MAHARI SIO LAZIMA, NI MILA POTOFU YA KUPIGWA VITA.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Moja ya Mila potofu isiyo na maana ni suala la Mahari. Hakuna sababu hata Moja yenye Maana ya MTU kutoa Mahari ndipo akabidhiwe MKE au Mume. Ni ujinga tuu! Na jamii ambayo sio za kiungwana ndio hufanya desturi hizo.
Uliwahi kujiuliza Kwa nini unatoa/unatolewa Mahari?
Mahari inamaanisha nini kwenye mahusiano ya ndoa?
Mahari inaongeza au kupunguza nini kwenye mahusiano ya ndoa Mpya?
Utoaji wa Mahari ni Mila na desturi za kizamani zilizopitwa na Wakati. Zimepitwa na Wakati Kwa sababu hazina uhalisia wowote. Na zimelenga kufanya biashara ya kumuuza MTU(Mwanamke) kama Bidhaa Fulani hivi.
Ni marufuku mabinti wa Tibeli kutolewa Mahari. Marufuku! Mimi kama Baba Yao, nimetamka kuwa Binti zangu hawatatolewa Mahari Kamwe. Kwa sababu Watibeli hawatolewi Mahari wala hawatoi Mahari.
Mfumo dume wa kununua Wanawake Kwa kile kiitwacho Mahari umelenga kuwageuza Wanawake kama Bidhaa fulani, kwamba Mahari ya Binti huyu ni milioni 2 au tatu au Ng'ombe nne. Ndio nini sasa, upumbavu tuu!
Unajua haya mambo wamefanya Wazee wetu(tunawaheshimu) lakini lazima tukubali kuwa kuna mambo hayakuwa na maana yoyote Ile.
Matokeo yake wazazi walafi na wenye uroho WA fedha waliwauza mabinti zao Kwa wanaume wenye vipato bila kujali hisia za mabinti zao kama wanawapenda hao wanaume au Laah!
Watumwa ndio wanauzwa, Watu huru hawauzwi. Binti za Tibeli ni Watu Huru. Hawauzwi wala kujiuza. Binti aliyehuru au wazazi wenye Hekima kamwe hawawezi mgeuza Binti Yao mtumwa na kumuuza Kwa mwanaume mwingine Kwa Ile biashara yenye jina la Mahari. Hilo halitotokea.
Binti huru anahaki zote za kuchagua Mume ampendaye, akaolewa na kuanzisha mji wake Kwa Moyo WA mapenzi. Na sio Aolewe Kwa Pesa ili baadaye Huko ndoani kitu kidogo tuu nilikutolea Mahari. Kitu kidogo tuu haukunitolea Mahari. Come on!
Ni jamii ya Watu wajinga wenye Akili za gizani wanaolipishana Mahari. Ujingaujinga tuu!
Yaani wazee wazima mnakaa mnajadili na ku-bargain kiasi cha Pesa za Binti yenu. Huo ni ujinga wa kiwango cha juu Kabisa. Alafu mwishowe ati mmoja anakuwa na deni kisa ameshindwa kumaliza.
Sijui mwingine anatolewa Mahari ya laki mbili, mwingine elfu 80, mwingine milioni tano mwingine milioni kumi. Yaani kama Watu waliochanganyikiwa. Hivi kweli Baba mwenye Akili kabisa unayempenda Binti yako unakubali kabisa kujadili thamani ya Binti yako na Pesa. Wanaume tuweni serious kidogo. Tuache mambo ya kijingajinga.
Binti amepata Mchumba, anayoruhusa ya kuja nyumbani kumtambulisha, kisha taratibu za sherehe za kumuaga Binti zianze huku upande wa pili wa Bwana harusi wakiandaa sherehe ya kumpokea Bibi Harusi. Sio lazima iwe sherehe kubwa Ila ni muhimu kufanyika kulingana na kipato chenu.
Kwa Vijana WA Zama hizi mambo yasiyo na maana yoyote yatazidisha mitafaruku isiyo na maana. Ndio maana Wazungu wao walishaachanaga na mambo ya Mahari miaka mingi iliyopita.
Mwanaume unapoenda kuoa sehemu au kwenda ukweni ni lazima uwe na Zawadi kadiri ya uwezo wako. Sio unaenda mikono mitupu kama mjinga. Halikadhalika na Mwanamke uendapo ukweni lazima uende na Zawadi. Hiyo Zawadi haitahesabika kama Mahari. Kumaanisha Hautapangiwa na yeyote Ila utaifanya Kwa mapenzi na uwezo wako WA Wakati huo.
Hivyo ndivyo Watibeli tunavyoendesha mambo yetu.
Nimemaliza! Mwenye swali aweza kuuliza.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Umeiongelea mahari, sifahamu kwa imani, mila, desturi au utamaduni upi.
Nikaona tukupe darsa dogo la kuifahamu mahari Kiislaam:
Kwanza kabisa ningependa tufahamu kuwa tunaposikia neno "mahari" kwa mila, desturi au imani nyingine yoyote nje ya Uislam wanakuwa wameliazima neno hilo kutoka Kiarabu linalotokana na sharia ya ndoa ya Kiislaam.
Mkataba wa ndoa ya Kiislamu
-Maher (iliyotafsiriwa kama mahari) ni mkataba ambao Waislam huingia kabla ya kufunga ndoa. Hairejelei kwenye mkataba wa ndoa yenyewe, bali mahari ni mkataba ambao mume atalipa kwa mkewe katika tukio la talaka au kifo ikiwa haijatimizwa wakati wa mkataba wa ndoa.
Katika sharia za Kiislam, Mahari ni zawadi au mchango unaotolewa na mume mtarajiwa kwa mke wake mtarajiwa, kwa mali waliyokubaliana, kama ishara ya heshima kwa bi-harusi, na pia inakuwa ni utambuzi wa uhuru wake kutoka kwa wazazi au walezi wake.
Mahari si zawadi kwa njia ya kitamaduni, lakini kwa hakika ni lazima na mke mtarajiwa huipokea kama haki yake.
Mahari inaweza kuwa pesa taslim, au aina yoyote ya mali iliyotolewa kabla ya ndoa au kugawanywa katika malipo ya mapema na yaliyoahirishwa (kopwa). Kiasi na muda wa malipo utategemea mambo ya kimila (kumbuka, mila na desturi za Waislam ni zile zisizokiuka Uislam) chini ya sharia ya Kiislam.
Ikitokea malipo ya mahari yameahirishwa (cheleweshwa au kopwa), sehemu iliyoahirishwa ina athari ya kumtunza mke baada ya talaka au baada ya kifo cha mumewe. Ingawa mke anaweza kusamehe malipo ya Mahari, anastahiki hilo kama suala la kanuni za dini ya Kiislam.
Kila Mahari itafsiriwa kwa masharti yake na kwa kuzingatia nia ya wahusika wakati mkataba ulipofanywa.
Ingawa sharia sheria ya nchi ni lazima iwe kwa maandishi yaliyotiwa saini na pande zote mbili na kushuhudiwa.
Makubaliano ya Mahari Kiislaam yanatambuliwa kuwa ni halali kisheria nchini Tanzania na nchi nyingi Ulimwenguni.
Ndoa ya Kiislam haitimii bila makubaliano ya mahari kwa pande mbili.
Nimejitahidi kuielezea Mahari Kiislaam kwa uchache wake, kama kuna makosa yoyote katika hayo basi ni yangu binafsi. Allah ndiye mjuzi zaidi.