Mahari ni biashara ya utumwa. Kwanini dunia ipo kimya?

Wacha mabinti wapate zawadi bwana 🥴
Basi tulipaswa pia kuacha mababu na mabibi zetu waendelee kutolewa zawadi kwa mabwana watumwa mpaka nasi pia tunge tolewa hiyo zawadi unayo isema si ndivyo ?
 
Hapo bado hujawaudumia ndugu wa mkeo, lini tutapiga hatua kiuchumi?
Hii changamoto kubwa sana kwenye jamii, sema ndivyo sasa jamii imevaa kitambaa cheusi juu ya hili swala.

Tunapaswa kuwa wezesha watoto wetu pesa ya kuanzia maisha na sio pesa ya kununua binadamu mwenzako[ mke] kwa kisingizio cha mahari.
 
Na rambirambi tusitoe basi maana kwa mtazamo wako utaona tunalipia kifo cha mtu 🥴
 
Ndoa ni utumwa?
Ndoa haiwezi kutafisirika utumwa kama haijatumia kiunganishio cha mahari ila kama imefanya kiunganishio cha mahari hio tayari ina kuwa biashara ya utumwa imefanyika hapo.
 
Na rambirambi tusitoe basi maana kwa mtazamo wako utaona tunalipia kifo cha mtu 🥴
Tuzingatie mada husika kwanza hilo la rambi rambi nalo linaweza kupatiwa muda wake wakati mwingine.
 
Unaamini mwanamke mzinifu anapaswa kupigwa mawe mpaka kufa ? Na wanawake hawapaswi kuongea chochote kile ndani ya nyumba zenu za ibada bali wakawaulize wanaume zao majumbani kwao ?

Nisinge penda sana tuanzishe mjadala wowote wa kidini lakini kwa hayo machache wenda yata fungua fahamu zako kidogo.

Sitegemee kuona mwana mama akiunga mkono utoaji wa mahari wa kifedha kitu ambacho ni mfanano na mtu kwenda kununua nyanya sokoni, sifikiri kama binadamu amekosa utu kiasi hiki mpaka kufananishwa na bidhaa za sokoni.

Karibu kwa hoja ndugu
Mambo ya Imani bora mlivyosema myaache maana mijadala yake Huwa ni mirefu especially inapotokea mjadala kati ya mtu mwenye Imani husika aliyefunzwa mambo ya Dini na kugraduate kwenye hizo issue na mtu/msela wa kitaa ambaye hana Imani na hajafunzwa kokote pale ila yeye anasoma maandiko na kutafsiri vile anavyoona sawa na yupo specifically kwaajili ya kumkosoa mwezake mwenye Imani.

Hamuwezi fikia muafaka. Unakuta huyu anaamini hivi na yule analazimsha mwezake aamini vile anavyoona yeye Iko sawa. Yaani ni vurugu mechi.
 
Ndoa haiwezi kutafisirika utumwa kama haijatumia kiunganishio cha mahari ila kama imefanya kiunganishio cha mahari hio tayari ina kuwa biashara ya utumwa imefanyika hapo.
Mahari ni zawadi, jamii nyingine mwanamke ndo anatoa, labda ukipata wewe hutoona shida. Kuulizana kiasi sio shida kwani ni kawaida kumuuliza mtu umnunulie zawadi gani, shida ladba ni kukataa kutoa mke wakati mume hana uwezo na kiasi kilichotajwa ndo inageuka biashara 🥴
 
Mababu zetu na mabibi zetu walio nunuliwa kipindi Cha utumwa kwa vipande vya fedha/mali wali heshimishwa na wazungu na waarabu si ndivyo mkuu unataka kumaanisha ?
Brother ulishawahi kusikia kitu kinaitwa PURPOSE au kwa kiswasili tunaita LENGO au DHUMUNI ?

Unajuwa pesa inaweza kuwa sadaka, nauli, ada, rushwa, hongo au mshahara, yaani inategemea tu, imetumika kwa LENGO Gani ?

Swala la mahari huenda wewe ukawa unalielewa tofauti na vile linavyopaswa kueleweka au inawezekana kwenye jamii yenu au ukoo wenu au tamaduni zenu au Imani au Dini yako ikawa inafanya mambo tofauti na wengine ndiyo maana ukawa na unaelewa tofauti.

Ni Iko hivi,katika tamaduni na Imani au Dini nyingi duniani mwanaume ni kiongizi wa familia na huu uongozi unakuja na majukumu ambayo yanamtaka mwanaume kuwa provider na protector wa familia.

Kwenye kumuasses mwanaume kama anauwezo wa kutekeleza hayo majukumu yake kila tamaduni,Imani au Dini Zina taratibu zake yapo makabila ambayo yalitaka muoaji ( mwanaume ) akaue Simba Ili kuonesha uweza na utayati wake kwenye kupenda,kuhudumia na kutunza familia to the point atakuwa tayari kujisacrice for the sake of his family especially his wife mfano wamasai walikuwa wanafanya hivyo.

