Hahaha endelea kujidanganya dogo..
Unadhani Gates amekaa kihasarahasara, hayo ma ebola ma ukimwi, ma kansa na ma saratani na chanjo zao watu wanapewa wanakufa unadhani ni kwa bahati mbaya,
.
Endelea pia kuwaamini motivation speakers akina vunjabei wakiongea kwenye ma tv mnakua na muwashawasha kudhani mtakua kama wao kwa kudhani mtaanza na jeans moja then kiwanda cha jeans
Mtu mweusi bwana akishindwa kukifafanua kitu,atakiita uchawi,
Kansa,ebola,ukimwi,ni magonjwa,Dunia ya leo,sayansi ina uwezo wa kutengeneza ugonjwa,au kirusi kama silaha,au Ili kutengeneza pesa kwenye Tiba,
Lakini kusema kwamba watu wamekaa sehemu wakatengeneza ukimwi Ili uue watu,Ili baadae watu wapige pesa kwenye Tiba,hizi ni "conspiracy theory"zisizo na ushahidi.
Naweza nikaamini,nchi za Ulaya na US,wanaweza wakaanzisha vita,mashariki ya Kati,Ili wauze siraha,na viwanda vyao vipate mapato,
Kipindi Cha Mkapa,UK walituuzia rada kwa bei kubwa,Tena tukashinikizwa tuinunue,Ili kuokoa ajira za wazungu kwenye kiwanda huko UK,sasa hapa,aliyetolewa kafara kwa kukosa huduma ni mbongo,aliyetoa kafara Ili apate mali ni serikali ya TZ,au UK?
Hizi ni mbinu za kiuchumi,na kijasusi,
Wakenya walipocheza ujasusi wakaua kiwanda Cha general tyre,Ili wao wazalishe tairi,sisi tulikosa ajira,wao wakapata,hiyo ndio kafara?
Hakuna ushahidi Dangote,au Bill gate,alienda makaburini,akacheza ngoma usiku,akamtoa mwanae kafara,au akalala na mama yake,au dada Ili kupata mali!!
Tuambie Bakheresa kamtoa nani kafara?!!
Maana usichanganye social responsibility ya makampuni kutoa kwa jamii,na kutoa kafara kwa mizimu,
Hizi story Zenu za makafara huwa hazifiki mbezi beach,zinaishia Tandale,
Haya Mond alikuwa fukara choka mbaya,kamtoa nani kafara Kufika hapo,
Shida mkishindwa kuelezea mtu kafikaje hapo na kuwaacha chini,mnamchukia na kuzusha story,ohhh anatembea na mama yake,,au anatembea na Dada yake.
Na wewe tembea na Dada yako upate mali.
Akili chafu kabisa,
Nenda kasome historia ya kampuni ya Benz,MTU,MAN,Caterpillar,zilianzishwa 1890+kwa watu kufsnya kazi,sio kuwaza kama wanga.