Mahakama yatupilia mbali mapingamizi ya utetezi, maelezo ya Mohamed Lingw'enya yapokelewa na Mahakama. Kesi kuu kuendelea Des. 15, 2021

Mahakama yatupilia mbali mapingamizi ya utetezi, maelezo ya Mohamed Lingw'enya yapokelewa na Mahakama. Kesi kuu kuendelea Des. 15, 2021

Mahakama kuu, Divisheni ya makosa ya uhujumu uchumi na rushwa, Ubungo-Mawasiliano, DSM, 14/12/2021


Wakati washtakiwa wote wakiwa wameingia mahakamani muda huu, ingawa bado hawajapanda kizimbani na mawakili wa pande zote wameingia ndani ya mahakama.. waandishi wa habari wamemzunguka FREEMAN Mbowe na washtakiwa wenzake na wanataka picha za ‘fonti fedii’ pale…

Jaji ameingia Mahakamani

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa

Wakili Peter Kibatala anatambulisha Jopo la Mawakili wa Utetezi

Nashon Nkungu
John Malya
Fredrick Kihwelo
Dickson Matata
Seleman Matauka
Edward Heche
Alex Massaba
Gaston Garubindi
Sisty Aloyce

Jaji anaita Washtakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani....

WS Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kutolewa Uamuzi tupo tayari Mheshimiwa

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji, Na sisi Pia Kwa Ruhusa yako tupo tayari

Jaji anaandika Kidogo, Mahakama ipo kimya

Jaji: Shauri hili ni kweli lina kuja kwa ajili ya Uamuzi ambao ulikuwa really served

Mahakama ilielekeza Mawakili Walete Hoja zao Kwa Maandishi ambapo wameleta

Wakati shahidi namba 08 ASP Jumanne Wakati Wa Kutoa Ushahidi Wake

Alieleza Kwamba alipewa kazi ya Kuandika Maelezo ya Mshitakiwa Wa tatu, Na baada ya Kueleza hivyo aliomba Maelezo hayo ya pokelewa Mahakamani, Ambapo Upande wa Utetezi Walipinga kwa Sababu 9..

Sababu ya Kwanza ni Mshitakiwa namba tatu hakuwa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam.. Na Haku andika Maelezo yoyote..

Sababu ya Pili Mshitakiwa Wa tatu alilazimishwa Kuweka Sahihi katika Maandishi ambapo pia Pamoja na Kulazimishwa hakupewa nafasi ya Kusoma Maelezo yake.. Alitishwa na Goodluck Minja na ASP Jumanne alimtishia Kwamba Asipoweka atateswa Kama alivyoteswa Moshi

Sababu ya 3 ni kwamba Maelezo yake yalirekodiwa Nje ya Muda, yalirekodiwa Siku ya Tarehe 09 August 2020 wakati amekamatwa 05 August 2020.

Sababu ya 4 ni kwamba Maelezo ya Onyo yalikuwa a yameandikwa kwa Sheria ya Kifungu 57((1) Ilivyofanyiwa Marejeo 2020 ambapo Sheria hiyo haipo

Sababu Nyingine NI kwamba alionywa kwa Sheria ya Kuzuia na Kupambama na Ugaidi wakati sheria hiyo haipo..

Sababu Nyingine NI Maelezo ambayo yanalengwa Kutolewa Mahakamani yapo Tofauti na yale Yaliyotolewa wakati wa Commital kwa Kutofautisha Subsection

Sababu ya Saba Hakuna Kifungu Kinachoonekana Kwamba wamechukua Maelezo na Kushitaki kwa kifungu kipi

Kutokana na Hoja zote Mbili zilizo letwa zilikuwa zinaangukia katika Sheria ya Ushahidi ambapo ilipelekea Kuwepo Kwa Kesi Ndogo

Kwa hiyo Mapingamizi hayo yalishughulikiwa kwa Njia ya Kuleta Hoja Mahakamani

Na Kwamba Baada ya Kesi Ndogo Submission ziletwe kwa Kuleta Hoja ya Kuunga Mkono kuhusu Mapingamizi Yanayo angukia Katika Sheria ya Ushahidi..

Jaji: Katika Kesi Ndogo Upande wa Mashtaka wenye Jukumu La Kuleta Mashahidi wa Kuthibitisha.. Walileta Mashahidi wanne..

ASP Jumanne
Goodluck Minja
ISSA Maulid
Msemwa

Na walileta Vielelezo, Barua ya Msajili Kama Kielelezo namba 1, Detention Register kama Kielelezo Namba 2 na Kielelezo namba 3

Jaji: Kwa Upande wa Utetezi walileta Mashahidi Watatu, Kielelezo Namba Moja Maelezo Ya GOODLUCK Minja, Nakala ya Hati ya Mashtaka , Dispatch Book, Nakala ya Hati ya Mashtaka ya Kesi namba 17/2020, Nakala ya Hati ya Mashtaka Ya Shahidi namba tatu kesi 63/2020 020

Na Kielelezo Kingine ni Diary ambayo Ulichukukiwa wakati WA shahidi Wa Mashtaka Anatoa Ushahidi Wake, Sababu Pande zote hawajazungumzia Kwa Kirefu Kielelezo Hiki basi na Mimi sitoongelea kwa akirefu Kielelezo Hiki, Mahakama haina Nia ya Kurejea Maelezo Ya Ushahidi wote

Jaji: Suala la Kutafuta Ukweli kwa Hoja namba Moja na Mbili na Hoja namba Tatu Mpaka namba Saba zilikuwa resolved Kwa submission zilizopangiwa parties Mahakamami... Ni Utaratibu wa Kawaida mambo yanayohusu Sheria Kuamuliwa kwanza..

Kwenda Kwenye Hoja za Kisheria si Sawa, Ni Vizuri kwenda Kwenye Hoja za Ushahidi Kwanza, Kwa sababu hiyo Tutaanza Mambo yanayuhusu Ushahidi kabla Mambo ya Kisheria..

Kwa Mujibu wa Sheria ya Ushahidi Sura ya 6 Kifungu 57 (1) pale ambapo Utetezi wa Napinga Maelezo ni Wajibu wa Mashitaka Kuthibitisha, Pasipo Kuacha Shaka..

Kutokana na Ushahidi Wa shahidi namba Moja na Shahidi Nmab tatu ndiyo Waliokwepo Wakati Wa naandika Maelezo, Kwa Mujibu wa Ushahidi Wao walimkamata Mshtakiwa Huko Rau Madukani,
Yaani...baada ya miyoo kutulia kwa mda, sasa miyoo mapgo yake wengi yanaenda kwa kasi hata Judge mwenyewe Pressure juu!!
 
Kama ni kweli Mbowe si GAIDI na watu wanamsingizia kwamba ni GAIDI basi watapata adhabu kubwa mno !! wajiepushe na hii kitu haraka sana, kuna adhabu ya KIFO yaja kwa wahusika wote kwani Mungu huwa hataniwi - Mzee wa Upako.
 
Mbowe si gaidi!
Wanapoteza rasilimali za umma kwa kesi isiyo na miguu wala kichwa.
 
Ifike wakati hizo "Court sessions" ziwe broadcasted live tu kama majirani zetu Kenya...ili majaji kama wanapora haki ya mtu Umma ujue.

Hata mambo ya kureport yanapotosha sana. Mahakama ilipaswa kuwa ndio chombo huru zaidi, na wazi zaidi kuliko mihimili mingine kwani ndiko sehem ya juu zaidi haki inapatikana.

KATIBA MPYA, KATIBA MPYA, KATIBA MPYA
 
Back
Top Bottom