PostGE2025 Mahesabu Mabovu: Utofauti kati ya mauaji ya Tanganyika 2025 na Zanzibar 2001

PostGE2025 Mahesabu Mabovu: Utofauti kati ya mauaji ya Tanganyika 2025 na Zanzibar 2001

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Sawa Malcom.... Je machafuko haya kuna mkono wa International agents? Nahisi kama kuna wageni wameingiza sera zao ili wanufaike nashindwa kuamini kama ni maamuzi ya Watanzania dhidi ya watanzania wenzao

Napata wasi wasi na hawa wawekwzaji wa hivi karibuni
Kwa hiyo Agents walioigiza mkono wao ndo walikua wanateka wakina madude, polepole, Ali kibao punguzeni ujinga kwenye vichwa vyenu
 
Tanganyika 2025 maandamano na vurugu zote ziliratibiwa na wananchi wadogo a.k.a Gen-Z ambao hawakuwakilishwa na chama chochote cha siasa, hivyo hata ufanya MARIDHIANO na CHADEMA nao wataingia kwenye orodha ya wasaliti kama ACT-Wazelendo.
Na hiki ndio kitu ambacho hawajawahi kukielewa at least umeweza kuwafumbua macho...
 
Maelezo mazuri sana.
Kwa namna wanavyozidi kujichanganya, ninapata ukakasi sana juu ya uwezo wao wa kufikiri. Kufikiria hao ndio think tank ya Taifa, walah we are doomed🙆‍♂️🙆‍♂️🙆‍♂️
 
Sawa Malcom.... Je machafuko haya kuna mkono wa International agents? Nahisi kama kuna wageni wameingiza sera zao ili wanufaike nashindwa kuamini kama ni maamuzi ya Watanzania dhidi ya watanzania wenzao

Napata wasi wasi na hawa wawekwzaji wa hivi karibuni
Waarabu wana mchango mkubwa sana sana kwenye mauaji yaliyotokea kabla, wakati na baada ya uchaguzi. Najua wengi watadhani wanaosema hivi wana udini au wanachukia waarabu, lakini nina uhakika kuna siku nchi itakombolewa na tutakuja kushangaa sana kuhusu mchango wao. Katu Tanzania hatuna hulka ya ukatili kama huu uliotokea.
 
Waarabu wana mchango mkubwa sana sana kwenye mauaji yaliyotokea kabla, wakati na baada ya uchaguzi. Najua wengi watadhani wanaosema hivi wana udini au wanachukia waarabu, lakini nina uhakika kuna siku nchi itakombolewa na tutakuja kushangaa sana kuhusu mchango wao. Katu Tanzania hatuna hulka ya ukatili kama huu uliotokea.
Kwamba waarabu wao ni timu Samia au timu Gen-Z?
 
Tatizo hawasomi alama za nyakati wanajua bado tuko gizani..!!
 
Mwaka 2001 baada ya Dhalimu Mkapa kufanya ukatili wa kutisha dhidi ya nchi ya Zanzibar alichomoka kupitia MUAFAKA I.

Mwaka 2001 ilikuwa ni rahisi kuficha maovu na ukatili nchini Zanzibari kwasababu teknolojia ilikuwa haijakomaa hivyo watu wengi hawakufahamu kinachoendelea.

Mwaka 2025 baada ya Samia na Jakaya kutekeleza mauaji ya maelfu ya watanganyika nao wanataka kutumia kitabu kilekile cha Dhalimu Mkapa kutaka kuchomoka kupitia MARIDHIANO.

Mwaka 2001 Mkapa aligombana na wasimamizi wa uchaguzi kutoka nje ambao walitoa ushauri kuhusu michezo michafu. Mwaka 2025 Samia amegombana na wasimamizi wa uchaguzi kutoka nje waliotoa ushauri kuhusu michezo michafu na akawasuta kwa hotuba ileile ambayo Mkapa aliitumia mwaka 2001.

Ili kupata taswira ya haraka juu ya utofauti wa Zanzibar 2001 na Tanganyika 2025 tuangalie haya machache kwa haraka:

MOSI, Zanzibar 2001 walau uchaguzi ulifanyika na kura zikapinduliwa kihuni. Tanganyika 2025 uchaguzi haukufanyika lakini mgombea akashinda kwa kishindo cha asilimia 97%.

