Maisha halisi nchini Marekani

Maisha halisi nchini Marekani

Umemwambia yeye ni blue collar, anatumikishwa na kunyonywa na Wazungu. Na ndio perspective yako hiyo. Na mimi nakwambia blue na white collar wote wana umuhimu wao duniani. Dunia bila blue collar isingekuwa dunia. Nani angefanya blue collar jobs kama wote wangekuwa white collar kama mimi? Jifunze ku-appreciate functions za wengine.
Nimekupa perspective out of personal experience. Hayo mambo y dharau umeingiza wewe.
 
Mimi nimekaa Marekani mji wa Washington. Ubaya wa Marekani hakuna undugu kila mtu kivyake kiutafutaji. Maisha ya Marekani ni magumu sana kwa kiingereza tunaita hand to mouth. Kwa gharama ya $600 kwa mwezi naona mtu huyo anapata mateso makubwa. Kama alivyosema kuwa anaweka akiba ya $4500 kwa mwezi. Kwa Afrika ukiwa unajishughulisha hicho kiasi ni kidogo kwa mfanyabiashara wa Afrika. Kinachotuharibu hapa Afrika hatuna utaratibu mzuri wa maisha. Familia tegemezi za afrika huwezi linganisha na familia ya America ya mtu mmoja, mkewe na mtoto. Nawashauri hapa kwetu Afrika kuna fursa nyingi sana kuliko America ambapo hata usingizi hupati kwa kudandia kazi za kuhama hama kwa siku.
 
Umemwambia yeye ni blue collar, anatumikishwa na kunyonywa na Wazungu. Na ndio perspective yako hiyo. Na mimi nakwambia blue na white collar wote wana umuhimu wao duniani. Dunia bila blue collar isingekuwa dunia. Nani angefanya blue collar jobs kama wote wangekuwa white collar kama mimi? Jifunze ku-appreciate functions za wengine.
Wewe umewahi fanya blue collar work marekani? Kwa taarifa yako, blue collar workers with stable employment make up the bulk of the middle class in the US. Sasa wewe hata US hujakanyaga unaanza ubishi wa kijinga. Jamaa kasema amefanya kazi States tofauti, sasa hapo maana yake hana permanent employer.
 
Habari JF

leo Katika mada yangu kichwa tajwa hapo juu, Ningependa nishare nanyi Uzoefu wangu wa maisha ya marekani, maana nimeona watu wengi sana wakijadili namna watu wanavyoishi nje, ajabu kati ya mia, tano tu ndo wanaelewa maisha halisi ya marekani.

Licha mimi huwa sipendi kuishi Marekani, lakini fursa zilizopo ndo zinatufanya tuelendelee kunganagia haya maisha, ndomana maisha yangu ya uwekezaji Yapo africa lakini utafutaji ni marekani kwa vile tu sijafikia malengo yangu ya maisha.

Miaka 6 ndani ya nchi ya marekani, ninaishi kwa Green card, nina ruhusiwa sasa kuomba uraia lakini mimi kwangu huwa si kipaumbele, maana nina uwezo wa kutoa na kuingia na kukaa nje ya marekani muda wa miezi sita.

Nimeishi majimbo na kufanya kazi kampuni tofauti tofauti, Mara nyingi nafanya hivyo tu ili kujifunza maisha halisi ya marekani. Mwaka jana nimefanya kampani saba na kuishi majimbo matatu. kufanya kazi marekani huwa nafanya tu kukaa bila kazi. nilichokifanya miaka minne ya marekani niliweka nguvu kuwekeza nyumbani jambo ambalo nilifanikiwa na kunipa huakika wa kuishi hapa bila kuwa na kazi.

Katika Harakati zangu za kucompare africa na marekani sehemu nzuri ya kuishi, niligundua africa kinachotufelisha ni uchumi ila ukiwa na pesa napendekeza kuishi afrca badala ya marekani. Marekani ni sehemu tu ya utafutaji ikiwa africa huna cha kupoteza(maono yangu)

MAZURI YA MAREKANI.
naipenda nchi ya marekani ni nchi ambayo inamuwesha kila mtu bila kujali nchi uliotokea kufanya lolote na ukafanikiwa, tofauti na nchi kama vile urusi, china. marekani ni nchi ya kila mtu kufanya anachoweza yaani nchi ya fursa. ukitaka kuwa doctoe, nurse nk.. hata kama umefeli elimu katika nchi yako marekani kuna njia nyingi za kukuwezesha ukarudi shule na ukatimiza ndoto zako.

