Maisha bila Mungu yamekuwa ya amani na furaha

Maisha bila Mungu yamekuwa ya amani na furaha

Ndio maana nikakwambia masuala ya Mungu ni next, advanced level/scope nyingine hauwezi kulinganisha na phenomena za duniani.

Ni sawa sawa na kufananisha maumivu ya kung'atwa na n'nge na maumivu ya mapenzi.

Mimi nina experience ya ninachokwambia... najaribu kufungua box utoke nje wewe unaishia kupinga.

Mimi ninafikiri uthibitisho ulio bora zaidi ni ule wa kushuhudia wewe mwenyewe na sio kuelekezwa, especially katika suala hili.

Mkuu, Don't take it for granted... IMANI ni msingi na ni gateway/portal kwa yale unayodhani hayapo au hayawezekani.

Note: Ushanielewa context ya ninachokizungumzia ila umeamua tu kusimama katika misimamo yako, that's good spirit though.

Kwa msimamo/na attitude uliyonayo nina uhakika hauwezi hata kuthubutu kujaribu imani inafanya kazi (hutakua na muda huo) labda nyakati zibadilike,

Hili nilijua kupitia ndoto hii. 👇👇👇

Mkuu mimi sina la ziada.
Nikikwambia mimi ndiye Mungu niliyeumba kila kitu na hilo suala liko nje ya uwezo wako kuelewa na kuamini, utakubali mimi ndiye Mungu?

Note: Ushanielewa context ya ninachokizungumzia ila umeamua tu kusimama katika misimamo yako, that's good spirit though.
 
Tatizo linaanza Watu wanapochanganya Nguvu Kuu ya asili(Mungu) na Dini.

Dini zinamapungufu kwasababu binadamu anaweza kuingiza mawazo yake.

Siku hizi dini inatumika kwa malengo mbalimbali sio kwaajiri ya Mungu tu.
Hujathibitisha kwamba Mungu yupo.

Kwa sababu hayupo.

Ukibisha, thibitisha Mungu yupo.
 
Nikikwambia mimi ndiye Mungu niliyeumba kila kitu na hilo suala liko nje ya uwezo wako kuelewa na kuamini, utakubali mimi ndiye Mungu?

Note: Ushanielewa context ya ninachokizungumzia ila umeamua tu kusimama katika misimamo yako, that's good spirit though.
Apo ni sawasawa na unawategea watu sanamu la mtu ili kuwatisha wasiibe mazao yako shambani.

Mimi sio naishia kuiamini tu bali napata na matokeo ya ninachokitaka.

Sasa wewe unaweza kutimiza matakwa yangu kupitia imani.
 
Roho ni nini?

Anza ku define hapo na uithibitishe ipo
Hili ndio tatizo ambalo upo nalo,
Mimi ni mwalimu wako, Na ndiye naelewa procedure ya namna ya kukufundisha

Yani ni hatua kwa hatua, Najua nianzie wapi niishie wapi ili wewe ufikie tamati ya kujua

Sasa maswali yako mengine majibu yake yapo mbele ya ufahamu ulionao kwa sasa, hivyo tulia nkufundishe

Nakuuliza tena upo tayari ?
 
Hili ndio tatizo ambalo upo nalo,
Mimi ni mwalimu wako, Na ndiye naelewa procedure ya namna ya kukufundisha
Mwalimu gani anaanza kufundisha kitu bila kutoa definition ya hicho kitu?

Utaanzaje kuzungumzia kitu bila kuki define kwanza na kutambua uwepo wake?

Ni sawa na uanze kujifunza chemistry bila ku define, What is chemistry?
Yani ni hatua kwa hatua, Najua nianzie wapi niishie wapi ili wewe ufikie tamati ya kujua
Hatua ya mwanzo kabisa ni kufafanua kitu,

kuki define ni nini?

kujua kipoje?

Na kipo kwa namna gani?
Sasa maswali yako mengine majibu yake yapo mbele ya ufahamu ulionao kwa sasa, hivyo tulia nkufundishe
Wewe unarukia kusema Mungu yupo, Roho ipo halafu huwezi hata kuthibitisha uwepo wa huyo mungu na roho.

Huoni kwamba unaelezea vitu ambavyo hata wewe mwenyewe huna ufahamu navyo?