PILI, Zanzibar 2001 vurugu zilifanywa na wananchi kwa kuchochewa na wanasiasa wenye mlengo mkali, hivyo ilikuwa ni rahisi kufanya MUAFAKA kwasababu wanasiasa wakipata wanachotaka basi watu wao hutulia. Tanganyika 2025 maandamano na vurugu zote ziliratibiwa na wananchi wadogo a.k.a Gen-Z ambao hawakuwakilishwa na chama chochote cha siasa, hivyo hata ufanya MARIDHIANO na CHADEMA nao wataingia kwenye orodha ya wasaliti kama ACT-Wazelendo.

TATU, Zanzibar 2001 madhara yalikuwa ni makubwa mno kutokana pia na udogo wake kama nchi. Ila Tanganyika 2025 madhara ya vifo vya raia ni makubwa mno kuliko kule Zanzibar, na hili limechangiwa na ukubwa wa Tanganyika na watu wengi mno kushiriki maandamano.

NNE, Zanzibar 2001 vurugu zilikuwa sehemu na sehemu, hasahasa PEMBA. Nchi ilikuwa imegawanyika na baadhi ya wazanzibari ambao wanawachukia wapemba kwa kuwaita MACHOTARA walishiriki kwenye udhalimu mkubwa dhidi ya ndugu zao. Tanganyika 2025 vurugu zilitokea maeneo yote ya nchi hadi vijijini, na watanganyika asilimia kubwa walikuwa kitu kimoja bila tofauti za DINI, ITIKADI, SIASA, RANGI au KABILA.

Kilichofanyika jana 14/11/2025 baada ya matamko ya BAKWATA ni mbinu zilezile za JAKAYA KIKWETE za kupenda kutumia karata ya UDINI kuwagawanya Wakristo na Waislamu ambayo aliitumia tena mwaka 2010 kwenye uchaguzi mkuu akishirikiana na Prof. Ibrahimu Lipumba na Masheikh wa BAKWATA. Hii mbinu haitafanikiwa kwasababu, huku mtaani BAKWATA haiaminiki na haipendwi kabisa na Waislamu ambao wengi wao ni wahanga wa dhulma za CCM tokea awamu ya kwanza.

TANO, Zanzibar 2001 wanasiasa wake ambao ndiyo chanzo kikubwa cha maandamano walikuwa radhi kupata MUAFAKA na walipopata nafasi za kisiasa basi wafuasi wao wakatulia. Tanganyika maandamano hayakuwa ya wanasiasa hivyo MARIDHIANO ni jambo lisiloweza kuzaa matunda kabisa hata kama CHADEMA itakubali.

SITA, Zanzibar 2001 wanasiasa wote, Sheikh Karume na Maalim Seif pamoja na wafuasi wao walikuwa ni Waislamu. Kiasilia Zanzibar ni nchi ya kiislamu tokea karne na karne, leo hii raia wake zaidi ya asilimia 98% ni Waislamu. Hivyo mbali na kugawanyika kwenye RANGI, ila DINI ilikuwa ni jambo linalowaunganisha (A Unifying Factor).

Tanganyika 2025 ni tofauti, ukitoa UTANZANIA watu wa DINI na MAKABILA yao, japo hivi siyo vya msingi sana kwa raia wa kawaida, karata ya JAKAYA KIKWETE kuwatumia BAKWATA itawasaidia kwa muda tu, lakini ukweli ni kwamba BAKWATA hawana nguvu kubwa hivyo ya ushawishi hata dhidi ya Waislamu wenzao.

Sipendi kusema hili, lakini LISSU ni MKATOLIKI na HECHE naambiwa ni MSABATO (taarifa za marekebisho). Kanisa Katoliki ushawishi wake juu ya washirika wake ni mkubwa mno tofauti kabisa na BAKWATA, KKKT, au TAG. Hichi walichokisema BAKWATA leo hii kitaigharimu mno CCM na siku TEC watakapotoa WARAKA wao ambao kipindi hiki uko kwenye kuandaliwa serikali itatikisika mno na nchi itazidi kupasuka vipande.

