INAENDELEA..........!
Ukiwa nchini Rwanda mwaka 1987 kuna usemi mkubwa ulikua unaenea miongoni mwa vikosi vya wanajeshi wa jeshi la serikali kwa mujibu wa afande ""F"" nao usemi huo ulikua unasema kua Wafaransa wanataka kuigawa nchi kwa watusi na ikumbukwe kua asilimia 100% ya wanajeshi walikua ni wahutu na jambo hili lilikua linaondoa weledi wa kijeshi kwa jeshi la Rwanda na kuleta ukabila kwa mujibu wa afande""F"".
Afande ""F""ambae alikua na cheo cha ukanali anasema baada ya kuwasilisha ripoti yake ya kijasusi mbeke ya komandi kuu ya kijeshi, alitoa pia ripoti ya mapendekezo kuhusu nini kifanyike ili kuweka mambo sawa mahali palipoyumba.
Na alisisitiza kua jeshi lisichanganywe na siasa za nchi husika. Baada ya hapo afande ""F""alirudi mpakani mjini Katuna kuendelea na kazi yake ya kulinda mpaka wa nchi ya rwanda.
DECEMBER 14 1987 KATUNA RWANDA.
Ilikua usiku mida ya saa nne na robo wakati ambao kanali afande""F"" alikua ndio anamalizia mlo wa chakula cha usiku ili akatazame ripoti ya ulinzi afu apumzike,alipopokea simu ya upepo (Radio call) ikimueleza kua kuna magroup ya vikundi vya watu wenye silaha wamevuka mpakani upande wa Uganda kitongoji cha kihunda na wameingia ndani ya aridhi ya rwanda wakiwa na maguruneti ya kurusha kwa mkono na maroketi ya kutungulia ndege na maroketi ya kuzuia vifaru na ni watu ambao kwa idadi yao hawazidi watu 800.
Afande "F" aliamka akavaa mkanda wake wa risasi za akiba kiunoni na akaijibu ile redio upepo kua kila komandi iandae ambushi au shambulio la kuvizia kama wale watu watavuka kilometa tatu kutoka mpakani na wawazingire kutokea upande wa mlimani wa kihunda na wasiwashambulie mpaka akitoa idhini.
Yeye binafsi alipanda Jeep ya kijeshi na kuifanya iwe komandi station yake kufuatilia hali yote nzima,,na kuripoti pia katika kamandi kuu mjini Kigali.
Kulikua na ukimya mkubwa ila baada ya dakika ishirini na saba ,,alipokea tena simu ya upepo ikisema upande ule wa kihunda mlimani kua wapo katika mfululizo wa mashambulizi ya risasi na roketi na maguruneti kutoka kwa vikosi vilivyoripotiwa mwanzo kuingia na vilikua vimevaa sare za jeshi la uganda,na walikua wanaacha maeneo yao na kurudi nyuma ili kuzuia maafa zaidi maana walikua wanazidiwa nguvu na wale watu waliowavamia.
""""""Namnukuu Afande F """"""
Hali ilikua tete maana vile vikosi vilivyovuka mpaka kutokea uganda vilikua na silaha bora na uzoefu wa kupigana milimani kuliko vijana wetu tuliokua tumewaweka jeshini mwaka huo na wengi wao hawakupata mafunzo ya kutosha kuhusu mapambano ya uwanja wa vita,bali mafunzo ya kulenga shabaha tu na mafunzo ya utimamu wa mwili na akili kama wanajeshi.
"""""Nimemaliza kunukuu"""""""
Afande F akaamua aombe usaidizi wa kikosi anga cha jeshi la Rwanda kikichokua kipo uwanja wa ndege kigali na pia kwenye uwanja wa ndege wa kijeshi katika kambi ya kijeshi ya Kamina ili apatiwe helikopta za mashambulizi ya angani na ndani ya lisaa limoja zaidi ya helkopta 11 zilikua tayari zipo uwanja wa mapambano kwenye mlima kihunda zikiwashambulia watu waliovuka mpaka kuishambulia rwanda kutokea Uganda na wakafanikiwa kuwarudisha nyuma na kuua wengi kati yao,,ila na wao walikua wamepata hasara za kutosha za maisha ya watu na mali katika post zao za mpakani upande ule wa mpakani ambapo mashambulizi ndipo yalipotokea.
Ikumbukwe kua kama anavyosema afande""F"" zile helikopta zote za kufanya assaulting zilikua zinaendeshwa na marubani wa kifaransa kutoka katika jeshi la anga la ufaransa lililokua na kituo katika uwanja wa ndege wa Kigali.
Afande ""F""anasema cha ajabu aliambiwa hili tukio asilitangaze kwa mtu yoyote yule na iwe siri raia wasijue kama habari rasmi bali uvumi.
Kwa mara ya kwanza hiyo December 14 1987 ndio kanali au afande""F"" alipambana na wanaharakati wa rwanda patriotic front wakitokea ndani ya jeshi la uganda waliojaribu kijeshi na kwa mapambano ya kurushiana risasi kuvuka mpaka na kuingia nchini rwanda wakitokea uganda kwa upande ule.Walikua wamejizatiti kwelikweli na haikua rahisi kuwarudisha nyuma bila msaada wa wanajeshi wa jeshi la anga la ufaransa.
PAULO JACOB KAGAME!
Huyu alikua ni nani na movement yake ya TWEHEZA ilikua inahusu nini na kwanini alikua na mahusiano ya karibu na serikali zote tatu za Uganda na Zaire na Rwanda kwa wakati ule.Na kwanini alikua mshirika mwaminifu wa afande""F"" katika medani ya ujasusi kwa kipindi cha miaka tisa mpaka mwaka 1990 walipokorofishana.
Paulo alikua mfanyabiashara na mwanajeshi pia na jasusi pia na mwanasiasa pia kwa wakati huo huo.
Paulo alikua mtu wa kuzitazama fursa kwa jicho la mbali na kuzikimbila. Paulo alikua mshirika aliyeaminika wa CIA na MOSSAD na M-15 na kuna nyakati alishirikiana na KGB na TISS kama. double agent.
Paulo aliweza kujinasibu kama mtu wa kuaminika wa serikali ya Rwanda toka mwaka 1982.Ni yeye pekee tu aliyekua na acsess ya kupata direct instructions kutoka kwa raisi,akiwazidi hata wale majasusi waliokuepo ndani ya serikali na aliaminiwa na jeshi hadi mwaka 1990 alipowasaliti kwa mujibu wa afande""F""
Tutaijadili movement ya TWEHEZA huko mbele ili tuifahamu. Baada ya tukio lile la mwezi December tarehe 14 mwaka huo 1987 basi hali ya mpakani mwa uganda na rwanda ikabadilika na kukawa na ongezeko la vikosi vya wanajeshi wenye uzoefu na vifaa katika mpaka huo hasa upande wa rwanda.
Katika mahojiano yetu afande""F""anasema kua wakati yeye yupo jeshini,pia kulikua na hisia za ukabila za hali ya juu baina ya jamii mbili kubwa za Watusi na Wahutu.
Na hili lilichangiwa na wanasiasa wa kinyarwanda waliokua na uchu wa madaraka.
ITAENDELEA....!