Hatuwezi tukajifungia kwenye box kwa ku-limit ufahamu wetu kwa vigezo vilivyowekwa na wanadamu wenzetu,
Safari bado sana na sayansi ni dynamic huko mbeleni yanaweza yakagundulika mambo mengine yenye sifa tofauti na haya tulioyazoae, na zika-setiwa stardards zingine kuweza kukitambua kitu.
Sasa mimi nafikili tusihitimishe jambo kwakua halina vigezo tulivyojiwekea sisi wenyewe, hii itakua ni sawasawa na kujifunga.
Mimi mwenyewe naona siwezi kukuthibitishia kwa vigezo unavyotaka wewe na pia isitoshe attitude yako yakuto/kutokua na amini/imani inaniwia mimi vigumu kutaka wewe binafsi u-experience hili suala... Kwasababu haya masuala ya kiroho huwa hayadili na kundi la watu, experience huwa inakua ni personal, kwakua kila mtu ana roho yake, na roho yako itakapopata nguvu/energy/mwanga/angaza kupitia harakati zako wewe mwenyewe ndani ya nafsi/ufahamu wako utahisi experience mpya na isiyo ya kawaida ambayo itajidhihirisha mpaka nje uku, utaona mabadiliko katika shughuli zako sometimes hata watu wanavyokuchukulia unaona wanakuja kwa gia tofauti na mwanzo hadi unajiuliza hivi hawa watu kimewakuta nini hadi wana-behave namna tofauti na mwanzo. (Inahitajika imani yako ku-experience nguvu ya Mungu)
Kwahiyo hili suala tusihitimishe kuwa MUNGU/NGUVU HAYUPO. BALI Kwa kua ni la kiroho basi liwe special case mpaka pale litakapo pata ufumbuzi.
Mbona mambo mengi tu hayajagunduliwa, na unaweza kuta siku litagunduliwa jambo likabadilisha taratibu na mienendo yetu na historian kwa ujumla yote yanawezekana.
Tatizo si tu kuwa huwezi kuthibitisha kuwa Mungu hayupo.
Ingekuwa tatizo ni hilo tu, ungeweza kusema kabisa, kimantiki, kwamba, kushindwa kuthibitisha kitu kuwapo si uthibitisho kwamba kitu hicho hakipo.
Na kwenye hoja hii, kimsingi, kimantiki, siwezi kukupinga. Hata kama naelewa umuhimu wa uthibitisho kama kitu pekee cha kujua kitu kipo au hakipo.
Tatizo lako ni kubwa zaidi ya kushindwa kuthibitishatu.
Tatizo lako kubwa zaidi ni kwamba, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kuwepo, kunaleta contradictions nyingi sana ambazo hazitatuliki, ambazo zinaonesha Mungu huyo hayupo.
Yani ni kama vile mtu akikuambia kwamba, katika Euclidean geometry kuna pembetatu ambayo hapo hapo ni duara.
Ukishindwa kuthibitisha kuwa katika Euclidean geometry kuna pembetatu ambayo hapohapo ni duara, una tatizo, lakini tatizo hilo si kubwa sana, si la msingi katika kuonesha kuwa pembetatu-duara hiyo haipo.
Kwa sababu, inawezekana pembetatu duara hiyo ipo, na wewe hujui tu kuthibitisha kwamba ipo.
Tatizo kubwa zaidi hapa linakuwa ukweli kwamba, kwa mantiki ya kanuni za Euclidean geometry, pembetatu haiwezi kuwa duara.
Kwa sababu.
1. Pembetatu ina pembe tatu, duara halina pembe.
2.Pembe tatu ina nyuzi 180, duara lina nyuzi 360
3. Pembetatu inaundwa na mistari mitatu minyoofu, duara haiundwi na mistari mitatu minyoofu.
Hapo tunaona pembetatu si duara na duara si pembetatu, anayesema kuna pembetatu ambayo ni duara inambidi aondoe hizi contradictions.
Na contradictions hizi zinatuonesha kuwa kusema pembetatu ni duara ni kusema uongo.
Vivyo hivyo, ukisema kuna Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote aliyeumba ulimwengu unaoweza kuwa na mabaya, umetengeneza contardiction kama ya kusema kuna pembetatu ambayo ni duara.
Na ukichunguza sana contradiction hii, unaona kuwa huyo Mungu hayupo, ni wa hadithi ya uongo ya kutungwa na watu tu.