Uchaguzi 2020 Maisha Baada ya Uchaguzi: CCM won the Battle and lost the War

Uchaguzi 2020 Maisha Baada ya Uchaguzi: CCM won the Battle and lost the War

Kwann Mbowe asitoe maelekezo kwamba wafuasi wote wa upinzani waombe kujiunga CCM.

Waisifie ccm, waende wakaongeze uahindani ndani ya CCM.

Humu jukwaani Woote tuwe ccm, asiwepo mpinzani hata mmoja. Na kila elekezo linalotolewa na ccm lipongezwe sana. Mada ziwe ni kupongeza tu bila kuchoka.

Huu ndo utakua mwelekeo wa siasa za 2020 mpaka atakapoamua kuondoka au watu watakapochoka na kumuondoa.

Kwa sasa salama yako ni kusifu.
 
Huu ndo utakua mwelekeo wa siasa za 2020 mpaka atakapoamua kuondoka au watu watakapochoka na kumuondoa.

Kwa sasa salama yako ni kusifu.
Ss basi tuanze kampeni za kuondoa ukomo. Lazima wote ccm na upinzani tupate tunachotaka. Tusikwamishane kabisa. Twende na mwelekeo wa kijani.
 
This was expected. Aliyeamini kitu tofauti alikuwa akiota mchana au alikuwa akijifariji moyoni tu ili kujipunguzia stress

Huwezi kushinda uchaguzi kwa TUME hii. Lissu, Zitto, Mbowe etc wote wanajua hili.
 
Asante Mkuu niseme Amen, lakini kumbuka hata Viongozi wa Upinzani Sio magenious au malaika kiasi Kwamba wakipewa Nchi itageuka Kuwa paradiso ghafla.. Nawapa pongezi watanzania kwa kuyapokea Matokeo, na pia nawaomba wakubaliane na Matokeo ya waliojiamulia leo yawe mabaya au mazuri, kupanga ni Kuchagua

Era ya kuishi mawazo ya mtu mmoja haina manufaa kwa nchi.

Iwe wapinzani wameshinda au la, mfumo wa kuweka checks and balances ni muhimu.

Ndiyo maana nasema nakuombea maisha marefu uone matunda ya huu uchaguzi.
 
Hakuna aliyetegemea uchaguzi uwe wa huru na haki. Lakini hakuna aliyetegemea wizi uwe wa wazi na wa kijinga hivi.

Chama Cha Mapinduzi, kama chama kikongwe barani Afrika, kimethihirisha hakipo tayari kuachia madaraka kwa njia ya sanduku la kura. Si Bara wala si Visiwani.

CCM si chama cha siasa tena, CCM ni mfumo uliyoishikilia nchi hii mateka. Hamna tofauti na CCP China, Putin’s Russia, Kim’s Korea, Castro’s Cuba, Lukashenko’s Belarus, n.k. Mifumo ya kisoshalisti na kikomunisti iliyoasisiwa na Mwalimu Nyerere.

CCM kwanza, Tanzania baadae. Wakuu wa vyombo vya dola pamoja na wakuu wa majeshi wapo kulinda kwanza maslahi ya Mwenyekiti wa CCM kisha CCM na mwisho Tanzania.

Kwao adui wa Mwenyekiti wa CCM ni adui wa Tanzania. Adui wa Chama ni adui wa Tanzania.

Huu uchaguzi ni kichekesho kingine kama ilivyokuwa 1995, 2000, 2005, 2010 na 2015. Mawakala wa vyama vya upinzani wanakamatwa na kutolewa kwenye vituo. Kura feki kwenye mabegi na maboksi zinaingizwa kujumuishwa kwenye mahesabu.

Haya yanasimamiwa na wakurugenzi, wakuu wa wilaya, wakuu wa Usalama wa Taifa na wakuu wa mikoa. Nani mnamdanganya?

Majeraha ya Uchaguzi huu, tofauti na miaka mingine, ni mpasuko mkubwa na kuhatarisha umoja wa nchi.

Watu wameenda kupiga kura ili roho zao ziwe na amani tu, haijalishi mtaiba kura zao au la! Hii ni chuki kubwa imepandwa.

Kibaya zaidi tofauti na watangulizi wa nyuma, Rais Magufuli hajui na hawezi kuunganisha Taifa kwa kauli na matendo yake na amezungukwa na wabinafsi wa hali ya juu.