SABA, Zanzibar 2001 CCM walipona kwasababu teknolojia haikuwa kubwa ya kuweza kufahamisha dunia kinachoendelea. Tanganyika 2025 karibia kila raia anazo video na picha za vitendo vya kutisha ambazo zitadumu vizazi na vizazi vikizidi kuleta hasira, doa na kuligawanya zaidi taifa.

NANE, Zanzibar 2001 lilikuwa ni janga la kitaifa (A National Crisis) na CCM pamoja na taasisi zake walifanikiwa kulidogosha na kuihadaa dunia. Bahati mbaya sana Tanganyika 2025 kutokana na teknolojia, limekuwa ni janga la kibinadamu (A Humanitarian Crisis) ambalo halimilikiwa tena na Tanganyika bali dunia nzima. Majirani wa Afrika wamelivalia njuga, Wazungu nao wamelivalia njuga, na kadiri siku zinavyoenda ndiyo bomu kubwa litalipuka.

Suala likishatoka kuwa Janga la Kitaifa (A National Crisis) hadi kuwa Janga la Kibinadamu (A Humanitarian Crisis) basi fahamu fika huwezi kulitatua kwa kutumia mbinu za siasa za ndani, huwa Jumuiya nzima ya Kimataifa (The International Community) inajiingiza hata kimabavu. Binafsi sidhani kama CCM ina msuli mkubwa kama Israeli, Urusi, Korea Kaskazini au Marekani kuweza kupambana na The International Community.

Mnaweza mkajiaminisha kwamba mbona hawa mabeberu tunakula nao na kulinda maslahi yao, lakini kama hata wao wenyewe wanageukana ninyi waafrika mnadhani hamtageukwa kweli ??? Kenya ni mshirika na muumini wao mzuri lakini walimshughulikia ipasavyo. Hata Makaburu waligeukwa na mabeberu wenzao. These are hard lessons.

================================================================
LEO HII NI HAYA TU.....
We nae mjinga mjinga tu,mimi nilienda piga kura,na niliona watu wakipiga kura,unasemaje uchaguzi haukufanyika!?
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Waarabu wana mchango mkubwa sana sana kwenye mauaji yaliyotokea kabla, wakati na baada ya uchaguzi. Najua wengi watadhani wanaosema hivi wana udini au wanachukia waarabu, lakini nina uhakika kuna siku nchi itakombolewa na tutakuja kushangaa sana kuhusu mchango wao. Katu Tanzania hatuna hulka ya ukatili kama huu uliotokea.
Wala hakuna UDINI ila ni ukweli mtupu. Washirika wakubwa wa Samia na Jakaya ni UAE, taifa ambalo linahusika na mauaji ya kimbari ya wasudani weusi kule Sudan. Ndugu zetu waislamu wengi hawana ujasiri wa kulizungumzia hili kwasababu wanafahamu fika kwamba Sudan kinachoendelea ni mauaji yanayofanywa na Waarabu dhidi ya weusi yakiongozwa na UAE.

UAE ni mfadhili mkubwa wa UISLAMU na hapo ndipo tatizo linaanza. Utawakuta kina Sheikh Ponda wanazungumza juu ya mauaji ya kule GAZA lakini Sudan kwasababu yanafanywa na waarabu hawewezi kukemea hata kidogo.

Kufika 2025, TPDF ndiyo mshierika mkubwa wa UAE tofauti na ilivyokuwa zamani ambapo tulishirikiana na UCHINA na URUSI. Baada ya Nkunda tumehama kabisa na sidhani kama kuna kurudi nyuma katika hili. Vyovyote vile Tanganyika imeshavamiwa na wametumia wazawa kuhujumu nchi.


​
 
Sawa Malcom.... Je machafuko haya kuna mkono wa International agents? Nahisi kama kuna wageni wameingiza sera zao ili wanufaike nashindwa kuamini kama ni maamuzi ya Watanzania dhidi ya watanzania wenzao

Napata wasi wasi na hawa wawekwzaji wa hivi karibuni
Watu mnaua kisa madaraka lawama WAWEKEZAJI?.🤔
 
Kila machafuko huwa ni fursa kwa watu. Hilo la mikono ya watu nitalisema siku nyingine, ila kuhusu maandamano na vurugu niseme tu kwamba nimeyashuhudia yote tokea yanaanza siku za kwanza sijasimuliwa: Vijana wanapigwa risasi na kukimbizwa hospitali nimeona, Kufukuzwa na magari ya jeshi nimeona, Nimesikia maneno ya vijana waliondamana na nikaogopa mno, Nimetembea mitaa ambayo ilifungwa (Lock-Down) nikashuhudia uharibifu, lakini kubwa nilitembea sehemu chache na kushuhudia jinsi ambavyo vitu vilipanda bei ndani ya usiku na kuona biashara haramu zikitamalaki na nimeshuhudia hadi watu wakigombania chakula hotelini kwasababu kilikuwa kimeisha.