Ikiwa ndo mara ya kwanza unaingia marekani, Kitu cha kwanza jifunze sana kingereza, kitu cha pili somea fani yeyote, cha tatu kuchuka Credit card. ukiwa na hayo matatu nchi ya marekani umemaliza mambo mengine yanakuja, na hayo yote inawezekana kufanyika kwa mtu yeyote anaishi marekani kihalali.

kazi na makazi, siwezi kushauri kuishi kwenye miji kama Chicago, New york, washington nk.. mara nyingi miji hii kazi zake ni professional. tena ina gharama kubwa ya rent. badala yake nenda kwenye majimbo kama dakota, kenctuky , mara nyingi ni kazi za viwanda au Entry job alafu rent iko chini.

Watu wengi kutoka nje ya marekani wanafanya ENRTY JOBS kutokana na lugha kuwa ngumu alafu pesa zinawachanganya hawataki kusoma.

Marekani kuna uraisi wa kumiliki nyumba gari na kufanya biashara unayotaka(biashara ya import chakula na kuuza kwenye maduka ya africa inalipa). hata kama huna huwezo huo. unaweza kutumia CREDIT yako na kupata nyumba, gari, au pesa baadae utalipa taratibu. kikubwa deal na Scores zako kuwa HIGH, na Credit ni kitu muhimu sana marekani.

Kazi ni nyingi na unaruhususiwa kufanya kazi masaa yote unayotaka hata kuwa na zaidi zaidi ya kumi, Mfano mimi nina ENTRY JOBS ndo always huwa nafanya kazi za aina hii, Kazi yangu ya Sasa Ni HMI CLASS tunatengenza class, nafanya kazi masaa 8 kila siku nalipwa $21 kwa saa na overtime $27, awali ilikuwa GE Appliance nilikuwa nalipwa $19, Before GE ilikuwa Fedex nilikuwa nalipwa $19.50, kabla ya Fedex ilikuwa Amazon $20.

Now kazi yangu ya sasa nafanya masaa ninayotaka nikisema kwamba nataka nipate $5000 mwezi huu inapatikana na gharama zangu za maisha ya marekani hazifiki hata $600(bills). So hapo nina kitu cha kufanya tayari africa. Imagine miez 12 ya kazi nikiruid africa huwez kusema tunarudi tumechoka.

Fursa nyingine ambayo kwangu huwa naona ni muhumu sana hapa marekani ni technology, Iphone ilipo marekani sio iliopo africa, chrome inavyofanya kazi marekani ni tofauti kabisa na africa, System za simu na Feature baadhi za Social Media ziko tofauti. kuna software kama vile Stripe huwezi kujiunga ikiwa unaishi africa, so mambo kama hayo ni muhimu sana na ni fursa kubwa.
Hat banl system ni tofauti kabisa zinavyotumika africa.

So kuishi marekani kuna fursa ya kuelimika pia, saivi ukimwabia banker maswala ya wallet pay, wireless pay, finger pay haya ni mambo mageni kwake au anasikiaga tu, ila wewe unaelimika kutoka na fursa ya mazingira unayoishi

ITAENDELEA.......
NO PM
Nasubiri muendelezo
 
Ninachoweza kukugurentee ni kwamba Bongo watu wapo smart kichwani lakini maisha yanawachapa, hili haliwezi kukuta Marekani.

Huwezi kuwa Marekani eti unaamka huna mia uende ukamboom mtu.

Ninaamini kwa dhati kabisa huko mbinguni Wabongo hawaendi motoni, moto wameshaupata hapahapa duniani.
Sawa ila sema tu huko motoni hao wabongo lazima waingie kwasababu ya utapeli wao na unafiki waliojawa nao
 
Inawezekana ukalipwa hiyo hela, lkn inaonyesha wewe ni blue collar worker. Ukiona blue collar employee analipwa pesa kama hiyo ujue it comes with a huge downside as far as health, general well-being and quality of life. Siyo kama unakaa kwenye desk lako siku nzima ukiwa kazini. Wazungu watakuwa wanahakikisha they get every dime’s worth out of your paycheck. Kama ni kweli, utakuwa unapelekeshwa sana kazini kwa mshahara huo. Na kama unabadilisha kazi mara kwa mara, and state to state, basi utakuwa private contractor. Unapewa kazi kwa temporary contracts. Contract ikimalizika unakuwa jobless, unless ume apply kazi sehemu nyingine before end of current contract.

Nabishana na mtu ambae hajuwi chochote. bora ukae kimya tu kuliko kujifanya unajua sana.
 
