Mahari sio lazima, ni mila potofu ya kupingwa

Mahari sio lazima, ni mila potofu ya kupingwa

Waafrika wengi wamewauza hata ndugu zao wanaume kwenye utumwa. Miaka 150 tu iliyopita.

Hivyo, kwenye hili la kuuza watu ili wapate pesa unaweza kubishana nao sana wasikuelewe.

Pesa inatawala, hayo mambo ya mantiki na principle hawaelewi.

Maisha yanaenda kichawichawi na kwa michezo ya pata potea sana, watu wana njaa.

Ukileta habari za principle na mantiki, wanaona unawazingua tu.

Usipolipa mahari utajua kwa nini Mbaraka Mwinshehe aliimba Wajomba Wamechacha.

RIP Mbaraka Mwinshehe, one of the best yet.

Tupo kwenye Giza Nene Mno.
Ukitumia logic utaambiwa unadharau Mila hata kama unachoongea linaingia akilini
 
Aliyekuambia Kijana wakiume hajatunzwa na kuandaliwa na Wazazi wake ni Nani?
Aliyekuambia Kijana WA kiume haandaliwi na kufunzwa Kwa ajili ya maandalizi ya kuanzisha familia ni Nani?
Aliyekuambia Mahari ni ishara ya upendo ni Nani?

Kwa nini mnawachukulia Wanawake kama Mali ya MTU mwingine? Ni Nani aliyewaambia na kuwadanganya kuwa Mtu akiolewa anamilikiwa na MTU mwingine?

Unaposema Mahari Ipo kwenye jamii zote unauhakika? Labda useme zamani Sana, Kwa sababu za Akili za kizamani, Zama za Giza kulipokuwa na biashara ya Utumwa, ambapo pia Mwanamke hakuchukuliwa kama MTU. Na wengi walikuwa Watumwa.
Nenda nchi za Ulaya alafu uwaambie hizo habari za Mahari usikie watasema nini?

Mahari ni biashara ya kuuza na kununua binadamu
Mwanaume ni JASIRI.

BORN A HERO!

NI MUWINDAJI!

Hupaswi kuwa mtu mwororo!

You get to be tough and pay dowry!

Men are Naturally Donners.

Women are Naturally recipients!

That is Naturally and it is Nature!!

Mwanaume asiyelipa Mahari ni Dhaifu !!
 
Mwanaume ni JASIRI.

BORN A HERO!

NI MUWINDAJI!

Hupaswi kuwa mtu mwororo!

You get to be tough and pay dowry!

Men are Naturally Donners.

Women are Naturally recipients!

That is Naturally and it is Nature!!

Mwanaume asiyelipa Mahari ni Dhaifu !!
Wewe kwanza jifunze spelling za hiyo lugha ujue tofauti ya donors na donners kabla ya kujifaragua kuwapa watu ushauri kwenye mambo ya kifalsafa ambayo yameukzidi kimo ungumbaru wako.

Hujajua spelling unataka kujifaragua kutoa ushauri kwenye mambo tete ya kifalsafa?
 
Mkuu umeongea kitu mhimu Sana vijana wengi wanashindwa kutambua tupo nyakati gani na dunia inahitaji nini. Kipindi mwanamke anatolewa mahari wazee wetu wali mhesabu mwanamke kama zana ya kazi hivyo inatakiwa kuuzwa au kununuliwa ndio maana unyanyasaji wawanawake ulikua hauishi. Lakini now days dunia imefanya civilization kwamba mwanamke anahaki sawa na mwanaume hivyo Basi hamna kununua au kuuza mwanamke , tena kunawazazi bila aibu utaskia KESHO tunasherehe yakumuuza mwanangu[emoji26] au tunaenda kununua mke[emoji26] mim naamini vijana ndio wakuwabadili fikra wazee wetu ili kuendana namfumo wa dunia
Tatizo Waafrika wengi wanapenda kuishi kwa kukariri, ukiwaletea kitu kipya kinachoonesha mapungufu fulani katika jamii, kama kuonesha ubaya kama wa hii habari ya mahari, wengi watakupinga kwa kutumia logical fallacies za argument from tradition na argument from authority.

