Maisha bila Mungu yamekuwa ya amani na furaha

Tena Mungu huyu huyu wa Sasa amechachuka balaa ukifanya usiku Asubuhi anajibu.. Mkuu stay tuned Mungu hadhihakiwi.....utapata tukio na utahitaji msaada wake huku ukikiri uwepo wake.....#save my post. Au tubu.
 
Tena Mungu huyu huyu wa Sasa amechachuka balaa ukifanya usiku Asubuhi anajibu.. Mkuu stay tuned Mungu hadhihakiwi.....utapata tukio na utahitaji msaada wake huku ukikiri uwepo wake.....#save my post. Au tubu.
Hii ndio dhihaka yenyewe.
 
Hii ndio dhihaka yenyewe.
Sio mwandishi mzuri Nina fact ya ninachoo gea siyo Kwa kuhadithiwa Bali Kwa kushuhudia Kwa milango yangu yote mitano ya fahamu kama huamini uwepo wa Mungu kaa nacho moyoni . .. .
 
Reactions: 511
Hii ndio dhihaka yenyewe.
Tena Mungu huyu huyu wa Sasa amechachuka balaa ukifanya usiku Asubuhi anajibu.. Mkuu stay tuned Mungu hadhihakiwi.....utapata tukio na utahitaji msaada wake huku ukikiri uwepo wake.....#save my post. Au tubu.
Maneno kwenye rangi ya njano ndio nimesema ni dhihaka.
Unaposema Mungu huyu wa sasa kwani wako wangapi? Je wa zamani amezeeka amemrithisha huyo wa sasa?

Matendo 13:41
“ ‘Angalieni, enyi wenye dhihaka, mkastaajabu, mkaangamie, kwa maana nitatenda jambo wakati wenu ambalo hamtasadiki, hata kama mtu akiwaambia.’ ”

Tafakari mwenyewe kulingana na amani ya moyo wako kisha chukua hatua, wala usinijibu
 
Khaaa subiria dhahama
 
Ukweli ndio huo.....ni sanaa ktkt matumizi ya lugha sijatukana au dhihaka Bali kuutukuza ukuu na ukali wake.....Wacha complication..Mkuu.
 
Ukweli ndio huo.....ni sanaa ktkt matumizi ya lugha sijatukana au dhihaka Bali kuutukuza ukuu na ukali wake.....Wacha complication..Mkuu.
Ujumbe umeupata. Kila la heri
Kama umenitukana hapo umesema complication, basi jua umejisema mwenyewe.
 
1 kor 1 : 18
Rudi kundini ndugu hujachelewa, Tatizo Bado hujakutana na Yesu umekutana na wachungaji, Masheikh na wengine wanaofanana na hao ambavyo kwa vyovyote vile nao Bado ni wanadamu.
Mtafute Yesu sio dini / Mali n.k, siku ukimpata Yesu kwako binafsi ndio utanielewa Nini nnamaanisha.
Nakuombea siku Moja hili pendo na neema ya Bwana wetu Yesu kristo ikupate.
Tafakari njema.
 
Reactions: 511
Hoja ya Epicurus imefafanuliwa vizuri na Mtakatifu Augostino na Akwinasi katika hoja ya akili na utashi huru.

Hatahivyo, hoja hiyo imeangalia jambo moja tu la uovu katika kuhoji uwepo wa Mungu kama Anayejua yote, kama Mwenye uwezo wote, kama Mwenye upendo wote na kama Mwenye maarifa yote.

Lakini si ouvu tu peke yake. Kuna pia suala la kifo na hatima ya ulimwengu.

Je, kama binadamu asingetenda dhambi asingekufa?

Na je, dunia kabla ya kuingia dhambi, viumbe au vitu vya asili viliumbwa kuwepo milele?

Au je! Dunia yetu kabla ya dhambi Mungu aliiumba kuwepo milele au kwa muda?

Hatahivyo, pamoja na hayo yote, tunapimaje kuwa kutokea kwa uovu duniani kunaondoa ukweli kwamba kuna Mungu amabye ana uwezo wote, ana maarifa yote, ana jua yote, na ana upendo wote?

Kwa binadamu kuwa na upendo ni nini na kwa Mungu kuwa na upendo ni nini? Kwa binadamu kuwa na uwezo ni nini na kwa Mungu kuwa na uwezo ni nini? Kwa binadamu kujua yote maana yake ni nini na kwa Mungu kujua yote maana yake ni nini?

