Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Unafanya kosa la logical fallacy, logical non sequitur.Katika mambo ambayo nimejifunza kwenye kitabu cha Philosophy of Religion ni kwamba mafundisho ya dini na dini kwa ujumla yanaweza kuwafanya watu wengi kushindwa kutumia uwezo wao wa kufikiri na hivyo kushindwa kujua ukweli na kujua kuamua au kufanya mambo bila kukosea.
Hilo linaonekana katika vipindi mbalimbali jinsi jamii za wanadamu walivyokuwa wakiamini kuhusu Mungu na au hata sababu za kutokea kwa hali mbalimbali.
Unaweza ukasema kuwa mtu hana uwezo wa kufikiri unaomuezesha kujua na kujua kuamua au kufanya mambo bila kukosea.
Lakini ninataka kukuuliza swali.
Je! Suala la uvumbuzi wa maarifa ya kujua kutengeneza magari au mitambo, uwezo huo ni wa nani?
Na uvumbuzi huo au uwezo huo una makosa gani ukiacha makosa yanayotokana na matumizi?
Na Je! Kufikiri maana yake ni nini? Na kati ya mnyama na mtu, mwenye uwezo wa kufikiri ni nani?
Kwa kuwa tu, watu wana uwezo fulani wa kufanya maamuzi fulani kufanya mambo bila kukosea, hilo halina maana watu wananuwezo wa kufikiri na kufanya mambo bila kukosea.
Unaelewa tofauti?
Yani ni hivi, mtu akiweza kufanya hesabu za kujumlisha za namba 1 mpaka 10 bila kukosea, hilo halimaanishi kuwa mtu anaweza kufanya hesabu bila kukosea.
Wewe unachokosea ni kwamba, unaangalia mfano wa mtu anayeweza kufanya hesabu za kujumlisha namba 1 mpaka 1 bila kukosea, halafu unahitimisha kuwa huyu mtu ana uwezo wa kufanya hesabu bila kukosea.
Wakati kuna ma polynomial equation na ma Riemann Zeta Function hujayaangalia huko.
Ushaona unapokosea hapo?
This is a non sequitur logical fallacy.
This is a hasty generalization logical fallacy.