Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
- Thread starter
- #81
Umeeleweka vyema kabisa mkuu.
Karibu Kwa mjadala
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umeeleweka vyema kabisa mkuu.
Ahsante,tuko pamoja mkuu.Karibu Kwa mjadala
MAHARI SIO LAZIMA, NI MILA POTOFU YA KUPIGWA VITA.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Moja ya Mila potofu isiyo na maana ni suala la Mahari. Hakuna sababu hata Moja yenye Maana ya MTU kutoa Mahari ndipo akabidhiwe MKE au Mume. Ni ujinga tuu! Na jamii ambayo sio za kiungwana ndio hufanya desturi hizo.
Uliwahi kujiuliza Kwa nini unatoa/unatolewa Mahari?
Mahari inamaanisha nini kwenye mahusiano ya ndoa?
Mahari inaongeza au kupunguza nini kwenye mahusiano ya ndoa Mpya?
Utoaji wa Mahari ni Mila na desturi za kizamani zilizopitwa na Wakati. Zimepitwa na Wakati Kwa sababu hazina uhalisia wowote. Na zimelenga kufanya biashara ya kumuuza MTU(Mwanamke) kama Bidhaa Fulani hivi.
Ni marufuku mabinti wa Tibeli kutolewa Mahari. Marufuku! Mimi kama Baba Yao, nimetamka kuwa Binti zangu hawatatolewa Mahari Kamwe. Kwa sababu Watibeli hawatolewi Mahari wala hawatoi Mahari.
Mfumo dume wa kununua Wanawake Kwa kile kiitwacho Mahari umelenga kuwageuza Wanawake kama Bidhaa fulani, kwamba Mahari ya Binti huyu ni milioni 2 au tatu au Ng'ombe nne. Ndio nini sasa, upumbavu tuu!
Unajua haya mambo wamefanya Wazee wetu(tunawaheshimu) lakini lazima tukubali kuwa kuna mambo hayakuwa na maana yoyote Ile.
Matokeo yake wazazi walafi na wenye uroho WA fedha waliwauza mabinti zao Kwa wanaume wenye vipato bila kujali hisia za mabinti zao kama wanawapenda hao wanaume au Laah!
Watumwa ndio wanauzwa, Watu huru hawauzwi. Binti za Tibeli ni Watu Huru. Hawauzwi wala kujiuza. Binti aliyehuru au wazazi wenye Hekima kamwe hawawezi mgeuza Binti Yao mtumwa na kumuuza Kwa mwanaume mwingine Kwa Ile biashara yenye jina la Mahari. Hilo halitotokea.
Binti huru anahaki zote za kuchagua Mume ampendaye, akaolewa na kuanzisha mji wake Kwa Moyo WA mapenzi. Na sio Aolewe Kwa Pesa ili baadaye Huko ndoani kitu kidogo tuu nilikutolea Mahari. Kitu kidogo tuu haukunitolea Mahari. Come on!
Ni jamii ya Watu wajinga wenye Akili za gizani wanaolipishana Mahari. Ujingaujinga tuu!
Yaani wazee wazima mnakaa mnajadili na ku-bargain kiasi cha Pesa za Binti yenu. Huo ni ujinga wa kiwango cha juu Kabisa. Alafu mwishowe ati mmoja anakuwa na deni kisa ameshindwa kumaliza.
Sijui mwingine anatolewa Mahari ya laki mbili, mwingine elfu 80, mwingine milioni tano mwingine milioni kumi. Yaani kama Watu waliochanganyikiwa. Hivi kweli Baba mwenye Akili kabisa unayempenda Binti yako unakubali kabisa kujadili thamani ya Binti yako na Pesa. Wanaume tuweni serious kidogo. Tuache mambo ya kijingajinga.
Binti amepata Mchumba, anayoruhusa ya kuja nyumbani kumtambulisha, kisha taratibu za sherehe za kumuaga Binti zianze huku upande wa pili wa Bwana harusi wakiandaa sherehe ya kumpokea Bibi Harusi. Sio lazima iwe sherehe kubwa Ila ni muhimu kufanyika kulingana na kipato chenu.
Kwa Vijana WA Zama hizi mambo yasiyo na maana yoyote yatazidisha mitafaruku isiyo na maana. Ndio maana Wazungu wao walishaachanaga na mambo ya Mahari miaka mingi iliyopita.
