Pitieni biashara za Wahindi ndiyo mtagundua Simba ni biashara kubwa inayouzwa kwenye frame badala ya mall.
Usije ukaona Muhindi anategeneza hela ndefu kwenye biashara zake, ukadhani na wewe ukiajiriwa utalipwa kama yeye.
Malipo kwenye kampuni za Wahindi huwa hivi;
Boss/Mkurugenzi/Mwenye Kampuni na wafanyakazi wengine wa kihindi.
1. Mshahara tshs 700,000/- (laki saba)
2. Housing allawance tsh 5,000,000
3. Usafiri tsh 3,000,000/-
4. Security tsh 1,500,000/-
5. Mawasiliano tsh 1,000,000/-
6. Health insurance tsh 4,000,000/- (kutibiwa Aga Khan).
JUMLA = Tsh 10,700,000, (Ondoa bima), hii ndiyo wahindi huwa wanakunja kwa mwezi.
Mfanyakazi wa Kibongo kwa wahindi.
1. Mshahara tsh 400,000/- (utadai vipi zaidi wakati mkurugenzi analipwa laki saba?)
2. Allowance ya chai chapati moja au kachori)
3. Bima ya matibabu tsh 300,000/-
JUMLA = Tsh 400,000, hii ndiyo mfanyakazi/mhasibu/IT mbongo wa mhindi anakunja kwa mwezi
Sasa hapo inabidi utafute juhudi ya kutoboa kimaisha.