Ukiondoa hizo logical fallacies mbili, ambazo nazo ni fallacies tu, huna msingi wa kutetea mahari.
 
Katika Mila za Uislamu, mahari ni zawadi apewayo binti kama katika kutathmini na kuutambua mchango wake mkuu kwenye kujenga familia hapo baadae.
Mara nyingi binti anapokaribia kuolewa, basi hufundishwa mbinu mbalimbali za kujenga familia yenye kuleta tija kwenye jamii.

Mwanamke hatolewi mahari kufanywa mtumwa, wala hio mahari haihusiki kabisa na mzazi. Mahari ni yake binti kama ishara ya upendo kwake. Wajibu wa wazazi ni kuhakikisha tu ya kwamba binti yao anapatiwa mahari inayostahiki kwani bado hana uzoefu wa mambo ya ndoa na taratibu zake.

Wewe kama ulioa bila mahari ni sawa, hakuna ubaya katika hilo ila si utumwa na wala katu mwanamke hafanywi kuwa ni biashara kwani huo ni ujima na wala suala la mahari halikuwekwa katika mukusudio hayo.
Haki ya Talaka imetolewa kwa pande zote mbili pale zinapoona hakuna mstakabali wa pamoja ama unyanyasaji wa utu na hadhi yake.
Kadhia hii kiunaonyesha wazi kabisa kuwa mahari si zana ya kudunisha mwanamke kama unavyotaka kutuaminisha.
 
Mwanaume ni JASIRI.

BORN A HERO!

NI MUWINDAJI!

Hupaswi kuwa mtu mwororo!

You get to be tough and pay dowry!

Men are Naturally Donners.

Women are Naturally recipients!

That is Naturally and it is Nature!!

Mwanaume asiyelipa Mahari ni Dhaifu !!

Adam hakulipa Mahari
Nuhu hakulipa Mahari
Ibrahim hakulipa MAHARI
Hao ni wanaume ambao nafikiri majina yao ni makubwa kuliko wanaume wengi Duniani.

Lakini hata kama wangelipa Mahari bado isingemaanisha kuwa Mahari sio biashara ya Utumwa ya binadamu
 
Wewe kwanza jifunze spelling za hiyo lugha ujue tofauti ya donors na donners kabla ya kujifaragua kuwapa watu ushauri kwenye mambo ya kifalsafa ambayo yameukzidi kimo ungumbaru wako.

Hujajua spelling unataka kujifaragua kutoa ushauri kwenye mambo tete ya kifalsafa?
Icho ni kitu gani!?

Spelling?

Suala siyo Spelling ni Hoja!!

Lipa mahari!!
 
Icho ni kitu gani!?

Spelling?

Suala siyo Spelling ni Hoja!!

Lipa mahari!!
Nakwambia hivi, hujui spelling na hoja una vile vile.

Ukiondoa logical fallacy ya argument from tradition na nyingine ya argument from authority, na kujimwambafy kimfumodume tu kwamba mwanamme jasiri kama unaishi kwenye zama za ujima na za hunter gatherers, huna hoja.
 
Icho ni kitu gani!?

Spelling?

Suala siyo Spelling ni Hoja!!

Lipa mahari!!

Kwa nini unafikiri Mahari sio Biashara ya binadamu?
Embu wasikie hawa mabinti wa Labani(Wake wa Yakobo)

Mwanzo 31:14-15
[14]Raheli na Lea wakajibu, wakamwambia, Je! Imetubakia sehemu au urithi katika nyumba ya baba yetu?
And Rachel and Leah answered and said unto him, Is there yet any portion or inheritance for us in our father's house?

[15]Hakutufanya kama wageni, maana ametuuza, naye amekula fedha zetu kabisa?
Are we not counted of him strangers? for he hath sold us, and hath quite devoured also our money.
 
You have been brainwashed my brother, ila wewe unajiona umekuwa educated/wiser.

