Maharage Chande kutoka Ukurugenzi TANESCO hadi Postamasta - amepanda au ameshuka?

Unaonesha huelewi mipango inayoendelea sasa hivi ya kuifanya posta kuwa taasisi kubwa sana kuliko unavyofikiria.

Posta inakwenda kuwa ni kituo cha huduma zote za jamii zinazotolewa na serikali. Itafanya kazi na itakuwa na mambo yote muhimu, mfano kupata kitambulisho cha taifa, kupata passport, kupata leseni, kupata vyeti vyote vinavyohusu RITA. Mpaka sim card za simu itafikia wakati ni posta tu watakaozitowa, ili kukomesha wizi wa matapeli wanaotumia simu.

Kusambaziwa barua na vifurushi mpaka mlangoni kwako. Kuuziwa chochote kupitia mfumo wa posta na kufikishiwa ulipo, kuanzia vya ndani ya Tanzania mpaka vya nje ya Tanzania. Na mengine mengi sana.

Katazame uzinduzi wa makao makuu ya posta yaliyofanyika Arusha ujionee na kujisikilizia posta inakuwaje.

Hilo ni bonge la promotion, jamaa hapo sasa aoneshe uwezo wake.
 
." Sababu ni zile zile. Watu wengi waliomba asiendelee kuwepo pale TTCL kwa sababu zile zile zilizomtoa TANESCO.

Huko Posta hakuna kukuru kakara zilizoko TTCL na TANESCO. Sasa amepangiwa eneo la kazi linaloonekana kwendana na uwezo wake wa kufikiri, kuhukumu na kutenda.

Rais amefanya uamuzi sahihi na kwa wakati sahihi. Pia, Rais amejisahihisha haraka.
NAUNGA MKONO HOJA
 
He is a right person pale TTCL kwa uzoefu wake aliopata akiwa private sector! Lakini mamlaka inajua tusiyojua. Namtakia heri kwenye majukumu yake mapya.
 
Ni mpumbavu tu anaweza amini hiki unachokisema..hapo walipo kwa majukumu hayo waliyo nayo posta wameshindwa kuleta tija, biashara ndogo kabisa ya kusafirisha vifurushi na vitu vidogo vidogo mtu anaona bora awape wenye mabasi kuliko kupeleka posta..hayo yoooote uliyoorodhesha watayaweza???
 
kabisa bi dada nilikuwepo chuga wakati wa uzinduz4 endapo yote yaliyopo kwenxe makaratasi yatfanyiwa kazi.
 
mama is a total failure in all aspects
 
Kama kawa
Kama dawa
Viwanda vya kuupaka rangi uongo vinaendeleza legacy
 
mama is a total failure in all aspects
Kuna hawa Watanzania wenzetu wanajifanya kusifia hata uozo unaofanyika badala ya kumshauri kwa haki.

Nchi ni kama inaongozwa kupitia maabara yaani tunafanya majaribio kila sekta
 
POSTA ipo kwenye TRANSFORMATION na bora POSTA kuliko TTCL iliyojifia na yenye MADUDU mengi.

Jamaa kapata sehemu ambayo anaanza nayo from scratch yan strategically wise jamaa anaenda kuipika Posta.

Sasa ni yeye kuamua kuiua au kuiweka vizuri zaidi.

Posta ni ya Kimataifa zaidi.
 
Ulitaka upewe wewe wadhifa wa Maharage?
Sina hata ndoto hiyo.

Nchi inaendeshwa kama tupo maabara tunafantiwa majaribio.

Imefika mahala sasa kila kitu lazima itoke idhini ya Rais. Umeme aidhinishe, maji aidhinishe itafika mahala hata ndoa zitasubiri idhini yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…