Mimi nimekaa Marekani mji wa Washington. Ubaya wa Marekani hakuna undugu kila mtu kivyake kiutafutaji. Maisha ya Marekani ni magumu sana kwa kiingereza tunaita hand to mouth. Kwa gharama ya $600 kwa mwezi naona mtu huyo anapata mateso makubwa. Kama alivyosema kuwa anaweka akiba ya $4500 kwa mwezi. Kwa Afrika ukiwa unajishughulisha hicho kiasi ni kidogo kwa mfanyabiashara wa Afrika. Kinachotuharibu hapa Afrika hatuna utaratibu mzuri wa maisha. Familia tegemezi za afrika huwezi linganisha na familia ya America ya mtu mmoja, mkewe na mtoto. Nawashauri hapa kwetu Afrika kuna fursa nyingi sana kuliko America ambapo hata usingizi hupati kwa kudandia kazi za kuhama hama kwa siku.

hujawahi kuishi marekani mkuu.
 
Wewe umewahi fanya blue collar work marekani? Kwa taarifa yako, blue collar workers with stable employment make up the bulk of the middle class in the US. Sasa wewe hata US hujakanyaga unaanza ubishi wa kijinga. Jamaa kasema amefanya kazi States tofauti, sasa hapo maana yake hana permanent employer.

Nyamaza mkuu, huna unachokijua.but sitak tubishane
 
Unazidi kutengeza mada yako. Anzisha uzi wako basi. Kuwa na permanent employment haikuwa dhumuni la mtoa mada. Bado unajitengenezea maswali yako kwenye mtihani na kuyajibu. Na wala mtoa mada hakutaka kuonyesha watu kuwa amefika Marekani. Mtoa mada ana-share opportunities nje ya Tanzania na kufungua macho wanajukwaa. Wee kwa akili yako mbovu unamwonyesha eti anafanya blue collar job, kwa hiyo ana-toil. That was not the point of his/her post. White or blue collar, toil or not, ever been to the US or not, stable or not, permanent or temporary - are all irrelevant to the post.

Kama una white collar job, shukuru Mungu. Usijione wee mjanja sana kwa kuwa na white collar job. Dunia inawahitaji wote - white collar na blue collar workers, temporary or permanent. I have a white collar job (siyo lazima iwe Marekani, dunia ni kubwa, Marekani ni kasehemu kadogo tu kwenye planet hii). Dunia ina zaidi ya watu bil 7, wote hawawezi kuwa US na wote hawawezi kuwa white collar. I earn much higher than the median wages in the US lakini naheshimu watu wanaofanya blue collar jobs akiwemo mtoa mada hii.
Wewe umewahi fanya blue collar work marekani? Kwa taarifa yako, blue collar workers with stable employment make up the bulk of the middle class in the US. Sasa wewe hata US hujakanyaga unaanza ubishi wa kijinga. Jamaa kasema amefanya kazi States tofauti, sasa hapo maana yake hana permanent employer.
 
Ni uvivu tu, ndio maana utakuta mtu anapiga debe apewe mia mbili mia mbili siku nzima wakati kijijini kwao kuna mapori ambayo anaweza tumia nguvu hizohizo kufyeka na kuanzisha mashamba..
Nani alikwambia subsistence agriculture inalipa?

Maisha ya kilimo nayafahamu nje ndani. Nimelima na nimefanya research za kilimo.

Commercial farming ndo kilimo kinalipa Tz na Duniani. Subsistence Farming haijawahi mlipa mkulima milele.

Ukifuata njia zote za kisasa za kilimo, gharama ni kubwa kuliko mapato. Hutakaa uone faida kwenye kilimo.
 
Usichokijua labda ni kwamba hao mabiliobea wengi pesa wanatafutia hukohuko mikoani unakokudharau..

Mfano mdogo tu, wabunge asilimia kubwa wakipata Ubunge wanahamia Dar. Hata matajiri pia, wengi wanavuna pesa mikoani na kuamia Dar. Ila bado msingi wa shughuli zao wanazifanya hukohuko mikoani..
Ndio maana nasema wanakuja kuchuma na kuondoka.

Mitaji mikubwa ipo concentrated in Dar. Nyie ndo mnakuwa mawakala wa kuwaibia wanyonge wenzenu.

Nimetembea mikoa yote kasoro Mara na Zanzibar. Hizo fursa hazipo na hazitakaa ziwepo.

Miundombinu bora ipo mijini, huduma bora za afya na elimu zipo mijini.

Mpaka leo wakazi wa Ifakara huko hawana barabara, unakaza kichwa uende ukalime mpunga kisa fursa ipo.

Utaishia kuuza mashineni tajiri atoke Dar akauze mara 2. Unadhani nani amefaidika hapo.?
 
Back
Top Bottom