Ukitaka kuoa binti wa kiislam wa unguja, wa maisha ya uchumi wa kati chini. Mara nyingi utaambiwa utoe mahari ya kitanda, kabati na dressing table. Na hivo vitu utavotoa kumpa mke ni kwamba vinakuja nyumbani kwako tena kutumika na wewe mke na watoto wenu.
Kwamba lengo ni kuhakikisha hiyo familia tarajiwa inaishi maisha ya staha.
Kwa mimi hii kwangu haina shida kbs!
Kuna mila ambazo zinatoa n'gombe kama mahari na mke akishindwa maisha huko kwa mumewe basi inabidi warudishe ng'ombe za watu, hii ni biashara ya utumwa kbs!
Pia kuna wale wazee wanaopanga wao mahari ya binti yao bila kumshirikisha binti na hata hawajali anaenda ishije huko, kimsingi wamemuuza kwq bei waliotaka.
Binafsi mahari halali ni ile itakayolenga kusaidia maisha ya familia mpya mke na mume.
Mimi ni mtibeli nikikutana na mwanamke wa tibeli niko tayari kufunga nae ndoa ya heshima" sio hawa wanaouzwa mtu akifika bei hawana hiari!