FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Unaonesha huelewi mipango inayoendelea sasa hivi ya kuifanya posta kuwa taasisi kubwa sana kuliko unavyofikiria.Umofia kwenu
Uteuzi uliofanywa na Rais Samia kwa kumtoa Maharage Chande TANESCO na kumpeleka kuwa Mkurugenzi TTCL na hatimaye ndani ya siku mbili akamteua kuwa PostaMasta inaleta tafakuri jadidifu kidogo.
Sisi wanaNzengo tunaweza kuwa na maswali yanayosumbua bongo zetu
CC: Pascal Mayalla Erythrocyte Retired Mshana Jr johnthebaptist Kidu52 Money Penny Dr Akeelah masa2000 Kigogo333 raraa reree Extrovert FaizaFoxy ChoiceVariable Lucas mwashambwa
- Cheo cha Postamsta kina nafasi gani kwenye madaraja ya utumishi wa umma?
- Sababu zilizosababisha aondolewe TANESCO zinafanana na zilizopelekea aondolewe TTCL?
- Mteuzi yaani Rais, anatuma ujumbe gani kwa umma kwa teuzi hizi kanganyifu? Yaani leo unamteua huyu unamuweka mahala fulani lakini kesho yake unamuondoa hapo kumpeleka kwingine
- PostaMasta anafanyakazi chini ya Mkurugenzi wa Posta. Je kwa level aliyofikia Maharage Chande inampa hadhi hiyo ama inamshusha hadhi awe hivyo?
- Kama endapo kuna sababu zinazoligharimu Taifa kwa kumuondoa Chande TANESCO, je aendelee kuligharimu Taifa huko aendako au alipata ajali ta kiutendaji?
- Je tuendelee kuamini kwamba Rais yupo makini kusimamia utumishi wa umma au anatekeleza matakwa ya waliomzunguka bila kuzingatia manufaa ya Umma?
- Je, CCM sasa inatapatapa kulazimisha maji kupanda mlima baada ya kukosa kuungwa mkono na wananchi ambapo kupitia kauli za makada waandamizi kwamba hata ikishindwa uchaguzi haiondoki madarakani?
- Kwa utendaji huu wenye mashaka mengi wa marais wa CCM l, je ni mara ngapi CCM imeipindua serikali kwa kuiba matokeo ya chaguzi mbalimbali nchini?
- Mkeka wa teuzi wa jana, umeonesha uwepo wa ombwe la utumishi wa umma. Tutarajie nini kwenye utendaji wenye kuleta matokeo?
Posta inakwenda kuwa ni kituo cha huduma zote za jamii zinazotolewa na serikali. Itafanya kazi na itakuwa na mambo yote muhimu, mfano kupata kitambulisho cha taifa, kupata passport, kupata leseni, kupata vyeti vyote vinavyohusu RITA. Mpaka sim card za simu itafikia wakati ni posta tu watakaozitowa, ili kukomesha wizi wa matapeli wanaotumia simu.
Kusambaziwa barua na vifurushi mpaka mlangoni kwako. Kuuziwa chochote kupitia mfumo wa posta na kufikishiwa ulipo, kuanzia vya ndani ya Tanzania mpaka vya nje ya Tanzania. Na mengine mengi sana.
Katazame uzinduzi wa makao makuu ya posta yaliyofanyika Arusha ujionee na kujisikilizia posta inakuwaje.
Hilo ni bonge la promotion, jamaa hapo sasa aoneshe uwezo wake.