Unapinga mahari kwa kuita ujinga, lakini unasisitiza umuhimu wa sherehe na zawadi, kwanini kama wapenzi wamekubaliana wasiende tu wakaanze maisha yao? Huoni kama hata hiyo sherehe na zawadi ni ujinga na kupotezeana tu muda? If you start thinking in that line then you can see how vague is your argument.
Kijana nina imani thabiti unaijua na kuielewa elimu ya Mantiki vizuri.

Sitashangaa pia wakija kuuliza kwa nini watu wasikutane kisha wakazalishana halafu kila mmoja akashika njia yake ya kwenda. Maana ni kupotezeana muda na unyanyasaji kwa mwanamke kwani anakosa ile nafasi ya kujiachia na faragha yake binafsi.
 
Kama mlizoea kukeketwa na mliona ni Sawa, na sasa mnajiona mlikuwa hamnazo ndivyo miaka ijayo Watoto wenu watawaona mlikuwa hamnazo Kwa biashara za Mahari.
Ni Kwa vile akile zenu zipo nyuma hazioni yaliyombele.
Mnamacho lakini hamuoni Kwa sababu ya upofu uliopo vichwani mwenu.

Baadaye itajulikana Mimi na ninyi Nani alikuwa ni mpumbavu, mwongea pumba
Mjinga wa kiwango cha lami, unatumia nguvu nyiingi kuandika Pumba sijui huoni aibu
 
Sio kweli uongo
Mwanamke anakuja kwako anahitaji kula,navazi nk atakula mapenzi na kuvas Mapenzi

Familia zenye uwezo huhakiki kabisa unahojiwa hadi ukome kwanza utaukizwa wewe shughuli zako za kukuingixia kipato ni zipi hawaozi kwa mtu asiyeekeweka kipato chake cha kueleweka sio cha ohh siku moja moja mimi huwa naokota embe dodo chini ya mwembe

Msichana Material sasa hivi akubali kuvua nguo na kutaka kuishi na wewe burebure tu tu sio rahisi sababu wanajua fika wazazi wake hata wawe na pesa vipi akishaolewa hawataleta nyumbani hata robo kilo ya sukari mjinjue wenyewe huko

Usifikiri ukioa mtoto wa mwenye pesa ukishaoa wakwe wenye pesa iwatahangaika na wewe na mkeo mtajijua wenyewe huko
Wambie hao mkuu wanadhani kuoa mtt wa msusi ndo washatoboa,mtremko miamala kila kuisha wakilia shida..hawajui ukishaoa mzigo lako hilo kwa shida na raha lako hilo
 
Wao ndio wanajua kama mahari ni wao wanauzwa au la kama wanaume humunwNa dai mahari ni kugeuza mwanamke bidhaa na slave trade

Let women speak their position jwa hii ya vidume koko maskini ambavyo havitaki kulipa mahari kwa visingizio kibao kuwa ohh maharizimepitwa na wakati ohh ni slave trade ohh ni kama mwanamke anageuzwa kuw bidhaa sokoni kwa bride price nk kumbe vidume vyenyewe vilofa hela havina they free drive

Kutaka free drive ndio vinakuja na concepts za ku justify ulofa wao kibao
Hawana tofauti na wale wanapewa mahari na kaka zao na wazazi wao kwa kuchangishana waoe akati muoaji hana hata Kitanda cha kumlaza bi harusi wala hana kipato,mwanaume komaa tafuta hela hakuna mahari kubwa shua at teling' yu
 
MAHARI SIO LAZIMA, NI MILA POTOFU YA KUPIGWA VITA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Moja ya Mila potofu isiyo na maana ni suala la Mahari. Hakuna sababu hata Moja yenye Maana ya MTU kutoa Mahari ndipo akabidhiwe MKE au Mume. Ni ujinga tuu! Na jamii ambayo sio za kiungwana ndio hufanya desturi hizo.

Uliwahi kujiuliza Kwa nini unatoa/unatolewa Mahari?
Mahari inamaanisha nini kwenye mahusiano ya ndoa?
Mahari inaongeza au kupunguza nini kwenye mahusiano ya ndoa Mpya?

Utoaji wa Mahari ni Mila na desturi za kizamani zilizopitwa na Wakati. Zimepitwa na Wakati Kwa sababu hazina uhalisia wowote. Na zimelenga kufanya biashara ya kumuuza MTU(Mwanamke) kama Bidhaa Fulani hivi.

