Mahari ni biashara ya utumwa. Kwanini dunia ipo kimya?

Screenshot_20221130-091241.jpg
Screenshot_20221130-090942.jpg
Screenshot_20221130-090949.jpg
Screenshot_20221130-090956.jpg
Screenshot_20221130-091001.jpg
 
Mimi sioni hivyo, ni zawadi tu 🥴
Hapana, wewe Kama mwanaume unge kubali kutolewa mahari ? Kwa wazazi wa pande mbili kukaa kuafikiana ni bei gani wanaweza kuuziana mtu ambaye ni wewe ? Mfano. Mzazi wako aseme 1 million na mzazi mwengine aseme laki 1 halafa mwisho waafikiane bei ya kuku uza ?

Hii kitu ina vunja utu wa mwanadamu ina paswa kupigwa vita na mwanadamu yoyote anaye jitambua.
 
Ila katika ualisia wa kibinadamu ni nini ?
Unamaanisha nini kusema "ualisia" wa kibinadamu?

Mimi nasema katika Uislam, mahari ukiangalia maana yake na mafundisho kuhusiana nayo kisha ukaangalia mafundisho na Sharia kuhusu Ibada nzima ya ndoa, mahari sio biashara ya utumwa.

Sijui kwenu mahari ni nini. Lakini katika Uislam mahari ni zawadi anayopewa mwanamke na mwanaume anayetaka kumuoa ili kuonesha ukweli wa kutaka kwake kumuoa na ni jambo la wajibu lililowekwa na Allah katika Qur'an kama haki ya mwanamke. Na haisihi ndoa katika Uislam bila ya mahari.

وآ توا النساء صدقاتهن نحلة

“Na wapeni wanawake mahari yao…” (An-Nisaa: 4)

يا أيها النبي إنا أحللنا لك أزواجك اللاتي آتيت أجورهن

“Ewe Nabii! Tumekuhalalishia wake zako uliowapa mahari yao…” (Al-Ahzaab: 50)

فما استمتعتم به منهن فآتوهن أجورهن فريضة

“ … basi wale mnaowaoa miongoni mwao wapeni mahari yao yaliyolazimishwa…” (An-Nisaa: 24)

Na mahari haina kiwango maalum ni makubaliano ya wao wawili (akitaja mwanamke au mwanaume aki offer kisha mwanamke akakubali kwa hiyari yake) na ni haki ya mwanamke mwenyewe sio wazazi au walezi. Inaweza kuwa Mali au jambo jengine. Sio pesa tu na ng'ombe. Inaweza kuwa ni vitu mbali mbali kulingana na ada na makubaliano. Na ni mwanamke mwenyewe ndie anataja na kuridhia. Na ikapendekezwa mahari iwe ndogo

Kuna ambao wanatoa Pete kama mahari, kuna ambao walioa na mahari yao ilikuwa ni kile walichokihifadhi katika Qur'an (yaani kiwango walichohifadhi katika Qur'an ) ndio ilikuwa mahari nk.

Ngoja nikupe mfano mmoja tu kutoka zama za Mtume kukuonesha; wakati wa Mtume(SwallaAllahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam) kulikuwa na Swahaba anaitwa Abu Talha (Radhwiya Allahu 'Anhu), Abu Talha alitaka kumuoa Umm Sulaym (Radhwiya Allahu 'Anha), lakini wakati Abu Talha anamposa Umm Sulaym, alikuwa sio Muislam. Umm Sulaym akamuambia Abu Talha; "Wa Allahi, mtu mfano wako harejeshwi, ila wewe sio muislam na mimi ni muislam, na haiwi halali kwangu kuolewa nawe, ukisilimu hiyo ndio mahari yangu na sitotaka kengine zaidi ya hilo". Abu Talha akasilimu na kule kusilimu kwake ndio ikawa ni mahari ya Umm Sulaym (Allah awe radhi nao wote wawili).

