Mahari ni biashara ya utumwa. Kwanini dunia ipo kimya?

Mahari ni biashara ya utumwa. Kwanini dunia ipo kimya?

Mahali Ni heshima,
Heshima kwa mkeo,
Heshima kwa wakweo,
Heshima kwa wazazi wako,
Mahali Ni ishara ya uanaume.
Uwezo wa kua Kichwa Cha familia
Huwez kujilipia mahali,kataa ndoa usioe
Mkuu nadhani mtoa mada Hana shida na mahari ila Ile "process" inakua kama slave trade!! Kuna familia naijua walikomaa wapewe million 8 wakati familia zote mbili ni maisha duni. Jamaa mpaka analilia wajomba wampunguzie eti ndio heshima??

Kwanini isiwe tu discretion ya anayeoa? Kwamba Ni zawadi tu kama appreciation sio Tena majadiliano ya kushushana bei.

Mimi binafsi naona Ile "process" inadhalilisha sana Binti.
 
Yakobo alioa wake wawili vipi nyie mnaruhusiwa kanisani? Yakobo huyo huyo alizaa na Vijakazi wake wawili vipi kanisani kwenu mnaruhusiwa?

Au ndio biblia nzuri ikitaja mahari ila ikitaja yakobo kula mabeki tatu unajikausha? Weird
Maswali muhimu sana
 
Mahali ni kama agano lenye lengo la kutimiza kitendo cha muunganiko wa jinsia mbili zilizoamua kuishi pamoja. Hata hio mahari haitoshi kulipia gharama za mzazi alizotumia kumlea binti.
Kwani kijana wa kiume haku lelewa na wazazi ? Na je waarabu na wazungu wali nunua mababu na mabibi zetu ili kulipia gharama za wao kulelewa na wazazi wao si ndivyo unavyo maanisha ndugu ?
 
Mkuu nadhani mtoa mada Hana shida na mahari ila Ile "process" inakua kama slave trade!! Kuna familia naijua walikomaa wapewe million 8 wakati familia zote mbili ni maisha duni. Jamaa mpaka analilia wajomba wampunguzie eti ndio heshima??

Kwanini isiwe tu discretion ya anayeoa? Kwamba Ni zawadi tu kama appreciation sio Tena majadiliano ya kushushana bei.

Mimi binafsi naona Ile "process" inadhalilisha sana Binti.
Kweli ndugu, vijana wanao oana wanapaswa kupewa hizo fedha kwa ajili ya kuanzia maisha yao na sio moja kati yao kunulika kama mtumwa kwa kigezo cha mahari.

Pande zote mbili za familia za wazazi wa mtoto wa kike na wazazi wa mtoto wa kiume wote wanapaswa kuchanga hizo fedha kwa ajili ya wanao katika maisha yao wanayo enda kuya anza.
 
Sijui umeitazamaje Mahari ila tambua kuwa kwa Waislam katika Uislam Mahari ni wajibu wa Kishariah, ni moja katika mambo ya wajibu kishariah.

Katika Uislam, bila Mahari haisihi ndoa.
 
Mkuu wewe ni great thinker tatizo 90% ya JF humu ni wajuaji sana hawawezi kufikiria wao ni matusi tu kisa kakaririshwa. Mfano mtu anasema eti Toka enzi za mababu ila ukimwambia aache Uislam na ukristo akatambike uone kama atakubali? Au ampeleke Binti yake kukeketwa atakubali?

Mimi binafsi sijawahi penda hii issue, unakuta Binti anajadiliwa kama bidhaa yaani wanaithaminisha Mali as if anauzwa!! Kama issue ni Hela kwani baada ya ndoa huwa wazazi hawaombi hela?

Hii mila ni mbovu sana
Mkuu, kwetu Waislam mahari ni sehemu ya Dini.
 
Kwani kijana wa kiume haku lelewa na wazazi ? Na je waarabu na wazungu wali nunua mababu na mabibi zetu ili kulipia gharama za wao kulelewa na wazazi wao si ndivyo unavyo maanisha ndugu ?
Mahari si utumwa,kwani mke ni mali ya nani
 
Mkuu nadhani mtoa mada Hana shida na mahari ila Ile "process" inakua kama slave trade!! Kuna familia naijua walikomaa wapewe million 8 wakati familia zote mbili ni maisha duni. Jamaa mpaka analilia wajomba wampunguzie eti ndio heshima??

Kwanini isiwe tu discretion ya anayeoa? Kwamba Ni zawadi tu kama appreciation sio Tena majadiliano ya kushushana bei.

Mimi binafsi naona Ile "process" inadhalilisha sana Binti.
Amekutana na familia ya hovyo inayogeuza mahali chanzo Cha mapato.
Mahali haitakiwi kua mzigo kwa mtoaji.
 
Unaamini mwanamke mzinifu anapaswa kupigwa mawe mpaka kufa ? Na wanawake hawapaswi kuongea chochote kile ndani ya nyumba zenu za ibada bali wakawaulize wanaume zao majumbani kwao ?

Nisinge penda sana tuanzishe mjadala wowote wa kidini lakini kwa hayo machache wenda yata fungua fahamu zako kidogo.

Sitegemee kuona mwana mama akiunga mkono utoaji wa mahari wa kifedha kitu ambacho ni mfanano na mtu kwenda kununua nyanya sokoni, sifikiri kama binadamu amekosa utu kiasi hiki mpaka kufananishwa na bidhaa za sokoni.

Karibu kwa hoja ndugu
ligi siwezi ndugu ila mahari ina heshima yake binafsi nimeolewa kwa mahari tena kubwa tu
 
Uzuri ni kwamba hata hawa wazee wachache waliobaki wameshindwa kabisa kutuelimisha vijana mahari ninini na inafaida gani hili jambo linaenda kufa lenyewe. Hakuna kijana atakuwa tayari kutoa pesa bila Ufafanuzi unaoeleweka.

Ninavyofahamu mimi,

Hapo zamani mwanamke alichukuliwa kama kijakazi kwajili ya kuzalisha Mali (kilimo, ufugaji) na kuzaa watoto wengi ili kupata nguvu kazi.

Kwakuwa mke alikuwa mfanyakazi wa hizo shughuli hapo juu ilibidi alipiwe mahari na mara moja akaanze kufanya kazi kwa mumewe.

Watu walimcheka mwanaume ambae ameomtolea mahari mwanamke mvivu.

Huu utamaduni umepitwa na wakati, mwanamke wa sasa sio mfanyakazi wa familia, ni goli kipa anasubiri aletewe kila kitu na awekewe mfanya kazi wa ndani hata kama anaingiza kipato.

Mahari haina faida yoyote, heshima inatoka moyoni iyo heshima ya kununua ni changa la macho tu.
 
Mahari haina faida yoyote, heshima inatoka moyoni iyo heshima ya kununua ni changa la macho tu.
Hakika ujumbe wako umeeleweka kabisa ndugu, hakuna shaka juu ya hilo.
 
binafsi nimeolewa kwa mahari tena kubwa tu
Sawa nimekuelewa ndugu na pongezi kwa kujivunia hivyo.
FB_IMG_1660944755202.jpg
 
Sijui umeitazamaje Mahari ila tambua kuwa kwa Waislam katika Uislam Mahari ni wajibu wa Kishariah, ni moja katika mambo ya wajibu kishariah.

Katika Uislam, bila Mahari haisihi ndoa.
Kwa hiyo ndugu hiyo shariah kwa mujibu wa imani yako imerasimisha moja kwa moja biashara ya utumwa kwa mfumo wa mahari ?
 
Back
Top Bottom