Mahari sio lazima, ni mila potofu ya kupingwa

Mahari sio lazima, ni mila potofu ya kupingwa

Kwa utamu ule wa mbususu nalipa mahari kwa moyo mmoja alimradi mbususu ipo
 
Hii ni ELIMU juu ya Mtu Mume na Mtu Mke.

Mtu Mke ni Zawadi kwa Mtu Mume tangu siku ya Kwanza.

Mwanaume asiyemchukulia Mwanamke kama Kitu cha Zawadi bado hajajua kwa nini anamuhitaji Mwanamke.

Mahari ni ishara ya ku appreciate Zawadi unayotarajia kupewa na wazazi husika!

Binti hutunzwa na wazazi tangu akiwa Mdogo akifundishwa kwamba atakuwa mtu wa Mtu Siku moja...

Atatolewa kuwa Mtu wa Mtu Mume siku moja!

Hiyo tu kwa mwanamume ni wake up call kwamba ameandaliwa mtu wa kuishi naye...ampende na Kumtunza kwa usitawi wa familia anayotarajia kuianza!

Kwanza kwa tamaduni za Kiafrika ndo na watoto wote wanatajwa kwa jina la Mwanamume..!Bado tu huoni Sababu ya kulipa Mahari?

Mahari yako kwenye jamii zote!!

Usijidanganye
Mwanamume shurti ujiandae kumpata Mke kwa kuonesha Ishara ya UPENDO na KUTHAMINI MATUNZO YA MKEWE MTARAJIWA KUTOKA KWA WAZAZI WAKE.

Aliyekuambia Kijana wakiume hajatunzwa na kuandaliwa na Wazazi wake ni Nani?
Aliyekuambia Kijana WA kiume haandaliwi na kufunzwa Kwa ajili ya maandalizi ya kuanzisha familia ni Nani?
Aliyekuambia Mahari ni ishara ya upendo ni Nani?

Kwa nini mnawachukulia Wanawake kama Mali ya MTU mwingine? Ni Nani aliyewaambia na kuwadanganya kuwa Mtu akiolewa anamilikiwa na MTU mwingine?

Unaposema Mahari Ipo kwenye jamii zote unauhakika? Labda useme zamani Sana, Kwa sababu za Akili za kizamani, Zama za Giza kulipokuwa na biashara ya Utumwa, ambapo pia Mwanamke hakuchukuliwa kama MTU. Na wengi walikuwa Watumwa.
Nenda nchi za Ulaya alafu uwaambie hizo habari za Mahari usikie watasema nini?

Mahari ni biashara ya kuuza na kununua binadamu
 
Kama umezaliwa na single mother, mahari ni kitu kibaya sana. Kama unaoa vyangudoa kama wale kutoka karibu na mlima mrefu sana Afrika, basi una hoja. Ila kama unaoa mke mke kweli mahari ni tunu

Iwe amezaliwa na changudoa, Single mother, au Mwanamke Bikra. Mahari ni biashara ya kununua Watu wasio huru. Watumwa.
Ungempa sababu kuu mbili za Kwa nini kuna biashara ya Mahari ili Watu wajifunze na sio kuleta hoja kama za Watu wajinga
 
Ee Mungu tunusuru watoto wa kiume wengi kugeuka mashoga na kutwa kuongelea mambo ya wanawakr likiwemo hili la mahari badala ya kuwaachia wanawake wenyewe ndio waseme mahari wanaionaje
Aaah hapa umezingua sasa, ushoga unaingiaje hapo...? Njoo na hoja za msingi kwanini mahari ilipwe au isilipwe
 
Mkuu umeongea kitu mhimu Sana vijana wengi wanashindwa kutambua tupo nyakati gani na dunia inahitaji nini. Kipindi mwanamke anatolewa mahari wazee wetu wali mhesabu mwanamke kama zana ya kazi hivyo inatakiwa kuuzwa au kununuliwa ndio maana unyanyasaji wawanawake ulikua hauishi. Lakini now days dunia imefanya civilization kwamba mwanamke anahaki sawa na mwanaume hivyo Basi hamna kununua au kuuza mwanamke , tena kunawazazi bila aibu utaskia KESHO tunasherehe yakumuuza mwanangu[emoji26] au tunaenda kununua mke[emoji26] mim naamini vijana ndio wakuwabadili fikra wazee wetu ili kuendana namfumo wa dunia
 

Nyerere describes bride price as evil in posthumous bio.

Akili ndogo haiwezi kuelewa somo linalotaka akili kubwa.
Hahah nilijua lazima uunge mkono.

Lipa mahari mkuu acheni janja janja.

Sio kila Jambo lazima ufanye with reason.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaongea Pumba as usual!

