Mahari ni biashara ya utumwa. Kwanini dunia ipo kimya?

kwa sababu naamini hiyo biblia
Unaamini mwanamke mzinifu anapaswa kupigwa mawe mpaka kufa ? Na wanawake hawapaswi kuongea chochote kile ndani ya nyumba zenu za ibada bali wakawaulize wanaume zao majumbani kwao ?

Nisinge penda sana tuanzishe mjadala wowote wa kidini lakini kwa hayo machache wenda yata fungua fahamu zako kidogo.

Sitegemee kuona mwana mama akiunga mkono utoaji wa mahari wa kifedha kitu ambacho ni mfanano na mtu kwenda kununua nyanya sokoni, sifikiri kama binadamu amekosa utu kiasi hiki mpaka kufananishwa na bidhaa za sokoni.

Karibu kwa hoja ndugu
 
Mahali Ni heshima,
Heshima kwa mkeo,
Heshima kwa wakweo,
Heshima kwa wazazi wako,
Mahali Ni ishara ya uanaume.
Uwezo wa kua Kichwa Cha familia
Huwez kujilipia mahali,kataa ndoa usioe
 
Mahali Ni heshima,
Heshima kwa mkeo,
Heshima kwa wakweo,
Heshima kwa wazazi wako,
Mahali Ni ishara ya uanaume.
Uwezo wa kua Kichwa Cha familia
Huwez kujilipia mahali,kataa ndoa usioe
Mababu zetu na mabibi zetu walio nunuliwa kipindi Cha utumwa kwa vipande vya fedha/mali wali heshimishwa na wazungu na waarabu si ndivyo mkuu unataka kumaanisha ?
 
Dah unanishauri vp mkuu,maana mwezi ujao napeleka mahari huko Uchagani.
 
Dah unanishauri vp mkuu,maana mwezi ujao napeleka mahari huko Uchagani.
Wewe na huyo unayetaka kumuoa katika uchumba wenu umewahi kutenga muda na kuelimishana ni kwa namna gani mahari ina tengeneza taswira mbaya juu yake? Mpe muda wa kufikiria hilo.

Ushauri unao takiwa kupatiana ni kwa pamoja wote nyie mnao oana na wazazi wote wa pande mbili kuchangiana pesa kwa kushikirina zitakazo wasaidia kuanzia maisha mfano ununuzi wa kiwanja kama hamna , ufunguaji wa biashara, ununuzi wa vitu vya ndani kama hamna n.k

Mnapaswa kwa pamoja muifanye hiyo pesa ya mahari iwe ya kuanzia maisha yenu ya kifamilia na sio kutumika kununua huyo mke kama bidhaa sokoni au mtumwa kitu kinacho shusha utu wa mwanadamu.

Mnapaswa muelekezane kwa utulivu na muelewane vizuri wote kwa pamoja pasipo kuwa na mmoja kati yenu mwenye kinyongo juu ya hilo kauli.
 
Week tatu nyuma nilialikwa na bwana mdogo mmoja ni bodaboda driver hawa wanaojitambua hawa,mwenza wake ni Mkigoma/Muha alichoambiwa kilinisikitisha sana.

Alitajiwa vitu kushushwa hesabu ikafika 6mill +,nilichomshauri??Legendaries wameshaelewa maana nilimwambia live kwa hatua hiyo hutatoboa.
 
Mahari ni nini unapaswa kujua, mahari anapewa nani unapaswa kujua na ni kwa nini unapaswa kujua.

Maana yoote ya mahari inaharibiwa na wazee kwa tamaa zao wao.
Mahari si ya mzee, wala mjomba, wala mama yake
mahari ni zawadi kwa mke mtarajiwa, kwa mapenzi yake anasema mie zawadi yangu ni kitu fulani, nawe kwa kuonesha unamthamini unamtafutia hicho, na watu wanaopenda wala hawataji mivitu ya thamani saaana, wengine hutaja kitu kidogo mnoo, nawe unakipeleka kwa heshima na upendo, kuonesha unamthamini mwenzio

Sio zee linasema mie bila milioni 15 huoi mwanangu, unabaki kujiuliza siku mwanae akiumwa nitamtafuna yeye, ama je vaada ya kumpa hizo fedha ndio tumemalizana, sintopigiwa simu mwanangu sukari imeisha nyumbani, sijui shemeji yako karudishwa shule ada hakuna, sijui mama yako jino linamsumbua.
Tamaa za watu ndio zimeharibu mantiki nzima ya mahaRi.
 
Ni hatari sana kwa hatua hii tuliyo fikia kwa kuwa thaminisha binadamu kwa viwango mbalimbali vya kifedha, hatua hii ina shusha utu wa binadamu kwa kiwango kikubwa sana.
 
