AbuuMaryam
JF-Expert Member
- Dec 26, 2015
- 2,577
- 4,637
NASAHA MUHIMU SANA...
Maisha mazuri au mabaya hayaletwi na kiongozi, bali ni kwa yale yanayochuma mikono yetu, tubadilike na tuwe wema kwanza sisi!
Tusijidanganye kwa kura, tufanye subra na tumche Allah tumtii kiongozi tuliyepewa na tuwe waadilifu.
Kura haziwezi kumuondoa au kumweka kiongozi ila akitaka Allah yeyote yule atamuweka.
Utapiga kura kwa unayemtaka, ila hatakuwa kiongozi isipokuwa aliyemtaka Allah. Na hata kama akiwa yule uliyemtaka. Allah hashindwi kuwataabisha juu ya huyo huyo mliyemtaka.
Jamani ndugu watanzania, tusifanye majaribio ya kumbugudhi au kutaka kumuondoa kiongozi aliye madarakani
Hatuwezi wote kuwa viongozi, Allah humpa uongozi yeyote anayemtaka yeye, na atamuondoa akitaka yeye!
Tuzikubali na kuzitii mamlaka zozote ambazo allah ataziweka kwa ajili yetu.
Inawezekana kabisa mkafanikiwa kumuondoa kiongozi aliyopo madarakani, ila kutokana na dhambi za mikono yetu allah akatuletea kiongozi dhaalim zaidi kuliko tuliyemtoa hata kama tumemchagua wenyewe.
Wangapi wamechagua wao wenyewe machaguo yao wenyewe wanaowapenda lakini mwisho wa siku walipoingia madarakani walikuwa waovu kuliko walivyotarajia, na walijuta juu ya yule wakitamani angerudi?
Jamani ndugu watanzania, tusifanye majaribio ya kumbugudhi au kutaka kumuondoa kiongozi aliye madarakani.
Hatuwezi wote kuwa viongozi. Allah humpa uongozi yeyote anayemtaka yeye. Na atamuondoa akitaka yeye!
Tuzikubali na kuzitii mamlaka zozote ambazo Allah ataziweka kwa ajili yetu!
Tumche allah kwa kuzitii mamlaka alizotuwekea Allah.
Tubadilike kwanza sisi Watanzania wenyewe, tuache kudhulumiana wenyewe kwanza. Allah anatuletea viongozi wanaoendana na sisi jinsi tulivyo.
Tukiwa wajeuri, majabari, wakorofi basi atatupa kiongozi ambaye atakuwa zaidi yetu.
Tukiwa wezi kuibiana wenyewe kwa wenyewe Allah atatuletea mafisadi majizi makubwa zaidi yetu.
Tutendeane wema...
Tuhurumiane...
Tufanyiane uadilifu...
Tumche Allah...
#maishamema_baadayauchaguzi