Kama mlizoea kukeketwa na mliona ni Sawa, na sasa mnajiona mlikuwa hamnazo ndivyo miaka ijayo Watoto wenu watawaona mlikuwa hamnazo Kwa biashara za Mahari.
Ni Kwa vile akile zenu zipo nyuma hazioni yaliyombele.
Mnamacho lakini hamuoni Kwa sababu ya upofu uliopo vichwani mwenu.

Baadaye itajulikana Mimi na ninyi Nani alikuwa ni mpumbavu, mwongea pumba
 
Hongereni

Wala sio Jambo la kupewa hongera, ni kama useme Watoto wetu hawakeketwi. Hapo hakuna haja ya Hongera.
Watibeli tunachoangalia ni Mantiki ya kila desturi, Mila na utamaduni pamoja na sheria za Dini.
Jambo lolote ambalo halina mantiki kwetu sio lazima/ no hiyari ya MTU kufanya au asifanye.

Ila kumuuza Mwanamke/mwanaume Kwa kile kiitwacho Mahari. Kwetu Hilo haliwezekaniki.
 
Hahah nilijua lazima uunge mkono.

Lipa mahari mkuu acheni janja janja.

Sio kila Jambo lazima ufanye with reason.

Sent using Jamii Forums mobile app

Janja janja ni nini?

Mimi nikienda dinner na shopping ya weekend moja tu ni mahari tayari, na ninafanya hivyo regularly, kila mwezi haikosi mara mbili, bado unataka nilipe mahari?

Unajua ukisema "si kila jambo lazima ufanye with reason" ushatumia reason hata hapo?

Na kama kweli si kila jambo lazima ufanye with reason, huoni kwamba wewe kupinga wanaopinga kulipa mahari kwa reason zako ni kupinga kauli yako mwenyewe ya "si kila jambo lazima ufanye with reason"?

Kabla hujanishauri mimi, wewe mwenyewe unaelewa unachotaka? Kauli zako zinajipinga zenyewe kwa namna ambayo siwezi kuufuata ushauri wako, hata kama ningetaka kufanya hivyo.

Nilipe mahari au nikubali kwamba si kila jambo lazima nifanye with reason, falsafa ambayo inanuruhusu nisilipe mahari?

Unaelewa kwamba unaji contradict mwenyewe?
 
Wala sio Jambo la kupewa hongera, ni kama useme Watoto wetu hawakeketwi. Hapo hakuna haja ya Hongera.
Watibeli tunachoangalia ni Mantiki ya kila desturi, Mila na utamaduni pamoja na sheria za Dini.
Jambo lolote ambalo halina mantiki kwetu sio lazima/ no hiyari ya MTU kufanya au asifanye.

Ila kumuuza Mwanamke/mwanaume Kwa kile kiitwacho Mahari. Kwetu Hilo haliwezekaniki.
Waafrika wengi wamewauza hata ndugu zao wanaume kwenye utumwa. Miaka 150 tu iliyopita.

Hivyo, kwenye hili la kuuza watu ili wapate pesa unaweza kubishana nao sana wasikuelewe. Kwa makusudi.

Wana uwezo mkubwa sana wa ku justify biashara ya kuuza watu kwa kutumia logical fallacies kama argument from tradition na argument from authority.

Pesa inatawala, hayo mambo ya mantiki na principle hawaelewi.

Maisha yanaenda kichawichawi na kwa michezo ya pata potea sana, watu wana njaa.

Ukileta habari za principle na mantiki, wanaona unawazingua tu.

Usipolipa mahari utajua kwa nini Mbaraka Mwinshehe aliimba Wajomba Wamechacha.

RIP Mbaraka Mwinshehe, one of the best yet.

 
You have been brainwashed my brother, ila wewe unajiona umekuwa educated/wiser.

Unapinga mahari kwa kuita ujinga, lakini unasisitiza umuhimu wa sherehe na zawadi, kwanini kama wapenzi wamekubaliana wasiende tu wakaanze maisha yao? Huoni kama hata hiyo sherehe na zawadi ni ujinga na kupotezeana tu muda? If you start thinking in that line then you can see how vague is your argument.
 
You have been brainwashed my brother, ila wewe unajiona umekuwa educated/wiser.

Unapinga mahari kwa kuita ujinga, lakini unasisitiza umuhimu wa sherehe na zawadi, kwanini kama wapenzi wamekubaliana wasiende tu wakaanze maisha yao? Huoni kama hata hiyo sherehe na zawadi ni ujinga na kupotezeana tu muda? If you start thinking in that line then you can see how vague is your argument.

Sherehe sio lazima
Zawadi sio lazima
Mahari sio LAZIMA.

Kwenye ndoa cha lazima ni Upendo. Upendo ndio ndoa.

Kwa hiyo kuwa brainwashed ni kukataa baadhi ya mambo yanayodhalilisha jamii? Mfano kupinga ukeketaji ni kuwa brainwashed?
 
Back
Top Bottom