Hatari sana, mahari kwa jamii kubwa za hapa duniani hupangwa na wazazi na wao ndio huamua mtumwa wao wana muuza bei gani kwa bwana mtumwa . Je ni million 2,5,10 n.k, ni ng'ombe 5,7,10 n.k

Dunia imefika hatua hii mbaya sana, inapaswa kupigwa vita hii biashara ya watu na wala sio heshima wala kujivunia kununua watu kupitia mahari.
 

Mahari siyo biashara. Hii inapima userious wako wewe muoaji (level of commitment) lakini pia heshima ya huyo anayeolewa. Humo ndani kuna mambo ya desturi pia. Ukiona unaanza kuhofia mambo ya mahamahali wakati wa kufanya maamuzi ya kuoa ujue wewe hujawa tayari kuoa. Solution inabidi u-step back kwanza
 
Kulikuwa hakuna ulazima ndugu wa kutumia lugha chafu katika huu mjadala, lugha chafu inapoteza maana na nguvu ya hoja zako. Jitahidi kutumia lugha nzuri ndugu utaeleweka tu ujumbe wako.

Karibu tena kwa hoja zako ndugu
Mkuu wewe ni great thinker tatizo 90% ya JF humu ni wajuaji sana hawawezi kufikiria wao ni matusi tu kisa kakaririshwa. Mfano mtu anasema eti Toka enzi za mababu ila ukimwambia aache Uislam na ukristo akatambike uone kama atakubali? Au ampeleke Binti yake kukeketwa atakubali?

Mimi binafsi sijawahi penda hii issue, unakuta Binti anajadiliwa kama bidhaa yaani wanaithaminisha Mali as if anauzwa!! Kama issue ni Hela kwani baada ya ndoa huwa wazazi hawaombi hela?

Hii mila ni mbovu sana
 
Kwa hiyo ndugu userious wa waarabu na wazungu katika biashara ya kununua watu ilipimwa kupitia viwango vya fedha na mali walivyo kuwa wana tunishiana kuwa ni nani kati yao mwenye uwezo wa kununua mababu na mabibi zetu kama watumwa kwa pesa au mali nyingi ? Kwa hiyo ni sahihi kwa sasa sisi kurudisha biashara ya utumwa na kuendelea kuruhusu kununua watu kama bidhaa za sokoni ?

Kwa hiyo ni sahihi kwa sasa sisi kurudisha desturi na tamaduni za kuoza mabinti zetu katika umri mdogo pamoja na kuwa keketa si ndivyo ?

Kwa hiyo utayari wa mtu kuoa unapimwa na uwezo wake wa kifedha au mali mfukoni mwake wa kumfanikisha yeye kununua binadamu mwenzake kama mtumwa ?
 
Mkuu vipi mila ya tohara upo tayari? Kwanini wewe ni mkristo au Muislam wakati Mila inataka ukatambikie mizimu?

Hizi double standards ni kwa faida ya nani?
 
Kweli kabisa ndugu, kuna tatizo kubwa sana katika jamii juu ya hili swala na uzito gani hasi linapewa ili liweze kupigwa vita ni mdogo sana tofauti na uzito chanya linalo pewa ili liendelee kukomaa kabisa ndani ya jamii .

Ni kwa nguvu kubwa linapakwa rangi ili lionekana ni jambo jema la kitamaduni lakini kiuhalisia ni lina vunja utu wa mwanadamu hasa jinsia ya kike kwa kiwango kikubwa linavunja utu wao pasipo wao kufahamu.

Binadamu Sasa amekuwa bidhaa hana tofauti na vitumbua sokoni vina tofautiana bei kutokana na mgahawa vinapo uziwa, vitu ndani vilivyo wekewa mfano iriki, mdalasini nk, mafuta yanayo vifanya kumelemeta , kuungua kwake au kuiva kwake n.k
 
mahari ipo mpaka kwa biblia tangu yakobo alichunga kwa miaka saba kama malipo ya kuchukua mke,malezi ya mtoto wa kike sio kazi ndogo
Yakobo alioa wake wawili vipi nyie mnaruhusiwa kanisani? Yakobo huyo huyo alizaa na Vijakazi wake wawili vipi kanisani kwenu mnaruhusiwa?

Au ndio biblia nzuri ikitaja mahari ila ikitaja yakobo kula mabeki tatu unajikausha? Weird
 
Mahali ni kama agano lenye lengo la kutimiza kitendo cha muunganiko wa jinsia mbili zilizoamua kuishi pamoja. Hata hio mahari haitoshi kulipia gharama za mzazi alizotumia kumlea binti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…