Mahakama kuu, Divisheni ya makosa ya uhujumu uchumi na rushwa, Ubungo-Mawasiliano, DSM, 14/12/2021
Wakati washtakiwa wote wakiwa wameingia mahakamani muda huu, ingawa bado hawajapanda kizimbani na mawakili wa pande zote wameingia ndani ya mahakama.. waandishi wa habari wamemzunguka FREEMAN Mbowe na washtakiwa wenzake na wanataka picha za ‘fonti fedii’ pale…
Jaji ameingia Mahakamani
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa
Wakili Peter Kibatala anatambulisha Jopo la Mawakili wa Utetezi
Nashon Nkungu
John Malya
Fredrick Kihwelo
Dickson Matata
Seleman Matauka
Edward Heche
Alex Massaba
Gaston Garubindi
Sisty Aloyce
Jaji anaita Washtakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani....
WS Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kutolewa Uamuzi tupo tayari Mheshimiwa
Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji, Na sisi Pia Kwa Ruhusa yako tupo tayari
Jaji anaandika Kidogo, Mahakama ipo kimya
Jaji: Shauri hili ni kweli lina kuja kwa ajili ya Uamuzi ambao ulikuwa really served
Mahakama ilielekeza Mawakili Walete Hoja zao Kwa Maandishi ambapo wameleta
Wakati shahidi namba 08 ASP Jumanne Wakati Wa Kutoa Ushahidi Wake
Alieleza Kwamba alipewa kazi ya Kuandika Maelezo ya Mshitakiwa Wa tatu, Na baada ya Kueleza hivyo aliomba Maelezo hayo ya pokelewa Mahakamani, Ambapo Upande wa Utetezi Walipinga kwa Sababu 9..
Sababu ya Kwanza ni Mshitakiwa namba tatu hakuwa Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam.. Na Haku andika Maelezo yoyote..
Sababu ya Pili Mshitakiwa Wa tatu alilazimishwa Kuweka Sahihi katika Maandishi ambapo pia Pamoja na Kulazimishwa hakupewa nafasi ya Kusoma Maelezo yake.. Alitishwa na Goodluck Minja na ASP Jumanne alimtishia Kwamba Asipoweka atateswa Kama alivyoteswa Moshi
Sababu ya 3 ni kwamba Maelezo yake yalirekodiwa Nje ya Muda, yalirekodiwa Siku ya Tarehe 09 August 2020 wakati amekamatwa 05 August 2020.
Sababu ya 4 ni kwamba Maelezo ya Onyo yalikuwa a yameandikwa kwa Sheria ya Kifungu 57((1) Ilivyofanyiwa Marejeo 2020 ambapo Sheria hiyo haipo
Sababu Nyingine NI kwamba alionywa kwa Sheria ya Kuzuia na Kupambama na Ugaidi wakati sheria hiyo haipo..
Sababu Nyingine NI Maelezo ambayo yanalengwa Kutolewa Mahakamani yapo Tofauti na yale Yaliyotolewa wakati wa Commital kwa Kutofautisha Subsection
Sababu ya Saba Hakuna Kifungu Kinachoonekana Kwamba wamechukua Maelezo na Kushitaki kwa kifungu kipi
Kutokana na Hoja zote Mbili zilizo letwa zilikuwa zinaangukia katika Sheria ya Ushahidi ambapo ilipelekea Kuwepo Kwa Kesi Ndogo
Kwa hiyo Mapingamizi hayo yalishughulikiwa kwa Njia ya Kuleta Hoja Mahakamani
Na Kwamba Baada ya Kesi Ndogo Submission ziletwe kwa Kuleta Hoja ya Kuunga Mkono kuhusu Mapingamizi Yanayo angukia Katika Sheria ya Ushahidi..
Jaji: Katika Kesi Ndogo Upande wa Mashtaka wenye Jukumu La Kuleta Mashahidi wa Kuthibitisha.. Walileta Mashahidi wanne..
