Mahakama yatupilia mbali ombi la Afande Fatma kusomewa mashtaka popote alipo

Mahakama yatupilia mbali ombi la Afande Fatma kusomewa mashtaka popote alipo

Kuna huyo wakili Madeleka akiongea utadhani keshashinda kesi, mpaka anasema hakimu ashtakiwe. Aiseee tabu sana
Madekela ana mihemko sana na anapenda sana mitandao.Wakili smart ni kibatala.Yuko na utulivu wakutosha.
 
Hakimu Wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma Nyamburi Tungalaja ametupilia mbali maombi yaliyowasilishwa mahakamani na upande wa walalamikaji na Wakili Peter Madeleka ya ombi la mahakama kusikiliza kesi ya Fatma Kigondo Afande popote alipo hata kama ni Hospitali.

Akizungumza mbele ya mahakama wakili aliemwakilisha wakili Peter Madeleka , wakili Aron Kishai amesema hakimu ametupilia mbali ombi hilo ambapo hakimu amesema ombi hilo halijakidhi vigezo na masharti na malalamiko hayo hayajandikwa kwa kufata utaratibu wa mahakama.

“Yaliyojiri Mahakamani leo tumeingia Mahakamani mheshimiwa Nyamburi Tungalaja ametupilia mbali yale maamuzi ambayo tuliyatarajia kwamba angesign yale malalamiko na amekuja na sababu kwamba ambayo yako chini ya kufungu cha (128)(2) (4) cha mwenendo wa makosa ya jinai ya kwamba yale malalamiko yana kasoro na hayajaandikwa kwa kufuata utaratibu wa mahakama.” Amesema Wakili Aron Kishai.

Aidha Wakili Aron amesema hakimu ametoa nafasi ya kukata rufaa kama upande wa ulalamikaji haujaridhika na maamuzi ya mahakama.
 

Attachments

  • IMG_3999.jpeg
    IMG_3999.jpeg
    836.6 KB · Views: 3
As it expected🤣🤣

Afghanstan afande kawashinda, je wataweza kumfanyia impichment Rais au Makamu wa Rais endapo akienda ndivyo sivyo kama ilivyotokea Kenya??
 
Back
Top Bottom