scolastika
JF-Expert Member
- Jan 26, 2019
- 3,863
- 5,719
kwa sababu naamini hiyo bibliaKwa kuwa jambo fulani biblia imeelekeza hata kama si sahihi ina kulazimu wewe kulitekeleza ?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kwa sababu naamini hiyo bibliaKwa kuwa jambo fulani biblia imeelekeza hata kama si sahihi ina kulazimu wewe kulitekeleza ?
Unaamini mwanamke mzinifu anapaswa kupigwa mawe mpaka kufa ? Na wanawake hawapaswi kuongea chochote kile ndani ya nyumba zenu za ibada bali wakawaulize wanaume zao majumbani kwao ?kwa sababu naamini hiyo biblia
Mababu zetu na mabibi zetu walio nunuliwa kipindi Cha utumwa kwa vipande vya fedha/mali wali heshimishwa na wazungu na waarabu si ndivyo mkuu unataka kumaanisha ?Mahali Ni heshima,
Heshima kwa mkeo,
Heshima kwa wakweo,
Heshima kwa wazazi wako,
Mahali Ni ishara ya uanaume.
Uwezo wa kua Kichwa Cha familia
Huwez kujilipia mahali,kataa ndoa usioe
Wewe na huyo unayetaka kumuoa katika uchumba wenu umewahi kutenga muda na kuelimishana ni kwa namna gani mahari ina tengeneza taswira mbaya juu yake? Mpe muda wa kufikiria hilo.Dah unanishauri vp mkuu,maana mwezi ujao napeleka mahari huko Uchagani.
Ni hatari sana kwa hatua hii tuliyo fikia kwa kuwa thaminisha binadamu kwa viwango mbalimbali vya kifedha, hatua hii ina shusha utu wa binadamu kwa kiwango kikubwa sana.Week tatu nyuma nilialikwa na bwana mdogo mmoja ni bodaboda driver hawa wanaojitambua hawa,mwenza wake ni Mkigoma/Muha alichoambiwa kilinisikitisha sana.
Alitajiwa vitu kushushwa hesabu ikafika 6mill +,nilichomshauri??Legendaries wameshaelewa maana nilimwambia live kwa hatua hiyo hutatoboa.
Hatari sana, mahari kwa jamii kubwa za hapa duniani hupangwa na wazazi na wao ndio huamua mtumwa wao wana muuza bei gani kwa bwana mtumwa . Je ni million 2,5,10 n.k, ni ng'ombe 5,7,10 n.kMahari ni nini unapaswa kujua, mahari anapewa nani unapaswa kujua na ni kwa nini unapaswa kujua.
Maana yoote ya mahari inaharibiwa na wazee kwa tamaa zao wao.
Mahari si ya mzee, wala mjomba, wala mama yake
mahari ni zawadi kwa mke mtarajiwa, kwa mapenzi yake anasema mie zawadi yangu ni kitu fulani, nawe kwa kuonesha unamthamini unamtafutia hicho, na watu wanaopenda wala hawataji mivitu ya thamani saaana, wengine hutaja kitu kidogo mnoo, nawe unakipeleka kwa heshima na upendo, kuonesha unamthamini mwenzio
Sio zee linasema mie bila milioni 15 huoi mwanangu, unabaki kujiuliza siku mwanae akiumwa nitamtafuna yeye, ama je vaada ya kumpa hizo fedha ndio tumemalizana, sintopigiwa simu mwanangu sukari imeisha nyumbani, sijui shemeji yako karudishwa shule ada hakuna, sijui mama yako jino linamsumbua.
Tamaa za watu ndio zimeharibu mantiki nzima ya mahaRi.
Habari za sasa wanachama wa Jamiiforums natumai wote ni wazima wa afya, nilikuwa na jambo lini kereketalo moyoni mwangu lihitwalo “MAHARI”
Nilikuwa na tatizo na huu utamaduni ulio zoeleka hapa dunia mpaka kukomaa wa malipo ya kifedha/mali kwa mwanaume/mwanamke ili kuweza kukidhi vigezo vya kuoa au kuolewa.
Mahari ni kitendo kinacho shusha utu wa watu hapa duniani kwa wake na kwa waume hauna tofauti na biashara ya utumwa iliyo kuwa imemea hapa duniani Karne za 19 kurudi karne nyuma iliyo husisha kununua watu walio thaminishwa kwa viwango mbalimbali vya kifedha na kimali kutokana na maumbile yao na uwezo wao wa kinguvu.
Duniani mpaka sasa kwa asilimia kubwa watoto wa kike wana thaminishwa kama bidhaa sokoni kwa kigezo cha mahari kama utamaduni kitu ambacho kinavunja utu wa mtu kwa kuwa mtu hawezi kuthaminishwa kwa kiwango chochote kile cha fedha au mali.
Sasa wazazi wameshikwa na viburi vya kitamaduni za kitumwa kwa kuwa thaminisha wanao kutokana na tabia nzuri walizo nazo wanao au uzuri wa rangi/ maumbile ya wanao na kutaja viwango mbali mbali vya kifedha au mali mfano [ Mzazi anasema“ hauwezi kuoa mwanangu bila million 5-10 au bila ng'ombe 10-2 ]
Huu utamaduni wa mahari ulio mbaya unao vunja utu wa watu hapa dunia umekaliwa kimya sana na dunia tofauti na tamaduni nyingine kama ukeketaji, ndoa za utotoni, biashara ya utumwa wakati wa ukoloni n.k hizi ni baadhi ya tamaduni zilizo pigiwa kelele na dunia mpaka kukoma nyingine kupungua kwa kasi sana hapa duniani.
