Maharage Chande kutoka Ukurugenzi TANESCO hadi Postamasta - amepanda au ameshuka?

Culture ya kutegemea teuzi au kazi za serikali ni akili za kimaskini sana, pesa ipo private sector na ukimwaona mtu kawa milionea kwa kufanya kazi serikalini lazima atakuwa mwizi tuu
 
Kashuka kiwango ingekuwa timu tungesema kashuka daraja
 
Lakini kama mteuzi kagundua kosa mapema sibora kalisahisha kuliko kungoja mambo yaharibike.
 
Huko Posta hakuna kukuru kakara zilizoko TTCL na TANESCO.
Akatafutiwa anakoweza kula kivulini kwa urefu wa kamba bila uwezo wa kufikiri, kuhukumu na kutenda...haya mawazo potofu unayatoa wapi?
Sasa amepangiwa eneo la kazi linaloonekana kwendana na uwezo wake wa kufikiri, kuhukumu na kutenda.
Are you serious Mama Amon? Acheni utani jamani...yaani huo uwezo wa kufikiri, kuhukumu na kutenda hauhitajiki TTCL wala TANESCO bali POSTA?

Masikini Tanzania, oops Tanganyika!
 
Namba 4 kuna uongo mkubwa. Hujafanya home work yako vizuri. CEO wa Shirika la Posta ni Postamaster General. Hakuna Mkurugenzi.
 
Mkurugenzi wa Tanesco haleti mvua, mvua zisiponyesha ,maji kwenye mabwawa yanapungua hatimaye mgao wa Umeme unafuata. Tanesco walishasema mapema kuwa mgao wa umeme unakuja. Tatizo hili litatokea hata kwenye bwawa la Mwalimu Nyerere. Hizi ndoto za kuacha umeme wa gesi na kukimbilia umeme unaotokana na maji ndio zimetuleta hapa. Mabadiliko ya tabia nchi yapo na yataendelea, inatakiwa tukumbatie vyanzo vipya vya umeme , jua, upepo,gesi na uranium (Nuklia)
 
Nadhani tangu baada ya Mkapa, hakukuwa tena na suala la vetting. Neno MWENZETU au MTU WETU ndilo dira na mwongozo wa teuzi karibia zote.
Hahahaha,Mkataba wa Mwintongo

Nauliza eti Postamasta anafanya kazi gani?
 
Nilishawaambia mara kadhaa nchi inaongozwa na under age kulingana na majukumu wanayopaswa kufanya, wengi wanaomsaidia mteuzi ni type ya kina Gerson Msigwa
 
Je Magufuli aliwezaje bila kuleta mgao na wakati huo huo mvua dusko zilikuwa zinaleta ukavu?

Je Magu alitudanganya kuwa wanafungulia maji ili kutengeneza punguzo la maji kwenye mabwawa kwa minajili ya biashara zao?
 
Hakuna Mkurugenzi wa posta bwana bali ni postamasta mkuu msitake kupambapamba wakati mtu kashushwa
 
Je Magufuli aliwezaje bila kuleta mgao na wakati huo huo mvua dusko zilikuwa zinaleta ukavu?

Je Magu alitudanganya kuwa wanafungulia maji ili kutengeneza punguzo la maji kwenye mabwawa kwa minajili ya biashara zao?
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…