Nachelea kusema serikali ilipoteza uwezo wa kuongoza Tanganyika kwa muda mfupi mno. Hawakujiandaa kwa jambo la namna hii na hawakuwa na kitabu (Script Book), zaidi zaidi ya kile cha 2001 Zenji, 2014 Mtwara, 2017 Kibiti. Mbinu na kitabu kilichotumika Kibiti na kina Mafwele ndicho waliamua kukitumia Tanganyika kote. Endapo Tanzania itaingia kwenye vita kama kubwa kama ile ya Kagera hata na nchi kama Rwanda au Uganda, amini nakwambia hatuwezi kumaliza mwezi nchi itakuwa ishapasuka vipande-vipande na serikali imeanguka.

JAMBO LA MUHIMU KUFAHAMU NI HILI: Every war is won on logistics not fighting alone. Serikali ya Tanzania ilizidiwa mno akili na walioratibu maandamano ambao ukweli ni kwamba FingerPrints za matukio zinaonesha kabisa kwamba ni wataalamu waliokubuhu wa mambo ya usalama hasa THE DARK ARTS OF INSURRECTION.

Kuhusu Logistics, maandamano rallying point yake ilikuwa ni UFUFUO NA UZIMA na UBUNGO INTERCHANGE/KIJAZI INTERCHANGE. Kimkakati KIJAZI INTERCHANGE ndiyo njia panda ya kimataifa muhimu kuliko zote Afrika Mashariki (The Busiest Interchange in East Afrika). Ukizingatia mji wa Dar Es Salaama ulivyokaa maelfu ya magari yanayotokea G/Mboto, Kimara, Mwenge na Magomeni yote hukutanikia KIJAZI INTERCHANGE.

Polisi na Wanajeshi wametawanywa Dar Es Salaam kote. Wataalamu walichofanya ni kufunga njia ya panda ya Kijazi (Barricaded the Kijazi Interchange) jambo ambalo lilisababisha magari yote kusimanana na foleni kubwa kufumuka. Ukifunga pale hata dakika 40 tu, foleni itafika hadi ndani ya muda mfupi sana Morogoro.

Ile Kijazi imefungwa, Mobility ya Riot Police ikawa ngumu kufika kwa haraka maeneo ya tukio. Hapa vijana wakajigawanya wengine wanaenda Shekilango Sinza, wengine Mwenge, na wengine Kimara wakishambulia kwanza vituo vya wapiga kura na kuharibu kila kitu. Hivyo adhma yao ya kuzuia uchaguzi ilifanikiwa kwa asilimia 100%.

Jambo jingine kuhusu vita ni The Element of Surprise. Waandamanaji walisema kwamba wangeanza kuandamana saa 12 asubuhi, lakini hawakufanya hivyo. Mpaka kufika saa 3 asubuhi serikali iliamini kabisa imeshashinda na mitandaoni nikaanza kuona maafisa wa usalama wa serikali, makada wa CCM na machawa wakianza kusherehekea kwa kubeza kwamba "Kiko wapi" ???

Muda ambao serikali ilidhani imeshinda, ndiyo vijana wakashambulia. Taharuki kubwa kwa watanzania na vyombo vya usalama wote tukishangaa imewezekanaje watanganyika hawa ambao wamelelewa maisha ya kuogopa wameingia kwa wingi vile barabarani. Nchi nzima haikuamini kinachotokea na ndipo kampeni kubwa ya Propaganda ikaanza kusambaa kama moto na sehemu zote Tanzania zikawaka moto kwa wakati mmoja, jambo ambalo serikali haikuwa na mbinu ya kulizima zaidi ya kutumia mabavu na kuendesha mauaji ya kikatili.