Ni rahisi kushangilia na kusema wameshinda na kuwagaragaza wapinzani.

Ni rahisi kwa wachambuzi wa mambo ya siasa kusema "Upinzani bado sana" au "Upinzani haukujipanga". Unabaki kujiuliza, kwa mazingira haya unategemea upinzani ujipange vipi ili kuwe na haki.

Media zote zimefungwa mdomo. Hakuna uchambuzi, sharia ni kusoma kile watawala wanataka basi.

Mediocrity (Sabaya, Makonda, Mambosasa, Polepole, Kabudi et al) is the order of the day. Short-termism is the norm.

Ipi gharama ya ushindi huu kwa CCM? Kupasua umoja wa nchi? Kutumia silaha na nguvu kuhalalisha ushindi hakukupi ushindi bali kunakuongezea maadui.

Mfano leo hii Kusini kuna tishio la Ugaidi bado tena unawaibia hao watu haki yao ya kuchagua viongozi wanaowataka. Wakuu wa Usalama na Ulinzi wanategemea nini?

Inasikitisha haya yanafanywa na tume iliyoundwa na Majaji na Wasomi. Haya yanasimamiwa na Majenerali wa vyombo vya Ulinzi na Usalama. Hii yote ni kumfurahisha Mwenyekiti.

Imemchukua Baba wa Taifa zaidi ya miaka 20 na Watanzania wamepitia sacrifices nyingi kujenga Umoja katika nchi hii.

CCM Mpya chini ya miaka 5, inafanikiwa kuvunja hii legacy na kujisifu wao ni wazalendo.

Nchi inaingia kwenye giza kubwa na kuishi mawazo ya mtu mmoja tu ambaye si mwerevu.

Taifa linaelekea kwenye mpasuko mkubwa tokea tupate Uhuru.
Very true
 
The gov is broke asf and have ongoing big project which need a lot of funding it does'nt have, they will squeez every penny from y'all and they wont give a damn if you are broke too.

And they will all be talking about plane, roads and flyover like its everything a citizen need
 
The gov is broke asf and have ongoing big project which need a lot of funding it does'nt have,they will squeez every penny from y'all and they wont give a damn if you are broke too.
And they will all be talking about plane,roads and flyover like its everything a citizen need

Bwawa la umeme la Nyerere linakisiwa kugharibu Shilingi Trilioni 9.

Haya makisio yanasemekana ni ya chini na inaweza kuwa mara mbili yake.

Mradi huu unalipwa in $. Utalii ambao ni biggest earner wa $ upo chini for the next two years.

Donors watapunguza misaada na wengine hawatatoa kabisa. Sekta ya Afya na Elimu itapata shida.

Hapa kuna watu wanashangilia. Bado miradi mingine mingi ipo haijafikia hata 50%, mfano SGR.

Bado ATCL inahitaji ruzuku.
 
Chadema ni watu wasio na staha kabisa , watu wafedhuli, wapenda matusi tuuu, inasikitisha Sana hata mode walikuwa upande wao daily kupigana ban ovyo ovyo just to defend their cowardnes, nashukru Wananchi wamewanyoosha ipasavyo. Hawa watu siwez wahurumia hata kdogo very ridiculous.
 
Hebu waambie hao,TZ itaendelea na amaani kama kawaida.Mtu kata zote umepigwa ndio ushinde
 
Kwani Ukihamia na wewe CCM Kama Mtanzania wa kawaida utapata Hasara gani Mkuu. Hujistukii tu hata hapo ulipo watu hawawazi Kama unavyowaza wewe watu wetulia kabisa maanake we ndo unaakili kuwazidi wao ama?
Upinzani kuongoza Hii Nchi bado Sana.. Kama majimboni tu wameshindwa Nchi wataiweza kweli Mkuu, Watanzania tumebarikiwa na Mungu, uwe na Imani na uongozi wa Magufuli Ila hao wabunge wenu huko majimboni ruksa kuwa doubt!!
Komenti ya kimbwa mbwa kama1hii ndiyo tatizo la kukabithi vichaa nchi we will remember black 2015 for ever
 
Baba wa Taifa aliwahi kusema mpumbavu ni sawa na MTU mfupi ambae huwezi kumrefusha na ukilazimisha kumrefusha utamuua.Nchi imeshachanika wajinga wanaweza kuelewaelewa hv ila usitarajie wapumbavu wataelewa mambo haya sio rahisi ksbisa .
 
Back
Top Bottom