MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,775
- 71,893
Mwaka 2001 baada ya Dhalimu Mkapa kufanya ukatili wa kutisha dhidi ya nchi ya Zanzibar alichomoka kupitia MUAFAKA I.
Mwaka 2001 ilikuwa ni rahisi kuficha maovu na ukatili nchini Zanzibari kwasababu teknolojia ilikuwa haijakomaa hivyo watu wengi hawakufahamu kinachoendelea.
Mwaka 2025 baada ya Samia na Jakaya kutekeleza mauaji ya maelfu ya watanganyika nao wanataka kutumia kitabu kilekile cha Dhalimu Mkapa kutaka kuchomoka kupitia MARIDHIANO.
Mwaka 2001 Mkapa aligombana na wasimamizi wa uchaguzi kutoka nje ambao walitoa ushauri kuhusu michezo michafu. Mwaka 2025 Samia amegombana na wasimamizi wa uchaguzi kutoka nje waliotoa ushauri kuhusu michezo michafu na akawasuta kwa hotuba ileile ambayo Mkapa aliitumia mwaka 2001.
Ili kupata taswira ya haraka juu ya utofauti wa Zanzibar 2001 na Tanganyika 2025 tuangalie haya machache kwa haraka:
MOSI, Zanzibar 2001 walau uchaguzi ulifanyika na kura zikapinduliwa kihuni. Tanganyika 2025 uchaguzi haukufanyika lakini mgombea akashinda kwa kishindo cha asilimia 97%.
PILI, Zanzibar 2001 vurugu zilifanywa na wananchi kwa kuchochewa na wanasiasa wenye mlengo mkali, hivyo ilikuwa ni rahisi kufanya MUAFAKA kwasababu wanasiasa wakipata wanachotaka basi watu wao hutulia. Tanganyika 2025 maandamano na vurugu zote ziliratibiwa na wananchi wadogo a.k.a Gen-Z ambao hawakuwakilishwa na chama chochote cha siasa, hivyo hata ufanya MARIDHIANO na CHADEMA nao wataingia kwenye orodha ya wasaliti kama ACT-Wazelendo.
TATU, Zanzibar 2001 madhara yalikuwa ni makubwa mno kutokana pia na udogo wake kama nchi. Ila Tanganyika 2025 madhara ya vifo vya raia ni makubwa mno kuliko kule Zanzibar, na hili limechangiwa na ukubwa wa Tanganyika na watu wengi mno kushiriki maandamano.
NNE, Zanzibar 2001 vurugu zilikuwa sehemu na sehemu, hasahasa PEMBA. Nchi ilikuwa imegawanyika na baadhi ya wazanzibari ambao wanawachukia wapemba kwa kuwaita MACHOTARA walishiriki kwenye udhalimu mkubwa dhidi ya ndugu zao. Tanganyika 2025 vurugu zilitokea maeneo yote ya nchi hadi vijijini, na watanganyika asilimia kubwa walikuwa kitu kimoja bila tofauti za DINI, ITIKADI, SIASA, RANGI au KABILA.
Kilichofanyika jana 14/11/2025 baada ya matamko ya BAKWATA ni mbinu zilezile za JAKAYA KIKWETE za kupenda kutumia karata ya UDINI kuwagawanya Wakristo na Waislamu ambayo aliitumia tena mwaka 2010 kwenye uchaguzi mkuu akishirikiana na Prof. Ibrahimu Lipumba na Masheikh wa BAKWATA. Hii mbinu haitafanikiwa kwasababu, huku mtaani BAKWATA haiaminiki na haipendwi kabisa na Waislamu ambao wengi wao ni wahanga wa dhulma za CCM tokea awamu ya kwanza.
TANO, Zanzibar 2001 wanasiasa wake ambao ndiyo chanzo kikubwa cha maandamano walikuwa radhi kupata MUAFAKA na walipopata nafasi za kisiasa basi wafuasi wao wakatulia. Tanganyika maandamano hayakuwa ya wanasiasa hivyo MARIDHIANO ni jambo lisiloweza kuzaa matunda kabisa hata kama CHADEMA itakubali.
SITA, Zanzibar 2001 wanasiasa wote, Sheikh Karume na Maalim Seif pamoja na wafuasi wao walikuwa ni Waislamu. Kiasilia Zanzibar ni nchi ya kiislamu tokea karne na karne, leo hii raia wake zaidi ya asilimia 98% ni Waislamu. Hivyo mbali na kugawanyika kwenye RANGI, ila DINI ilikuwa ni jambo linalowaunganisha (A Unifying Factor).
Tanganyika 2025 ni tofauti, ukitoa UTANZANIA watu wa DINI na MAKABILA yao, japo hivi siyo vya msingi sana kwa raia wa kawaida, karata ya JAKAYA KIKWETE kuwatumia BAKWATA itawasaidia kwa muda tu, lakini ukweli ni kwamba BAKWATA hawana nguvu kubwa hivyo ya ushawishi hata dhidi ya Waislamu wenzao.
Sipendi kusema hili, lakini LISSU ni MKATOLIKI na HECHE naambiwa ni MSABATO (taarifa za marekebisho). Kanisa Katoliki ushawishi wake juu ya washirika wake ni mkubwa mno tofauti kabisa na BAKWATA, KKKT, au TAG. Hichi walichokisema BAKWATA leo hii kitaigharimu mno CCM na siku TEC watakapotoa WARAKA wao ambao kipindi hiki uko kwenye kuandaliwa serikali itatikisika mno na nchi itazidi kupasuka vipande.
SABA, Zanzibar 2001 CCM walipona kwasababu teknolojia haikuwa kubwa ya kuweza kufahamisha dunia kinachoendelea. Tanganyika 2025 karibia kila raia anazo video na picha za vitendo vya kutisha ambazo zitadumu vizazi na vizazi vikizidi kuleta hasira, doa na kuligawanya zaidi taifa.
NANE, Zanzibar 2001 lilikuwa ni janga la kitaifa (A National Crisis) na CCM pamoja na taasisi zake walifanikiwa kulidogosha na kuihadaa dunia. Bahati mbaya sana Tanganyika 2025 kutokana na teknolojia, limekuwa ni janga la kibinadamu (A Humanitarian Crisis) ambalo halimilikiwa tena na Tanganyika bali dunia nzima. Majirani wa Afrika wamelivalia njuga, Wazungu nao wamelivalia njuga, na kadiri siku zinavyoenda ndiyo bomu kubwa litalipuka.
Suala likishatoka kuwa Janga la Kitaifa (A National Crisis) hadi kuwa Janga la Kibinadamu (A Humanitarian Crisis) basi fahamu fika huwezi kulitatua kwa kutumia mbinu za siasa za ndani, huwa Jumuiya nzima ya Kimataifa (The International Community) inajiingiza hata kimabavu. Binafsi sidhani kama CCM ina msuli mkubwa kama Israeli, Urusi, Korea Kaskazini au Marekani kuweza kupambana na The International Community.
Mnaweza mkajiaminisha kwamba mbona hawa mabeberu tunakula nao na kulinda maslahi yao, lakini kama hata wao wenyewe wanageukana ninyi waafrika mnadhani hamtageukwa kweli ??? Kenya ni mshirika na muumini wao mzuri lakini walimshughulikia ipasavyo. Hata Makaburu waligeukwa na mabeberu wenzao. These are hard lessons.
================================================================
LEO HII NI HAYA TU.....