Kuna jamaa kule juu kakuelezea namna ambavyo wachaga wanahitaji ng'ombe and the list goes on and on.

Sasa hii sio biashara ya kuuziana watu maana wanaotoa pesa na wanaoenda kuua simba, pia wanaopeleka cherehani na vitu kadha wa kadha, Hivi vitu havimaanishi kuwa wanauziana watu(wanawake) ni inategemea tu na malengo Yao ni nini, Sasa huwezi kuapply mtazamo wako kwenye kila tamaduni ilihali hufahamu DHUMUNI la hizo tamaduni kufanya hivyo ni nini.

ZINGATIA; Pesa inaweza kuwa SADAKA, ADA, NAULI,H HONGO, RUSHWA au MSHAHARA inategemea tu imetumika kwa malengo gani na huwezi lazimisha kila mtu anayetoa pesa awe ametoa rushwa ilihali DHUMUNI la kutoa pesa hulijuwi.
 
Mahari ni kipimo (testing) ya wewe kuweza kumudu huyo unaehitaji kuishi nae km Mahari inakushinda je huyo unaehitaji kuishi nae utamuweza? Wazee walioanzisha mahari hawakua mafala
 
Unaamini mwanamke mzinifu anapaswa kupigwa mawe mpaka kufa ? Na wanawake hawapaswi kuongea chochote kile ndani ya nyumba zenu za ibada bali wakawaulize wanaume zao majumbani kwao ?

Nisinge penda sana tuanzishe mjadala wowote wa kidini lakini kwa hayo machache wenda yata fungua fahamu zako kidogo.

Sitegemee kuona mwana mama akiunga mkono utoaji wa mahari wa kifedha kitu ambacho ni mfanano na mtu kwenda kununua nyanya sokoni, sifikiri kama binadamu amekosa utu kiasi hiki mpaka kufananishwa na bidhaa za sokoni.

Karibu kwa hoja ndugu
[emoji294][emoji294][emoji294][emoji294][emoji294][emoji294]
 
Unaamini mwanamke mzinifu anapaswa kupigwa mawe mpaka kufa ? Na wanawake hawapaswi kuongea chochote kile ndani ya nyumba zenu za ibada bali wakawaulize wanaume zao majumbani kwao ?

Nisinge penda sana tuanzishe mjadala wowote wa kidini lakini kwa hayo machache wenda yata fungua fahamu zako kidogo.

Sitegemee kuona mwana mama akiunga mkono utoaji wa mahari wa kifedha kitu ambacho ni mfanano na mtu kwenda kununua nyanya sokoni, sifikiri kama binadamu amekosa utu kiasi hiki mpaka kufananishwa na bidhaa za sokoni.

Karibu kwa hoja ndugu
Nakubaliana nawewe
 
Mambo ya Imani bora mlivyosema myaache maana mijadala yake Huwa ni mirefu especially inapotokea mjadala kati ya mtu mwenye Imani husika aliyefunzwa mambo ya Dini na kugraduate kwenye hizo issue na mtu/msela wa kitaa ambaye hana Imani na hajafunzwa kokote pale ila yeye anasoma maandiko na kutafsiri vile anavyoona sawa na yupo specifically kwaajili ya kumkosoa mwezake mwenye Imani.

Hamuwezi fikia muafaka. Unakuta huyu anaamini hivi na yule analazimsha mwezake aamini vile anavyoona yeye Iko sawa. Yaani ni vurugu mechi.
Kweli ndugu.
 
Mahari ni zawadi, jamii nyingine mwanamke ndo anatoa, labda ukipata wewe hutoona shida. Kuulizana kiasi sio shida kwani ni kawaida kumuuliza mtu umnunulie zawadi gani, shida ladba ni kukataa kutoa mke wakati mume hana uwezo na kiasi kilichotajwa ndo inageuka biashara 🥴
Sio kwamba siungi tumkono mwanamke kutolewa mahari pia hata kwa wanaume wanao tolewa mahari napo siungi mkono.

Huu ni udhalilishaji wa utu wa mwanadamu kutafsiriwa kama bidhaa sokoni na wala sio zawadi, utu wa mwanadamu haupaswi kufananishwa na chochote kile.
 
We utakuwa na wivu si bure 🥴 wacha mabinti watolewe mahari kuwe na shamra shamra nyumbani
 
ulieanzisha uzi popote ulipo kunywa soda 5 nakuja kulipa naisi tukipata watu 10 kati ya 100 wenye mawazo km wewe hskika taifa litasonga mbele
 
Back
Top Bottom