Kuna mambo mengi ya kuangalia, kujifunza na kujua ikiwa ni pamoja na kujua huyo Mungu.

Kwa hiyo juu ya uovu kuwezekana duniani na ukweli kwamba Mungu ana uwezo wote, ni Mwenye upendo wote, ana maarifa yote, ana jua yote bado ni mambo ambayo hayajajulikana vizuri.
 
Umeandika mengi, lakini nichukue kimoja cha kwanza tu ili tukimalize hicho kabla ya kwenda kwingine.

Hoja ya Agustino na Aakwinasi kuhusu utashi huru, ni hoja mufilisi.

Na kwa kweli, ukiisoma kwa makini hoja ya Epicurus, utaliona hili.

Watu hatuna utashi huru kama wanavyodai Agustino na Akwinasi. Hatuna hata uamuzi tuzaliwe au tusizaliwe. Hatuamui tuzaliwe na nani, wapi, lini, hatuchagui vinasaba tutakavyorithi. Haya ni mambo yanayoamua kwa kiasi kukubwa maisha yetu yatakuwaje.

Utashi huru ni njozi tu. Pia, utashi huru una contradict sifa ya Mungu kujua yote. Mtu kuwa na utashi huru maana yake ana uamuzi wa mwisho kuamua atafanya nini, Mungu akishajua tu mtu atafanya nini, maana yake ni kwamba mtu hana utashi huru.

Kwa maneno mwingine, ama mtu ana utashi huru na Mungu hana ujuzi wote, ama Mungu ana ujuzi wote na watu hawana utashi huru, mawili haya ni "mutually exclusive".

Ninaiweka hoja ya Epicurus, na majibu yake, likiwamo jibu la utashi huru, na jinsi majibu yake yote yasivyokidhi kimantiki, kwa njia ya picha ili nieleweke vizuri zaidi.

 
Huyo Mungu mwenyewe huwezi kuthibitisha kuwa yupo.

Ukibisha, thibitisha Mungu yupo.

Hatuwezi tukajifungia kwenye box kwa ku-limit ufahamu wetu kwa vigezo vilivyowekwa na wanadamu wenzetu,

Safari bado sana na sayansi ni dynamic huko mbeleni yanaweza yakagundulika mambo mengine yenye sifa tofauti na haya tulioyazoae, na zika-setiwa stardards zingine kuweza kukitambua kitu.

Sasa mimi nafikili tusihitimishe jambo kwakua halina vigezo tulivyojiwekea sisi wenyewe, hii itakua ni sawasawa na kujifunga.

Mimi mwenyewe naona siwezi kukuthibitishia kwa vigezo unavyotaka wewe na pia isitoshe attitude yako yakuto/kutokua na amini/imani inaniwia mimi vigumu kutaka wewe binafsi u-experience hili suala... Kwasababu haya masuala ya kiroho huwa hayadili na kundi la watu, experience huwa inakua ni personal, kwakua kila mtu ana roho yake, na roho yako itakapopata nguvu/energy/mwanga/angaza kupitia harakati zako wewe mwenyewe ndani ya nafsi/ufahamu wako utahisi experience mpya na isiyo ya kawaida ambayo itajidhihirisha mpaka nje uku, utaona mabadiliko katika shughuli zako sometimes hata watu wanavyokuchukulia unaona wanakuja kwa gia tofauti na mwanzo hadi unajiuliza hivi hawa watu kimewakuta nini hadi wana-behave namna tofauti na mwanzo. (Inahitajika imani yako ku-experience nguvu ya Mungu)

Kwahiyo hili suala tusihitimishe kuwa MUNGU/NGUVU HAYUPO. BALI Kwa kua ni la kiroho basi liwe special case mpaka pale litakapo pata ufumbuzi.

Mbona mambo mengi tu hayajagunduliwa, na unaweza kuta siku litagunduliwa jambo likabadilisha taratibu na mienendo yetu na historian kwa ujumla yote yanawezekana.
 
Tatizo si tu kuwa huwezi kuthibitisha kuwa Mungu hayupo.

Ingekuwa tatizo ni hilo tu, ungeweza kusema kabisa, kimantiki, kwamba, kushindwa kuthibitisha kitu kuwapo si uthibitisho kwamba kitu hicho hakipo.

