Mainjinia wa Maji wa Mikoa watakuwa wameenda field usiku huu kuhakikisha sehemu zote hatuna shida ya Maji

Mainjinia wa Maji wa Mikoa watakuwa wameenda field usiku huu kuhakikisha sehemu zote hatuna shida ya Maji

Chukwu emeka

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2018
Posts
24,314
Reaction score
38,919
Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kama kuna watu usiku huu hawatalala ni Mainjinia wa Maji na wilaya katika mikoa mbalimbali nchini, kauli ya Rais, Mama Samia kuwahusu itawakosesha amani kabisa hasa kama kwenye maeneo yao ya kazi kuna miradi inasuasua. Joto lao wengi litakuwa limevuka 37C..

Wengi wamezoea kufanya kazi kwa mazoea sana,wamezoea rushwa, wanawasumbua sana wananchi wanapowafuata maofisini mwao na wanausumbufu mkubwa wa nenda urudi baada ya wiki.

Kwanza, watapelekeshwa sana na Waziri maana nayeye ameshaambiwa akizingua, atazinguliwa.

Maji ni uhai, mama akifanya vizuri kwenye maji atawasaidia mama zetu kwa kiwango kikubwa sana maana kubaadhi ya maeneo kuna shida kubwa sana ya maji.

Na kazi iendelee......
 
Kuna sehemu mpakavunashangaa vyanzo vya maji vingi lakini maji hayatoki kama vile wilaya ya Rungwe,Busokelo,Kyela,mito kibao ,mabomba yapo maji hayatoki ,Hawa wajitathimini siwachongei ila wale uvivu wao.Hapa kazi iendelee.
 
Mama anza na Kwimba maana kero imekua endelevu yani huduma ya maji inapatikana kwa magumashi mno hasa mji wa Ngudu na maeneo yote huku vijijini tunatumia kitu inaitwa malambo
 
Kuna sehemu mpakavunashangaa vyanzo vya maji vingi lakini maji hayatoki kama vile wilaya ya Rungwe,Busokelo,Kyela,mito kibao ,mabomba yapo maji hayatoki ,Hawa wajitathimini siwachongei ila wale uvivu wao.Hapa kazi iendelee.
Nikweli kabisa, huko kuna mto kiwira na Songwe pamoja na vimito kibao kabisa
 
Tatizo taasisi nyingi za Serikali watu wanafanya kazi kwa mazoea maana hakuna kupimana katika utendaji kazi na pia Kuna Kama kuogopana Fulani.
Kama taasisi hizi watu hawatawekewa malengo ya kazi na kusimamiwa vyema malengo hayo daima uzembe hautokaa uishe.
Nikweli, kujuana jana pia kwingi....ningumu kupata kazi bila kimemo....wamejazana kwa kujuana tu humo.....sitasahau kuna taasisi tulifanya usaili kwa post ambayo mtu tayari anafanya training
 
Na kila mwezi wanakula mishahara na posho,mvua maeneo hayo karibu ni mwaka mzima,Yaani kama nivkweli Raisi kaamua waende tuu kufanya kazi zingine.
Yeah nikweli Rungwe ni kijani kibichi mwaka karibia wote, na kyela ni bonde ambalo maji hata ziwa nyasa tu au mto Songwe au kiwira yangetosha kabisa
 
Back
Top Bottom