Muandamanaji wa kawaida ambaye anafanya maandamano kwa mara ya kwanza lazima anakuwa na woga na hajajipanga. Tanganyika watu walijipanga mno, na kila kilichofanyika Dar Es Salaam kilifanyika Mbeya, Mwanza, Arusha, Dodoma na Mara. Waandamanaji walishambulia vituo vya wapiga kura na kuviharibu, walianza kuchoma mali za makada wa CCM, kuharibu mabango ya Raisi Samia kwa kuyashusha chini na kuyatia kiberiti, ila baya zaidi ni kwenda kutembelea nyumba za vigogo wa CCM kuzichoma au kuwatafuta wanafamilia wao.

Sheli za Lake Oil zimeshambuliwa Tanzania kote. Hapa Dar Es Salaam kuna sheli nyingi mno kutoka Kijazi hadi Tabata, Mwenge, Shekilango na Magomeni ila kwanini walishambulia Lake Oil vile ??? Kuna sehemu niliwaona vijana waandamanaji wakichukua tairi kwenye duka la Mzee fulani wa kiislamu wakitaka walichome, yule mzee alitoka na kuwaambia hapo ndipo anapatia riziki ya kusomeshea watoto wake. Wale vijana waliacha mara moja na kurudisha yale matairi.

Ndiyo kwenye kila machafuko wizi na uharibifu usio na mantiki hutokea kwasababu kwenye kila msafara wa mamba kenge pia wamo. Ila ukilinganisha Tanganyika, Zanzibar au Kenya, hapa watu walikuwa wamejipanga mno na uharibifu kwa mali ambazo siyo za makada wa CCM ulikuwa Minimal.

KUBWA ZAIDI LA KUWATAARIFU: Hakuna kipindi Jeshi la Polisi limepoteza watu kama kipindi hiki. Polisi waliuwawa sana Mwanza na Mbeya. Aliyepiga marufuku Petrol kuuzwa alikuwa na akili mno. Mbeya walishaanza kutengeneza Molotov-Cocktails ambazo zilitumika kuwashambulia polisi.

Jambo ambalo watanganyika walikuwa hawalifahamu ni kwamba zile vurugu zingeendelea zaidi ya wiki, vyombo vya usalama vilikuwa nimeshaishiwa na akiba ya vifaa vya kutuliza vurugu. Gas Cannisters, Bullets and Petrol/Fuel vilikuwa vinaenda kuisha kabisa. Tangu siku ya kwanza walikuwa wanafyatua Gas Cannisters na Smoke Bombs ambazo Tanganyika haizitengenezi bali inaagiza nje. Walichofanya ni kuua watu na kuhakikisha mji unafungwa halafu wakawa wanapita kila baada ya masaa kadhaa wanafyatua risisi na mabomu kuonesha kwamba wako maeneo, ila ukweli ni kwamba viliisha na ingeendelea zaidi yangeikuta serikali.

SOMO KUTOKA LIBYA 2011: Serikali ya Ghaddafi ilitumia nguvu kubwa mno ya kijeshi kupambana na waandamanaji. Alikuwa anaenda kuwashinda maaduia, tatizo ni kwamba serikali iliishiwa na silaha kama risasi, mizinga na mabomu ambayo Libya aliagiza nje. Fahamu fika kwamba, silaha haziuzwi kama Pipi na Biskuti. Unapoagiza silaha nje ya nchi, unaweka order kabisa na zinazalishwa na kuanza kuletwa kwa miezi kadhaa.

TATC-NYUMBU hawawezi kuchonga risasi katika ngazi ya kiviwanda (An Industrial Scale), hawana watu wengi hivyo pia hata materials wanaagiza nje. Hivyo serikali ya Tanzania ingetumia mbinu ya kwenda kununua kwa majirani kama Zimbabwe, Mozambique, Burundi, au kuomba kwa Uchina, Urusi na Korea-Kaskazini jambo ambalo lingechukua muda mrefu sana.

