GE2025 Maigizo au Utakatishaji fedha? CCM njooni hapa tusemezane

GE2025 Maigizo au Utakatishaji fedha? CCM njooni hapa tusemezane

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mlifanya makosa makubwa kumpa Tundu UWENYEKITI wa CHADEMA na Heche maana wale wote 2 ni vichwa maji. Hakuna mwenye utulivu wa akili ambaye angeweza kumshauri vinginevyo mwenzie. Nawaona kama majuha. Walishindwa kuusoma mchezo wa Samia.

Lissu anaropoka kuanzisha uasi mwezi April 2025 na baada ya mwezi 1 anakamatwa na kuwekwa ndani.

Mwezi mmoja baadaye Msajili wa vyama anaitisha kikao cha kusaini kanuni za maadili, naye Heche anagoma KUSAINI. Tundu kachonga jeneza la CHADEMA na Heche kapigilia misumari.

Wenzenu wanakwenda kwenye uchaguzi nyinyi CHADEMA mnakwenda Mahakamani. Wenzenu wanafanya fundraising nyinyi akina Mshana Jr mnakesha kuandika nyuzi za kuponda.

Fanyeni matanga ya msiba wa CHADEMA ila tarehe 29/Oktaba muanue tanga
Nimejikuta nakuonea huruma Sana kwa hiki ulichoandika ila kwakuwa sikufahamu physically.. Kuna maoni yangu siwezi kukuwekea
 
Hatua ya Kwanza
Mgombea Mwenza anatoka hadharani tarehe 11/ 08/ 2025 na kudai kuwa chakavu wanahitaji 100B waweze kufanikisha kampeni ya kubakiza Costra Nosta sebuleni kwao. Roadmap ni harambee scheme

Hatua ya pili
Tarehe 12/ 08/ 2025 inafanyika harambee kabambe ambapo jumla ya Bilion 86+ zinakusanywa. Wafanyabiadhara wanaonekana walikuwa wameshajiandaa kitambo kuchangia.

MATUKIO FIKIRISHI
  1. Tangazo la harambee linatoka leo, kesho yake tukio linajiri kwa ufanisi mkubwa
  2. Kamati ya maandalizi hakuna wala waratibu lakini mialiko imeshatumwa, ukumbi umeshachaguliwa na kulipiwa less than 24hrs pamoja na itifaki zote kupangiliwa na kupangika
  3. Washiriki ni wawekezaji wakubwa ambao ndani ya muda mfupi wameonesha kujiandaa kikamilifu kushiriki huku wengine wakijinasibu kuwa walifanya vikao na wenzao waliowawakilisha
Kwa hayo machache tujiulize tumegundua nini kwenye hili jambo?

My Take:
  1. CCM kuishiwa mikakati na mbinu za kipropaganda ni ajali, makusudi au kukosa kujiamini?
  2. Tukio hili la harambee linazidi kuiweka CCM shimoni kwa sababu sehemu kubwa ya washiriki wanatuhumiwa kwa.ufisadi na matukio yanayohusisha kukosa maadili kijamii.
  3. CHADEMA imeendesha kampeni zake kwa kuchangiwa na Watanzania wengi kwa mtindo wa tone tone, lakini CCM inachangiwa mabilioni kutoka kwa matajiri wachache. Hii inatuma ujumbe kuwa wenye nguvu wameungana na kujenga umoja nyuma ya CCM kuwakabili wanyonge wa tone-tone
  4. Mtanzania unaenda kutiki hapo Oktoba kwa utaratibu ama demokrasia ipi?
  5. Suala la utakatishaji fedha lipo kwenye heading tu. Sijaliandikia humu ndani zaidi ya passage hii

CCM akina Tlaatlaah, Lucas Mwashambwa, chiembe, Pascal Mayalla, Ritz na wengineo, nawaalika tujadili haya maigizo ya chama chenu...
MiCCM ni mijitu mititusa sana.
 
Write your reply...kila mtu anashabikia kitu kinachompa maslahi kimaisha tambua kutafuta ridhiziki ni vita isio kwisha kila siku ni mapambano ya jasho na damu hivyo huwezi kumzuia mtu asifanye kile kinachompa ridhiki iwe halali au dhuruma
Kuna faida gani ya kuwa na uongozi pamoja na Sheria?
 
Mwalimu wangu Nguruvi3 na Mwalimu wangu wa Tuition Mag3 , Mchambuzi na wengine wengi tuliokuwa tunatembelea jukwaa la "Great Thinkers" ukimya wenu unanipa wasiwasi.

Mje msaidie kutoa elimu ya namna kujadili masuala mazito yanayolihusu Taifa.
 
Hizi ni siasa mjomba.Siasa ni akili na mbinu haijalishi ni mbinu gani.Sasa kama wewe unafikiri unavyoandika andika hivi mitandaoni au kuwaita majina mabaya wenzako wanashtuka utakua unajidanganya.Ccm ilishatoka uko kitambo.
Chakavu Chetu Mbovumbovu ( CCM)
 
Back
Top Bottom