ASP Jumanne
Goodluck Minja
ISSA Maulid
Msemwa
Na walileta Vielelezo, Barua ya Msajili Kama Kielelezo namba 1, Detention Register kama Kielelezo Namba 2 na Kielelezo namba 3
Jaji: Kwa Upande wa Utetezi walileta Mashahidi Watatu, Kielelezo Namba Moja Maelezo Ya GOODLUCK Minja, Nakala ya Hati ya Mashtaka , Dispatch Book, Nakala ya Hati ya Mashtaka ya Kesi namba 17/2020, Nakala ya Hati ya Mashtaka Ya Shahidi namba tatu kesi 63/2020 020
Na Kielelezo Kingine ni Diary ambayo Ulichukukiwa wakati WA shahidi Wa Mashtaka Anatoa Ushahidi Wake, Sababu Pande zote hawajazungumzia Kwa Kirefu Kielelezo Hiki basi na Mimi sitoongelea kwa akirefu Kielelezo Hiki, Mahakama haina Nia ya Kurejea Maelezo Ya Ushahidi wote
Jaji: Suala la Kutafuta Ukweli kwa Hoja namba Moja na Mbili na Hoja namba Tatu Mpaka namba Saba zilikuwa resolved Kwa submission zilizopangiwa parties Mahakamami... Ni Utaratibu wa Kawaida mambo yanayohusu Sheria Kuamuliwa kwanza..
Kwenda Kwenye Hoja za Kisheria si Sawa, Ni Vizuri kwenda Kwenye Hoja za Ushahidi Kwanza, Kwa sababu hiyo Tutaanza Mambo yanayuhusu Ushahidi kabla Mambo ya Kisheria..
Kwa Mujibu wa Sheria ya Ushahidi Sura ya 6 Kifungu 57 (1) pale ambapo Utetezi wa Napinga Maelezo ni Wajibu wa Mashitaka Kuthibitisha, Pasipo Kuacha Shaka..
Kutokana na Ushahidi Wa shahidi namba Moja na Shahidi Nmab tatu ndiyo Waliokwepo Wakati Wa naandika Maelezo, Kwa Mujibu wa Ushahidi Wao walimkamata Mshtakiwa Huko Rau Madukani,
Kwamba Wakati wanawakamata Walikuwa na Mwenzao Moses Lijenje, Na Washitakiwa kwa ridhaa yao Waliongoza Zoezi la Kumtafuta Moses Lijenje Katika Maeneo ya Moshi na Wilaya ya Hai, Kwa amba Baada ya Kushindwa Kumpata Siku ya Tarehe 06 August 2020 Walianza Safari kuja Dar es Salaam
Jaji: Na wakiwa kabidhi Sehemu ya a Mapokezi na a Ada ya hapo waliondoka Kwenda Kufanya Usafi, Na Kwamba walipokelewa na DC Msemwa.. Na walirudi tena kumuhitaji Mshtakiwa Namba tatu Kuja Kumuandika maelezo..
Kwa ajili ya Kuandika Maelezo yake ya onyo na Kwamba Mshitakiwa Alitoa Maelezo yake kwa hiari yake,
Ushahidi Wake uliungwa Mkono na Shahidi namba Mbili, alieleza kwamba aliwapokea baada ya Washtakiwa Kufikishiwa Kwake na Kuwaingiza Kwenye Kumbukumbu ya DETENTION REGISTER..
Kwa Mujibu wa Ushahidi Huo yeye anashuhudia Kwapo Katika Kituo hicho, Anashuhudia kuwa pokea na Kumtoa tena kisha kumpokea tena Mshtakiwa Namba tatu.. Mshtakiwa namba tatu aliporudishwa alikuwa kwenye hali Nzuri
Na Shahidi namba Moja anaendelea Kusema Kwamba Baada ya Kumalizia Kumuandika Maelezo na Kumsomea kisha akamrudisha tena Mahabusu,
Jaji: Ushahidi huu ulipingwa na Upande Wa Utetezi ambapo Mshtakiwa Watatu alitoa Ushahidi Wake Kwamba hajawahi Kufika katika Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam..
Walipofikishwa Dar es Salaam Walifikia Kituo cha Polisi Tazara na Kupelekwa Mbweni
Ambapo alichukuliwa kwenye Chumba alichokuwepo Kupelekwa Chumba Kingine na kisha Kulazimishwa Kusaini Maelezo, Maelezo yoyote yanayosema Kwamba aliyatoa ni ya Uongo...
Akaendelea Kusema Kwamba Upande wa Mashtaka Umeshinda Kuthibitisha kwamba Msemwa alikuwepo Kituo cha Polisi Kati Dar es Salaam Siku hiyo...
Jaji: Hata alipoulizwa alishindwa Kusema aliwapokea zamu yake,
Shahidi wa Pili yeye alisema Kwamba alikamatwa huko Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro na Kuletwa Kituo Cha Polisi Oysterbay alimkuta Msemwa
Na Kwamba Kwa Sababu hakuwa amekula alimuagiza Afande Msemwa akamchukulie Chakula na Akaendelea Kuwa Rafiki ya Afande Msemwa..
Na Kwamba hata Baada ya Kupelekwa Mahakamani alirudishwa tena Kituo cha Polisi Oysterbay kwa Siku 19..