Ushauri binafsi: Kwa nini fedha/mali zinazo tumika kukamilisha biashara hii ya utumwa[ mahari ] visiwanye wazazi wa pande zote mbili wakutane kwa pamoja na kukusanya fedha ua mali hizo kwa pande zote mbili na kuwa changia watoto wao fedha za kuanzia maisha yao kitu ambacho kitakuwa msaada kwao na kwa maisha yao.
Maswali:
1. Kwa nini dunia ipo kimya kuhusu komaa kwa biashara hii ya utumwa ya kuuza watu kwa kigezo cha tamaduni ?
2. Licha ya kuwa wanawake ndio waathirika wakuu wa biashara hii ya utumwa iitwayo mahari, kwa nini wame likalia kimya swala hili ?
3. Kwa nini wapiganiaji wakuu wa swala la usawa wa kijinsia na haki za binadamu wame likalia kimya swala hili la biashara ya utumwa linalo vunja utu wa binadamu kwa kigezo cha mahari ?
4. Je ni haki na ni sahihi mtu kuendelea kuthaminishwa kwa viwango vya kifedha au mali ?
5. Kwa nini wanawake walio wengi hawataki kuolewa bila kunuliwa ? Na hutambiana wao kwa wao kwa viwango vya kifedha au mali vilivyo tumika kuwa nunua ?
Karibuni wadau kwa michango yenu, Ila zingatieni zaidi mada husika na maswali tajwa.
Mkuu wewe ni great thinker tatizo 90% ya JF humu ni wajuaji sana hawawezi kufikiria wao ni matusi tu kisa kakaririshwa. Mfano mtu anasema eti Toka enzi za mababu ila ukimwambia aache Uislam na ukristo akatambike uone kama atakubali? Au ampeleke Binti yake kukeketwa atakubali?Kulikuwa hakuna ulazima ndugu wa kutumia lugha chafu katika huu mjadala, lugha chafu inapoteza maana na nguvu ya hoja zako. Jitahidi kutumia lugha nzuri ndugu utaeleweka tu ujumbe wako.
Karibu tena kwa hoja zako ndugu
Kwa hiyo ndugu userious wa waarabu na wazungu katika biashara ya kununua watu ilipimwa kupitia viwango vya fedha na mali walivyo kuwa wana tunishiana kuwa ni nani kati yao mwenye uwezo wa kununua mababu na mabibi zetu kama watumwa kwa pesa au mali nyingi ? Kwa hiyo ni sahihi kwa sasa sisi kurudisha biashara ya utumwa na kuendelea kuruhusu kununua watu kama bidhaa za sokoni ?Mahari siyo biashara.Hii inapima userious wako wewe muoaji(level of commitment) lakini pia heshima ya huyo anayeolewa.Humo ndani kuna mambo ya desturi pia.ukiona unaanza kuhofia mambo ya mahamahali wakati wa kufanya maamuzi ya kuoa ujue wewe hujawa tayari kuoa.solution inabidi u-step back kwanza
Mkuu vipi mila ya tohara upo tayari? Kwanini wewe ni mkristo au Muislam wakati Mila inataka ukatambikie mizimu?Mahari siyo biashara.Hii inapima userious wako wewe muoaji(level of commitment) lakini pia heshima ya huyo anayeolewa.Humo ndani kuna mambo ya desturi pia.ukiona unaanza kuhofia mambo ya mahamahali wakati wa kufanya maamuzi ya kuoa ujue wewe hujawa tayari kuoa.solution inabidi u-step back kwanza
Kweli kabisa ndugu, kuna tatizo kubwa sana katika jamii juu ya hili swala na uzito gani hasi linapewa ili liweze kupigwa vita ni mdogo sana tofauti na uzito chanya linalo pewa ili liendelee kukomaa kabisa ndani ya jamii .Mkuu wewe ni great thinker tatizo 90% ya JF humu ni wajuaji sana hawawezi kufikiria wao ni matusi tu kisa kakaririshwa. Mfano mtu anasema eti Toka enzi za mababu ila ukimwambia aache Uislam na ukristo akatambike uone kama atakubali? Au ampeleke Binti yake kukeketwa atakubali?
Mimi binafsi sijawahi penda hii issue, unakuta Binti anajadiliwa kama bidhaa yaani wanaithaminisha Mali as if anauzwa!! Kama issue ni Hela kwani baada ya ndoa huwa wazazi hawaombi hela?
Hii mila ni mbovu sana
Yakobo alioa wake wawili vipi nyie mnaruhusiwa kanisani? Yakobo huyo huyo alizaa na Vijakazi wake wawili vipi kanisani kwenu mnaruhusiwa?mahari ipo mpaka kwa biblia tangu yakobo alichunga kwa miaka saba kama malipo ya kuchukua mke,malezi ya mtoto wa kike sio kazi ndogo