbuka CAG na T 1.5? Kaondolewa na hakuna kilichotokea.
Takukuru ipo Ofisi ya Rais kisheria kabisa. Hadi leo ni malumbano ya T 1.5

Unakumbuka kesi ya Wakurugenzi kuwa wasimamizi wa chaguzi?

Mahakama ikaamua wasimamizi wanaapishwa na hivyo wanatenda haki. Think about that!

kwamba Mahakama ya Tanzania inaamini Mtanzania akila kiapo huyo ni muadilifu kabisa!!!
Hakuna Waziri au katibu mkuu au Mkurugenzi anayefanya ''uhalifu'', wameapa!

Bungeni kuna watu 19 wanalipwa pesa za umma. Ni kupitia mamlaka ya katiba, ipo sheria ya viongozi kutoshtakiwa kwa makosa akiwemo Rais, Waziri mkuu na Spika.
Katika mazingira haya nini unategemea katiba ya 1977 inaweza kufanya tofauti?

Hoja ni nyingi muhimu ni kuelewa katiba mpya inalenga kupunguza uozo iliyopo si kwamba ni mbovu bali ipo taabani.

Kinachoendelea mahakamani ni jambo la heri la kuwafumbua macho Watanzania.
Kuna mengi hawakujua lakini leo wanayaona na hili la kesi ya Mbowe ni jema

Kudhani ni kesi ya Mbowe ni kujidanganya! Yanayoendelea yatamkuta yoyote yule.


JokaKuu Alinda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…