Kwanza eleza ulifamu vipi na unathibitishaje kuna Mungu?

Ulifamu vipi na unathibitishaje kuna Roho?
Nakuuliza tena upo tayari ?
 
Huoni kwamba unaelezea vitu ambavyo hata wewe mwenyewe huna ufahamu navyo?
Una haraka sana mwanafunzi, Mimi mwalimu ndiye nliyeibua hoja ambayo nataka nkufundishe wewe

Sasa maswali yako kama "Roho ni nini" ni wajibu wangu nngekueleza bila hata wewe kuniuliza kwanza

Mwanafunzi una mihemko sana, Calm down kwanza
 
Una haraka sana mwanafunzi, Mimi mwalimu ndiye nliyeibua hoja ambayo nataka nkufundishe wewe
Kuibua hoja unaweza hata kuibua hoja ya uongo.

Ili tuhakikishe kwamba hoja yako ni ukweli lazima uithibitishe ipo.
Sasa maswali yako kama "Roho ni nini" ni wajibu wangu nngekueleza bila hata wewe kuniuliza kwanza
Eleza roho ni nini?

Ulijuaje ipo?

Na unathibitishaje ipo?

Na si mawazo yako ya kufikirika tu.
Mwanafunzi una mihemko sana, Calm down kwanza
 
Kuibua hoja unaweza hata kuibua hoja ya uongo.

Ili tuhakikishe kwamba hoja yako ni ukweli lazima uithibitishe ipo.

Eleza roho ni nini?

Ulijuaje ipo?

Na unathibitishaje ipo?

Na si mawazo yako ya kufikirika tu.
Sasa hapa itakua ni kama u unanihoji, Na sio kukufundisha

Anyways, Roho ni umbile lisiloonekana ambalo lipo pamoja au ndani ya mwili wa kiumbe hai
 
Sasa hapa itakua ni kama u unanihoji, Na sio kukufundisha
Assume, Mimi nimeibua hoja kwako nikaanza kukueleza kwamba kuna Dragons 🐉 watemao moto🔥 midomoni mwao.

Halafu wewe ukataka kujua, Je hao Dragons wapoje? wanafananaje? Walitoka wapi? Na Wako wapi?

Halafu mimi nikashindwa kukuthibitishia wewe, uwepo wa hao Dragons ninaodai wapo.

Na pia nikashindwa kukuelezea hao Dragons walipo, walitoka wapi na wako wapi.

Je wewe utakubali tu kwamba Dragons watemao moto midomoni mwao wapo kwa vile tu, Mimi nimekwambia hivyo?

Au utataka uthibitisho wa hao Dragons na wewe u prove na uwaone kweli?
Anyways, Roho ni umbile lisiloonekana ambalo lipo pamoja au ndani ya mwili wa kiumbe hai
Kama Roho ni umbile lisilo onekana, Wewe uliliona wapi na ulijuaje lipo?

Uli liona wapi hilo umbile "Roho" ndani ya mwili wa binadamu ukajua lipo?

Huoni kwamba unaelezea kitu ambacho hata wewe mwenyewe hukijui na wala hujawahi kukiona?

Ila unadai kipo tu, Bila ushahidi wowote ule?

Surgery mbalimbali na upasuaji unafanyika kwenye mwili wa binadamu na viumbe wengine,

Na madaktari hawajawahi kukuta au kuona hilo umbile "Roho" popote pale ndani ya mwili wa binadamu au kiumbe yeyote yule.

Huoni kwamba hiyo Roho, ni fiction tu?
 
Apo ni sawasawa na unawategea watu sanamu la mtu ili kuwatisha wasiibe mazao yako shambani.

Mimi sio naishia kuiamini tu bali napata na matokeo ya ninachokitaka.

Sasa wewe unaweza kutimiza matakwa yangu kupitia imani.
Sasa na wewe unaposema mambo ya imani ni next level kwa nini usiwe unawategea watu sanamu la mtu ili kuwatisha wasiibe mazao yako shambani?

Nimekwambia thibitisha Mungu yupo.

Mpaka sasa hujathibitisha.

Kwa sababu hayupo.

Ukibisha, thibitisha Mungu yupo.
 