Ni marufuku mabinti wa Tibeli kutolewa Mahari. Marufuku! Mimi kama Baba Yao, nimetamka kuwa Binti zangu hawatatolewa Mahari Kamwe. Kwa sababu Watibeli hawatolewi Mahari wala hawatoi Mahari.

Mfumo dume wa kununua Wanawake Kwa kile kiitwacho Mahari umelenga kuwageuza Wanawake kama Bidhaa fulani, kwamba Mahari ya Binti huyu ni milioni 2 au tatu au Ng'ombe nne. Ndio nini sasa, upumbavu tuu!
Unajua haya mambo wamefanya Wazee wetu(tunawaheshimu) lakini lazima tukubali kuwa kuna mambo hayakuwa na maana yoyote Ile.

Matokeo yake wazazi walafi na wenye uroho WA fedha waliwauza mabinti zao Kwa wanaume wenye vipato bila kujali hisia za mabinti zao kama wanawapenda hao wanaume au Laah!

Watumwa ndio wanauzwa, Watu huru hawauzwi. Binti za Tibeli ni Watu Huru. Hawauzwi wala kujiuza. Binti aliyehuru au wazazi wenye Hekima kamwe hawawezi mgeuza Binti Yao mtumwa na kumuuza Kwa mwanaume mwingine Kwa Ile biashara yenye jina la Mahari. Hilo halitotokea.
Binti huru anahaki zote za kuchagua Mume ampendaye, akaolewa na kuanzisha mji wake Kwa Moyo WA mapenzi. Na sio Aolewe Kwa Pesa ili baadaye Huko ndoani kitu kidogo tuu nilikutolea Mahari. Kitu kidogo tuu haukunitolea Mahari. Come on!

Ni jamii ya Watu wajinga wenye Akili za gizani wanaolipishana Mahari. Ujingaujinga tuu!
Yaani wazee wazima mnakaa mnajadili na ku-bargain kiasi cha Pesa za Binti yenu. Huo ni ujinga wa kiwango cha juu Kabisa. Alafu mwishowe ati mmoja anakuwa na deni kisa ameshindwa kumaliza.

Sijui mwingine anatolewa Mahari ya laki mbili, mwingine elfu 80, mwingine milioni tano mwingine milioni kumi. Yaani kama Watu waliochanganyikiwa. Hivi kweli Baba mwenye Akili kabisa unayempenda Binti yako unakubali kabisa kujadili thamani ya Binti yako na Pesa. Wanaume tuweni serious kidogo. Tuache mambo ya kijingajinga.

Binti amepata Mchumba, anayoruhusa ya kuja nyumbani kumtambulisha, kisha taratibu za sherehe za kumuaga Binti zianze huku upande wa pili wa Bwana harusi wakiandaa sherehe ya kumpokea Bibi Harusi. Sio lazima iwe sherehe kubwa Ila ni muhimu kufanyika kulingana na kipato chenu.

Kwa Vijana WA Zama hizi mambo yasiyo na maana yoyote yatazidisha mitafaruku isiyo na maana. Ndio maana Wazungu wao walishaachanaga na mambo ya Mahari miaka mingi iliyopita.

Mwanaume unapoenda kuoa sehemu au kwenda ukweni ni lazima uwe na Zawadi kadiri ya uwezo wako. Sio unaenda mikono mitupu kama mjinga. Halikadhalika na Mwanamke uendapo ukweni lazima uende na Zawadi. Hiyo Zawadi haitahesabika kama Mahari. Kumaanisha Hautapangiwa na yeyote Ila utaifanya Kwa mapenzi na uwezo wako WA Wakati huo.
Hivyo ndivyo Watibeli tunavyoendesha mambo yetu.

Nimemaliza! Mwenye swali aweza kuuliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Sijasoma mpaka mwisho lakini una hoja naomba usikilizwe.
 
Kwani mahari nini?tambua kuna mahari na mali watu uchanganya mambo haya,wewe umekusudia nn?
 
Back
Top Bottom