Mwanaume unapoenda kuoa sehemu au kwenda ukweni ni lazima uwe na Zawadi kadiri ya uwezo wako. Sio unaenda mikono mitupu kama mjinga. Halikadhalika na Mwanamke uendapo ukweni lazima uende na Zawadi. Hiyo Zawadi haitahesabika kama Mahari. Kumaanisha Hautapangiwa na yeyote Ila utaifanya Kwa mapenzi na uwezo wako WA Wakati huo.
Hivyo ndivyo Watibeli tunavyoendesha mambo yetu.
Nimemaliza! Mwenye swali aweza kuuliza.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Sidhani kama mwanamke ana bei ambayo waweza mnunua, ni kama shukrani tu, na asante kwa Mzazi kumlea.
Hata kwa Mungu mambo yakifanikiwa huwa tunatoa shukran, sasa sijui tunanunua nini kwa Mungu?
Mtu kamlea mwanaye, Kamsomesha mpaka kafika chuo, na ajira labda kapata, kuna shida gani kushukuru?
Na mahari sio lazima, kataa kulipa, utamchukua tu mkeo, watu wakipendana hakuna wa kuwakataza.
Lakini mimi nakataa kwamba magari ni mila mbovu na ya zamani isiyofaa, lazima tuseme asante.
Mahari siyo "mahali".Kijana ashauri mahali kukatwa Kodi.
Kwani huyo mzazi wa mwanaume naye si kamsomesha pia mwanae??Nae anahitaji shukraniSidhani kama mwanamke ana bei ambayo waweza mnunua, ni kama shukrani tu, na asante kwa Mzazi kumlea.
Hata kwa Mungu mambo yakifanikiwa huwa tunatoa shukran, sasa sijui tunanunua nini kwa Mungu?
Mtu kamlea mwanaye, Kamsomesha mpaka kafika chuo, na ajira labda kapata, kuna shida gani kushukuru?
Na mahari sio lazima, kataa kulipa, utamchukua tu mkeo, watu wakipendana hakuna wa kuwakataza.
Lakini mimi nakataa kwamba magari ni mila mbovu na ya zamani isiyofaa, lazima tuseme asante.
Ulishawahi kupeleka posa sehemu ukaambiwa hivyo? Au unaota tu?Unakuta unaambiwa mahari mil.5 usipotoa hatukuozi mwanetu....
mimi ilinitokeaUlishawahi kupeleka posa sehemu ukaambiwa hivyo? Au unaota tu?
Ilikutokea vipi, kwa imani ipi? fafanuwa.mimi ilinitokea
Mimi hata wakitaka 50k siwapi, hawataki wachukue mtoto wao, mama Sasha mwenyewe sasa kipindi nimepewa kima akanambia achana nao wanafikiri hela zinaokotwa kafanyie mambo mengine hela zako
Watibeli mnapatikana wapi? Maana mnaeza kuwa msaada wetu hapo mbeleni kwa suala hilo
Hili swala la mahari tumeliona toka kwenye historia ya zamani. Mfano kwenye Biblia hili swala lipo. Unaweza jiuliza Biblia ina mda gani toka iwepo na swala hili lina maana gani. .
Tatizo lako la kutafsiri ni potovu ndio maana unalitafsiri kwa uelewa mdogo. Kama ungetambua mahari lina maana gani na kwa nini inalipwa basi usingesema una logic kubwa. Kwako wewe mahari ni kumnunua mwanamke🤣 kama ni kumnunua hata mimi napinga ila nakupa kazi nenda katafute mahari maana yake ni nini? ukishindwa njoo nikufafanulie. .
Have a blessed day...
Hilo kabila linapatikana wapi aisee, kumbe hakuna mahari kwanza hizo PISI NI WAKALI au ndo wanazidiwa na vinyago vya kariakoo vile vya nguoWatibeli hatutoi Mahari wala Binti zetu hawatolewi Mahari.
Unafahamu maana ya shukrani??Sidhani kama mwanamke ana bei ambayo waweza mnunua, ni kama shukrani tu, na asante kwa Mzazi kumlea.
Hata kwa Mungu mambo yakifanikiwa huwa tunatoa shukran, sasa sijui tunanunua nini kwa Mungu?
Mtu kamlea mwanaye, Kamsomesha mpaka kafika chuo, na ajira labda kapata, kuna shida gani kushukuru?
Na mahari sio lazima, kataa kulipa, utamchukua tu mkeo, watu wakipendana hakuna wa kuwakataza.
Lakini mimi nakataa kwamba magari ni mila mbovu na ya zamani isiyofaa, lazima tuseme asante.
Hilo kabila linapatikana wapi aisee, kumbe hakuna mahari kwanza hizo PISI NI WAKALI au ndo wanazidiwa na vinyago vya kariakoo vile vya nguo