Huoni kwamba unaelezea kitu ambacho hata wewe mwenyewe hukijui na wala hujawahi kukiona?
Unauliza swali ambalo unajipachikia majibu wewe mwenyewe tena, Kwanini usisubiri ujibiwe au ufundishwe ndipo uje na haya majibu yako uchwara ?

Nlishakwambia haya ni maarifa pia, Sasa kama ni maarifa ukianza kufafananisha na mifano ya hadithi ambazo hazieleweki unategemea utapata majibu ?

Unaleta ujuaji wakati unataka kueleweshwa utaelewa vipi sasa ?
 
Sehemu ya maandishi yako umethibitisha kuwa Mungu yupo ..rudia Tena kuopitia andiko lako kusoma tena
 
Unauliza swali ambalo unajipachikia majibu wewe mwenyewe tena, Kwanini usisubiri ujibiwe au ufundishwe ndipo uje na haya majibu yako uchwara ?
Hujajibu na hujathibitisha Mungu yupo.

Hujajibu na hujathibitisha Roho ipo.

Mpaka sasa unazunguka zunguka tu, you are just meandering.
Nlishakwambia haya ni maarifa pia, Sasa kama ni maarifa ukianza kufafananisha na mifano ya hadithi ambazo hazieleweki unategemea utapata majibu ?
Maarifa gani yasiyo na uthibitisho?

Hujathibitisha Mungu yupo, Hujathibitisha roho ipo.

Una niletea hadithi za uwepo wa Mungu na roho ambao kuwathibitishia huwezi na umeshindwa.
Unaleta ujuaji wakati unataka kueleweshwa utaelewa vipi sasa ?
Unaleta hadithi za uwepo wa Mungu na roho ambazo hata wewe mwenyewe, Huzijui na mpaka sasa umeshindwa kuthibitisha.

Unaruka ruka tu.
 
Maarifa gani yasiyo na uthibitisho?
Ebu ngoja nkuulize swali, Huwa unaota ndoto ? Nadhani ni ndio

Mfano mimi huwa sioti ndoto, Na nahitaji unithibitishie kuwa huwa unaota yaani kuna ndoto unaweza kunithibitishia ?
 
Ebu ngoja nkuulize swali, Huwa unaota ndoto ? Nadhani ni ndio
Hapana Sioti.

Mada inahusu Mungu na Roho.

Thibitisha kwanza wapo, Acha kurukia vitu vingine.

Hujajibu na hujathibitisha Mungu yupo.

Hujajibu na hujathibitisha Roho ipo.

Unarukia vitu vingine.
Mfano mimi huwa sioti ndoto, Na nahitaji unithibitishie kuwa huwa unaota yaani kuna ndoto unaweza kunithibitishia ?
 
Hapana Sioti.

Mada inahusu Mungu na Roho.

Thibitisha kwanza wapo, Acha kurukia vitu vingine.

Hujajibu na hujathibitisha Mungu yupo.

Hujajibu na hujathibitisha Roho ipo.

Unarukia vitu vingine.
Acha ujinga kijana, Bado nipo kwenye mada hii hii

Ila wewe kutoa mifano ya dragons hapa unaona ni sawa, Mimi nkitoa mfano wa ndoto unaona sio sawa ?

Umeona ni mtego umeona ukwepe
 
Hapana Sioti.

Mada inahusu Mungu na Roho.

Thibitisha kwanza wapo, Acha kurukia vitu vingine.

Hujajibu na hujathibitisha Mungu yupo.

Hujajibu na hujathibitisha Roho ipo.

Unarukia vitu vingine.
Uwepo wa Mungu unatambulika "kwanza" na mtu binafsi,
Swala linalohusu Roho vivyo hivyo ni jambo binafsi ambalo mtu mmoja mmoja ana experience

Mimi ambaye tayari natambua na nna experience kuhusu haya maarifa kazi yangu ni kukupa maarifa ya namna ya wewe kuexperience wewe mwenyewe,

Yani ujithibitishie wewe mwenyewe ukiwa peke yako, Baadae ndio tutakuwa wamoja kwenye kutambua uwepo wa maswala kama haya kwasababu wote tunakua tume experience hali jinsi ilivyo na mambo jinsi yalivyo
 
Back
Top Bottom