Na kwenye hoja hii, kimsingi, kimantiki, siwezi kukupinga. Hata kama naelewa umuhimu wa uthibitisho kama kitu pekee cha kujua kitu kipo au hakipo.

Tatizo lako ni kubwa zaidi ya kushindwa kuthibitishatu.

Tatizo lako kubwa zaidi ni kwamba, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kuwepo, kunaleta contradictions nyingi sana ambazo hazitatuliki, ambazo zinaonesha Mungu huyo hayupo.

Yani ni kama vile mtu akikuambia kwamba, katika Euclidean geometry kuna pembetatu ambayo hapo hapo ni duara.

Ukishindwa kuthibitisha kuwa katika Euclidean geometry kuna pembetatu ambayo hapohapo ni duara, una tatizo, lakini tatizo hilo si kubwa sana, si la msingi katika kuonesha kuwa pembetatu-duara hiyo haipo.

Kwa sababu, inawezekana pembetatu duara hiyo ipo, na wewe hujui tu kuthibitisha kwamba ipo.

Tatizo kubwa zaidi hapa linakuwa ukweli kwamba, kwa mantiki ya kanuni za Euclidean geometry, pembetatu haiwezi kuwa duara.

Kwa sababu.

1. Pembetatu ina pembe tatu, duara halina pembe.
2.Pembe tatu ina nyuzi 180, duara lina nyuzi 360
3. Pembetatu inaundwa na mistari mitatu minyoofu, duara haiundwi na mistari mitatu minyoofu.

Hapo tunaona pembetatu si duara na duara si pembetatu, anayesema kuna pembetatu ambayo ni duara inambidi aondoe hizi contradictions.

Na contradictions hizi zinatuonesha kuwa kusema pembetatu ni duara ni kusema uongo.

Vivyo hivyo, ukisema kuna Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote aliyeumba ulimwengu unaoweza kuwa na mabaya, umetengeneza contardiction kama ya kusema kuna pembetatu ambayo ni duara.

Na ukichunguza sana contradiction hii, unaona kuwa huyo Mungu hayupo, ni wa hadithi ya uongo ya kutungwa na watu tu.
 
Kutokujua jambo fulani haimaanishi kwamba ndio kuna Mungu.

Ninyi mmeenda direct na mmehitimisha kusema Mungu yupo, ilihali mmeshindwa kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu.

Sasa kama umeshindwa kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu, Utasemaje directly na kuhitimisha kwamba yupo?

Kwa nini unahitimisha kitu fulani kipo, ilhali huna hata uthibitisho wa uwepo wake?
 
Tena Mungu huyu huyu wa Sasa amechachuka balaa ukifanya usiku Asubuhi anajibu.. Mkuu stay tuned Mungu hadhihakiwi.....utapata tukio na utahitaji msaada wake huku ukikiri uwepo wake.....#save my post. Au tubu.
Tangu nimeandika huu uzi mbona hajibu kama kweli yupo. 🤣

Watu wakihoji tu kuhusu Miungu yenu mnakuja na vitisho!
 
Aisee maelezo yamenyooka nimekulewa vizuri kabisa... Mfano huo haujaleta contradiction yoyote katika kuthibitisha pembe tatu.

Sasa hiyo ni kwa mazingira/muktadha /settings za duniani.
============================

Mambo mengi yanayoonekana keujichanganyi ni kwasa tunayafikilia tukiwa na taswila ya hapa duniani, hili ndio tatizo letu. Maandiko yaliyo mengi ni mafunuo/kiduniani duniani inakua kama code... Muktadha wake ulikua katika ulimwengu wa ROHO.

Kwa upande wa imani huku kuna kitu kinaitwa ulimwengu wa roho ambako binadamu wa rohoni hakutani na hizi contradictions na ndiko uwezo wa Mungu kamili unadhihilika na ndiko mtu wa rohoni aliyeko duniani kwa msaada wa hili vazi la mwili, kwa imani akiomba chochote na kuamini basi amekipata...

Na kwa mtu asie wa rohoni anayeishi duniani pasipo imani/haamini anategemea vazi la mwili kama ndio kinga yake ya misukosuko duniani basi hatakua na msaada wowote bali ni kukabiliana na changamoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…