Mahojiano yangu na washirika wa FDLR kuhusu uhasama wao na RPF- Inkotanyi

ushauri aliotoa kikwete ndio ulikuwa the best. FDLR ni wanyarwanda, huwezi kuwafukuza nchini wakae uhamishoni milele kama kagame alivyoishi uhamishoni zaidi ya 30 years, halafu ukasema upo salama. kuna siku tu wao au watoto wao au wajukuu zao watakuja kukurudia na wewe unaweza kufukuzwa ukaishi uhamishoni miaka hiyo vilevile. la maana aliloshauri kikwete lilikuwa ni wakutane, wasameheane, waishi pamoja kama wanyarwanda, hiyo haingempunguzia chochote kagame kwasababu tayari yeye ni rais. maadamu wapo msitu wa congo ambako kuna waasi kibao na kagame mwenyewe alishaishi msitu wa congo, watoto wao watakuwa wazoefu wa vita sana huko kwa waazi na kuna siku watarudi rwanda kwa kishindo. sema kagame anafadhili m23 ambao ni watusi wenzie ili wawe wanapunguza nguvu, sasa hatujui kama m23 watadumu milele na kama hatatokea nchi yeyote duniani adui wa kagame akafadhili FDLR ili kumkomesha kagame. amevaa mabom bila yeye kujua.
 
Hahahahah, nice , paul vs afande F ,hongera Jacob kwa uzi mzuri
 
Sasa kuna kizazi cha 1994 nacho kipo uhamishoni wanataka kurudi ,wkt huo Paulo anataka kutoa madaraka kwa kizazi cha umri huo lkn kilichotoka uhamishoni
 
Upo sahii mkuu
 
Mkuu ina maana RPF ni jeshi la Watusi pekee?
 
Hawakuwa na maisha marefu jeshini kwanini? Waliuwawa? Au walifukuzwa?
 
NB:ALIR NI TAWI LA WALIOJITENGA NA FDLR NA HII NI HABARI NDEFU SANA INAHITAJI UZI WAKE PEKEE
Hizo sababu za wao kujitenga na Fdlr unaweza kututajia kwa uchache ?


ASKARI WOTE WA KIHUTU WALIOJIUNGA NA RPF HAWAKUA NA MAISHA MAREFU JESHINI.
Baada ya Rpf kudhibiti nchi, Kuna uasi bado uliendelea hivyo baadhi ya askari wa jeshi la Habyarimana waliingizwa kwenye vikoai vya Rpf na kupewa vyeo ili kuzima huo uasi, vipi sasa hawakudumu?

Bizimungu alikuwa mhutu mwenye cheo ndani ya Rpf, kipi kilimsibu mpaka kutofautiana na makamu wake mwenye nguvu ?

zitto junior
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…