NAMALIZIA NA HILI: Maandamano yalivyokuwa yanaanza, wanajeshi wengi kule MWENGE walikuwa wanawahamasisha watanzania watoke nje. Sehemu nyingine wanawaambia watanzania msichome kwanza, toeni mitungi ya gesi. Sehemy nyingine kama Sinza-Remi Ongala alishuka mzee na gari yake akatoa mapesa kuwapa vijana kama hongera ya kuandamana.

=================================================================
SIYO RAHISI KUANGUSHA DOLA, lakini miaka yote hapa Tanganyika serikali imetawala kimabavu kwasababu watu wamekuwa hawana vitu vikubwa viwili: UJASIRI na SILAHA. Matukio ya kutokea tarehe 29 Oktoba 2025, yamewapa Watanganyika kitu ambacho hawakuwa nacho kwa muda mrefu, UJASIRI. Matukio mliowafanyia yamepelekea wao kutafuta kitu cha pili ambacho ni SILAHA.

DOLA ingechanga karata zake vizuri kama Kenya na Ruto, maandamano yangeishia kuwa baina ya Gen-Z na serikali. Hata wazazi wangetumiwa kuwakemea watoto wao kwa madhara waliyoyasababisha au kufuata mkumbo. Lakini bahati mbaya sana ni kwamba mlipoanza kuwauwa hawa watato mlitengeneza MAELFU YA MISIBA. Hapa kwetu Tanganyika MISIBA ni suala la jamii nzima na siku zote MAREHEMU HUWA HANA DHAMBI, hata awe ni mkorofi kivipi.

Umemuaa AIKAMBE wa Kimara, ambaye ni mtoto kwenye familia ya SHIRIMA yenye watoto 4. Hao watoto wana marafiki zao wengine ambao watakuja kwenye msiba. Hata wazazi wa AIKAMBE hata kama wanafahamu mtoto wao ni Mkorofi watapata sababu ya kuhalalisha ukorofi wake kwa jinsi ambavyo ameuwawa kikatili. Mwezi wa 12 familia ya SHIRIMA huwa inakutana Krismasi kule Kilimanjaro.

Hivyo watapeleka huu msiba na mazungumzo makubwa huko yatakua ni jinsi AIKAMBE aliuwawa kwa amri ya SAMIA na KIKWETE. Ugomvi unageuka kuwa wa UKOO dhidi ya SERIKALI, jambo ambalo linaenda kutokea Kilimanjaro yote.

Sasa jambo kama hili linaendelea kutokea kule MBEYA kwa wakina Gwakisa na wazazi wake. Kule Mwanza kwa marehemu Mwololoku na Mzazi wake MAZIKU. Kule Mara kwa marehemu Masiko na wazazi wake kina MWITA. Hicho nachokisema hapa ni moja ya sababu kubwa kwanini vita haiwezi kuisha kule IRAQ, YEMEN, SYRIA na LEBANON.

=================================================================
Kila nikifiria siku za mbeleni moyo wangu hugubikwa na majonzi na woga mkubwa. Siku hizi nashindwa hadi kulala vizuri, nalala saa kumi usiku nakuwa kwenye mawazo mengi sana. The Tanzania we grew up in, is gone and it will never come back.


=========================================================
NB: Maafisa Usalama wa Tanzania walishindwa kusoma alama za nyakati. Dalili kubwa kabisa ya vurugu hizi ilionekana siku ile vitu vya Mwendokasi na Mabasi yake vilivyoshambuliwa kwa Mawe. Ili ilitosha kuwakumbusha kwamba ni watu wa aina gani mnaoshughulika nao kipindi hiki. Walipoilazimisa serikali kinguvu kutoa mabasi walifahamu fika kwamba serikali inaogopa.

Wale walioandamana kutoka Kimara tarehe 29 Oktoba 2025, ndiyo haohao watumiaji wakubwa wa Mwendokasi ambao miezi miwili nyuma walishambulia mabasi hayo kwa mawe na kupambana na polisi. Hili liliwapita kichwani au aidha mlilipuuza. Kuna kitu tunaita The Salami Slicing Tactic, ambapo unaanza kumshambulia adui kidogo-kidogo, siku anaamka ushamkata mwili mzima. Watanganyika walianza na Mwendokasi, wakaja Uchaguzi, kinachofuata hakitapendeza kabisa.
​
Hii ungeiweka kama mada inayojitegemea, ingependeza zaidi.
 
Back
Top Bottom