Mahesabu msiyopenda kusikia kuhusu Makamu mpya wa Rais

Yaani Chadema bwana wakati huo huo hawaitaki CCM na wakati huo huo wanawataka watu fulani wa CCM.
So pathetic
Kikatiba uchaguzi mwingine utafanyika 2025. Kwa sasa yeyote asiyependa CCM analazimika kuishi na CCM hadi 2025 atakapopata nafasi nyingine ya kujaribu tena.
 
Mzee Kayanza Peter Pinda atafaa sana kwa hii transition
 
Hakuna kitu kama hicho kitatokea,jeshi liko nyuma ya Raisi Samia suluhu Hassan.Unafikiri rahisi kihivyoo eeeh.
Rejea hotuba ya General Mabeyo jana.
Jeshi limesha ona likifuata hawa wanasiasa watapoteza nchi maana wote wana maslahi yao binafsi
 
Ndio mana nasema mama afumue mizizi yote ya JPM apange safu yake haraka na kuwaweka kando ya mfumo hawa wapambe wa JPM mana kivyovyote hataweza kuwaridhisha mana walishalamba Uhuru na Ukwasi mkubwa sana, Mama aje na safu yake ambayo itakuwa loyal kwake
Lakini pia hawa Walio achwa na Mzee nataka niwatahazarishe kuwa Amiri Jeshi Mkuu ni mtu mwenye Nguvu sana sana Wasijaribu kufanya lolote wataumia tu, Na hili mzee Magu ali prove kuwa Rais ni Mhimili uliojichimbia ndio maana tumeshuhudia watu kama kina kinana wana surrender, Hata Mkwere anafahamu fika power ya Rais achana na porojo za kitaa sijui kuungwa mkono, Rais anahitaji Inner circle ndogo sana ya kumsupport tena iwe loyal haswa the rest waweza kushugulikiwa wakati wowote na saa yoyote
 
Rais halazimiki kuvunja baraza la mawaziri. Ni hiari yake kufanya hivyo, katiba haijamlazimisha. Hivyo akiamua kuendelea na baraza hilohilo ni sawa tu, hatakuwa amevunja katiba popote.
Kumbuka hii ni serikali inayoendelea, ya awamu ya 5, siyo serikali mpya.
 
Kama ulimsikia kiongozi mmoja wakati anatoa salamu za kumuaga JPM akitamka mwaka 2022, ilihali akizungumzia tukio la mwaka 2020 hebu na anyooshe mkono.
Niliwaza sana kauli ile ya JK ni kuwa aliteleza au Ndio mambo ya Long term plan
 
Awaache mpaka wampigie kura ya kutokuwa na imani naye? Yeye mjinga wakati ana mamlaka makubwasana kuwazuia .
 
Japokuwa sijui siasa... Ila Aise msimsahau RC Anthony Mtaka ... Anafaa kabisa kuwa makamu wa rais... Ni maoni tu..
 
Ni uhuru wa mawazo na wa kujieleza. Hayo ni mawazo yako, na wengine pia wana mawazo yao. Karibu.
 
Spika mwenyewe wakati wa kutoa rambirambi, nilishindwa kumuelewa ni kama mtu aliyestukizwa!
Aliyoyayongea hayakuwa na mwelekeo au utashi wa Spika, Nahisi tunahitaji spika mwingine anaejitambua.
 
Bunge hili kutokuwa na imani na Rais!!! hakuna kitu hicho kutokea karibuni...kumbuka wabunge hawa wengi wameingi bungeni kwa "fadhila" ya alieondoka...
 
Huijui Katiba ya JMT nyamaza!!
Huna mamlaka ya kuninyamazisha. Kama unafahamu ibara ya katiba inayosema tofauti na nilivyosema iweke hapa tuelimishane.
Reaction sahihi kwa mtu asiyejua jambo siyo kumnyamazisha, ni kumjuza asichokijua.
 
Kwahiyo unadhani kutokuwa na imani na Rais ni kwamba makamu ndio atakuwa Rais?

Hakuna kitu kama hicho. Soma katiba vizuri.

Kuna mazingira ambayo makamu anaweza kuwa Rais kwenye Ibara ya 37 ya katiba yetu.
Mkimuondoa kwa kura ya kutokuwa na imani anakuja na kulivunja bunge na tunarejea kwenye uchaguzi.
 
Bunge hili kutokuwa na imani na Rais!!! hakuna kitu hicho kutokea karibuni...kumbuka wabunge hawa wengi wameingi bungeni kwa "fadhila" ya alieondoka...
Umenena vema, "aliyeondoka", siyo "aliyepo"
 
Weka vifungu mkubwa. Ibara ya ngapi hiyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…