Kenya 2022 MAHESABU YA KURA: Kumbe elimu ya Kenya ipo chini sana na upeo wa wakenya upo chini mnoo!

Kenya 2022 MAHESABU YA KURA: Kumbe elimu ya Kenya ipo chini sana na upeo wa wakenya upo chini mnoo!

Kenya 2022 General Election
Kwa maana hiyo sasa, kama walipiga kura watu 14,000,000 manaake kwenye majumuisho wanakuwa 14,001,400
Hao 1400 wametoka wapi?

Japo mwisho wa siku baba apumzike. Imetosha sasa!
Wacha Hustler Ruto aongoze Kenya kwa amani!
Umechanganya vitu viwili kwa wakati mmoja. Hoja za wale makamishina wanne za hesabu ziko mbili.

Hoja yao ya kwanza ni kuwa Jumla ya asilimia ya wagombea wote wanne ni 100.01% badala ya kuwa 100%. Kuwajibu hoja yao hiyo ni kuwa hiyo 100.01% inajitokeza ikiwa umejumlisha asilimia zenye desimali zilizovutwa (Round off decimal), kimahesabu ni jambo linaweza kujitokeza, na linapojitokeza linapaswa kuupuziwa kimahesabu (Neglibible error). Hivyo haipo popote na haijajumuishwa popote kwenye kura
What is 10% ya 14 000,000
What is 1% ya 14,000,000
What is 0.1% ya 14,000,000
What is 0.01% ya 14,000,000
Compare the answers of the above to maths calculations za four commissioner's

Wale makamishna walisema wazi kuwa, asilimia iliyozidi ni 0.01% na wakasema kimahesabu yao hiyo ni sawa na kura 140,000.

Vyote viwili walivyosema hapo kimahesabu ni uongo mtupu. Hakuna mahesabu ya namna hiyo duniani popote.
 
Kituko kikubwa cha karne kuhusu hesabu leo kimeonekana huko Kenya baada ya makamishina wanne wa tume ya uchaguzi waliotangaza kujitoa kwenye mchakato wa kutangaza matokeo ya urais kuja na hoja finyu za ukilaza wa mahesabu.

Mbali na sababu zingine walizozitoa, kubwa lilikuwa ni wao kujenga hoja kwenye mahesabu ya matokeo kwenye mambo mawili.

-Wao kushangaa hesabu ya jumla ya kura zilizovutwa (round off) kuwa 100.01% (Kitu ambacho kimahesabu kiko sahihi)

-Kudai kuwa hiyo 0.01% iliyozidi wao wanaitafsiri katika kura zote (milioni 14) ni sawa na kura 140,000. (Kitu ambacho sio sahihi, usahihi ni kura 1400)

Ajabu ni kuwa, wahusika waliojenga hoja hizo walijitamba kuwa wao ni wasomi na karibu kila mtu kwa Kenya ni msomi wa kuweza kuchambua hayo mahesabu. Na mwisho hoja zao zikachukuliwa na kupigiwa debe na mamilioni ya wakenya wanaomuunga mkono upande wa Raila Odinga.

Hizo hesabu za desimali na makadirio huwa zinazofundishwa watoto wa darasa la nne hapa Tanzania na nyingine kurejewa kwa kina kidato cha kwanza.

Ni aibu kubwa kwa taifa la Kenya, ukilaza unaposhabikiwa na kuungwa mkono.

Poleni Wakenya kwa hii aibu.
Mahakama ikithibitisha kuwà kuna kura zaidi ya asilimia 100 zilizopigwa hata iwe 0.01 ngoma inarudiwa.
 
Back
Top Bottom