Kuna ambao mahari waliyoiridhia ilikuwa ni viatu (ndala mbili) kama yule mwanamke kutoka kabila la Bani Fazara na Mtume akamuuliza kama ameridhia hilo, akamjibu kuwa karidhia.

Sijui nikufafanulieje mimi sio fasaha sana, ila elewa kuwa katika Uislam mahari ni tofauti na unavyoelewa wewe.

Kazakh destroyer

Allah anajua zaidi.
 
Kwa hiyo kwa kuwa mahari ime hararishwa kwenye Quran basi hauna budi kuzitekeleza pasipo hata kutazama nafasi ya mtu kuthaminishwa na bidhaa za sokoni au kitu chochote ?

Kwa hiyo kwako kila jambo lililo rasimishwa ndani ya quran unapaswa kulitekeleza pasipo hata kuhoji uhalali wa hilo Jambo ? Je ni mambo mangapi yapo kwenye Quran lakini haupo tayari kuya tekekeza ?

Je upo tayari kupigana Vita za jihad za kumwaga damu za watu ? Je upo tayari kupiga mawe mwanamke mzinifu mpaka kufa ?

Kwa nini usitazame nafasi ya mtu kuwa haipaswi kuthaminishwa na kitu chochote kile ?

Je ni sahihi waarabu na wazungu kurudi na kuendeleza biashara ya utumwa maana pia vitabu vyenu vya dini vimerasimisha hilo swala ? Upo tayari kununuliwa kama mtumwa kupitia vitabu vyenu vya kiimani ?

Nisingependa sana tuanzishe mjadala wa kidini uta hamisha kabisa hii mada yote na kugeuka kuwa mada ya mapambano ya kiimani, unapaswa kuitazama nafasi ya utu wa mwanadamu kwa jicho la tatu kwa utulivu zaidi ?

Je ungekuwa wewe mwanume una fanyiwa hivyo ni kwa kiasi gani ingeshusha utu wako ndani ya jamii pasipo wewe kufahamu au kufahamu ? tunapaswa kutafakari haya Mambo kwa kina zaidi.
 
Naona unaanza kulalamika.

Nasikitika kusema hatujaelewana kabisa. Yawezekana unavyofahamu kuhusu mahari au unacholazimisha watu wakifahamu kuhusu mahari sivyo tunavyofahamu sisi Waislam.

Halafu hayo mambo mengine uliyoandika naona hujui kuhusu Uislam. Ungekuwa unajua kuhusu Uislam usingeniuliza maswali hayo.

Mimi ni Muislam (na ninajivunia mno hilo al hamdulillaah), nimejisalimisha kwa Allah. Nimesikia na ninatii. Unapotaka nisiikubali Qur'an maana yake unataka nisiwe Muislam hiko ndicho unachomaanisha. Na kuwa kwangu Muislam ni LAZIMA niikubali na niifuate Qur'an.

Siku nyengine elewa hili aiseeee. Kwa Muislam Dini yake ni muhimu na ya thamani mnooo.

Allah akuongoze.
 
Dini ni muhimu kwako lakini utu wa mwanadamu unapaswa kuwa muhimu zaidi kwako kuliko dini, sawa ndugu kuwa na siku njema.
 
Hapana, wewe Kama mwanaume unge kubali kutolewa mahari ? Kwa wazazi wa pande mbili kukaa kuafikiana ni bei gani wanaweza kuuziana mtu ambaye ni wewe ? Mfano. Mzazi wako aseme 1 million na mzazi mwengine aseme laki 1 halafa mwisho waafikiane bei ya kuku uza ?

Hii kitu ina vunja utu wa mwanadamu ina paswa kupigwa vita na mwanadamu yoyote anaye jitambua.
Tatizo umekariri kuuza. Ni zawadi. Badilisha mtazamo 🥴
 
Hapo bado hujawaudumia ndugu wa mkeo, lini tutapiga hatua kiuchumi?
 
Back
Top Bottom