Maisha halisi nchini Marekani

Maisha halisi nchini Marekani

Hivi mbona mmoja wenu huko akifariki huko Kusafirisha Mwili tu huwa ni Shughuli Pevu.?
Bakuli La michango linatuhusu mpaka huku Kwa Mtogole.!
Halafu Mkifiwa na Mzazi Utasikia Mtoto Kashindwa Nauli Kuja Kumzika Mzazi Wake..! Hivi Diaspora Tuelezeni shida nini?
Mi mwenyewe nilitaka Kuja kuwa Diaspora ila ninachokishuhudia Kinachowatokea huko nimeghairi..!

Katika Diaspora 20 ni Wawili au Watatu ndo Wanatoboa.
[emoji23]
 
Nimezaliwa na kukulia Dar.

Huko kijijini naenda kuzika.

Wakenya wanaenda Njombe kuchukua parachichi wanaenda kuuza dubai. Bado unasema hawaji kuchuma?

Mbao, Mahindi wanapeleka kwao vingine wana export.

Hakuna foreigner anakuja kukuendeleza wewe.

Nyie wa vijijini mnakuwa mawakala wa kuwaibia watanzania wenzenu.
Wabongo tunapaswa kufahamu kuwa, tupate exposure yakuja kuwekeza bongo ila tusijidanganye kuwa mifumo ya nchi za magharibi zinaweza kusaidia kuvimba ugenini.
 
Hivi mbona mmoja wenu huko akifariki huko Kusafirisha Mwili tu huwa ni Shughuli Pevu.?
Bakuli La michango linatuhusu mpaka huku Kwa Mtogole.!
Halafu Mkifiwa na Mzazi Utasikia Mtoto Kashindwa Nauli Kuja Kumzika Mzazi Wake..! Hivi Diaspora Tuelezeni shida nini?
Mi mwenyewe nilitaka Kuja kuwa Diaspora ila ninachokishuhudia Kinachowatokea huko nimeghairi..!

Katika Diaspora 20 ni Wawili au Watatu ndo Wanatoboa.

Huwa inahuzunisha zaidi pale mtu anapoishi amerika miaka 15 hadi 20 hajatoboa, halafu ikatokea amerudi bongo kuishi. Yaani huwa wanachanganyikiwa nyie acheni
 
Halafu Mkifiwa na Mzazi Utasikia Mtoto Kashindwa Nauli Kuja Kumzika Mzazi Wake..! Hivi Diaspora Tuelezeni shida nini?
Mi mwenyewe nilitaka Kuja kuwa Diaspora ila ninachokishuhudia Kinachowatokea huko nimeghairi..!
Nauli sio tatizo.

Ukweli ni kwamba watu hawana Makaratasi, wanaogopa wakitoka hawatoweza kurudi/kuingia tena
 
Mikoani hakuna fursa zozote acheni kujazana upumbavu kichwani.

Vijana wanaona bora wawe machinga dar kuliko huko unakoona kwenye fursa.
Mfano hai ni mimi, hunihamishi mkoani

Tena kimkoa changu cha juzi tu 2012
 
Huwa inahuzunisha zaidi pale mtu anapoishi amerika miaka 15 hadi 20 hajatoboa, halafu ikatokea amerudi bongo kuishi. Yaani huwa wanachanganyikiwa nyie acheni

Mtu ambae anaishi Marekani ni watu wawili tofauti.
mfano: Teknology, Education, Laguage, life system. connection.

Inawezekana mtu anaishi hana bitambulisho, huyo siwez kumjadili.
 
Inawezekana ukalipwa hiyo hela, lkn inaonyesha wewe ni blue collar worker. Ukiona blue collar employee analipwa pesa kama hiyo ujue it comes with a huge downside as far as health, general well-being and quality of life. Siyo kama unakaa kwenye desk lako siku nzima ukiwa kazini. Wazungu watakuwa wanahakikisha they get every dime’s worth out of your paycheck. Kama ni kweli, utakuwa unapelekeshwa sana kazini kwa mshahara huo. Na kama unabadilisha kazi mara kwa mara, and state to state, basi utakuwa private contractor. Unapewa kazi kwa temporary contracts. Contract ikimalizika unakuwa jobless, unless ume apply kazi sehemu nyingine before end of current contract.
Aisee..
Wewe unaishi Marekani au uliwahi kuishi........umetisha mkuu
Anawapanga na Mr sule na kuwajibu na Matola
Sijaona hawa wawili wakipishana........
 
Mzee nimekusoma vizuri.Naomba unishauri mimi ni kijana ambaye nina degree ya usimamizi rasmali watu,nifanyeje ili niweze kuja kuhustle maisha huko US kwa kutumia hii taaluma yangu ili nitoboe fasta
Habari JF

leo Katika mada yangu kichwa tajwa hapo juu, Ningependa nishare nanyi Uzoefu wangu wa maisha ya marekani, maana nimeona watu wengi sana wakijadili namna watu wanavyoishi nje, ajabu kati ya mia, tano tu ndo wanaelewa maisha halisi ya marekani.

Licha mimi huwa sipendi kuishi Marekani, lakini fursa zilizopo ndo zinatufanya tuelendelee kunganagia haya maisha, ndomana maisha yangu ya uwekezaji Yapo africa lakini utafutaji ni marekani kwa vile tu sijafikia malengo yangu ya maisha.

Miaka 6 ndani ya nchi ya marekani, ninaishi kwa Green card, nina ruhusiwa sasa kuomba uraia lakini mimi kwangu huwa si kipaumbele, maana nina uwezo wa kutoa na kuingia na kukaa nje ya marekani muda wa miezi sita.

Nimeishi majimbo na kufanya kazi kampuni tofauti tofauti, Mara nyingi nafanya hivyo tu ili kujifunza maisha halisi ya marekani. Mwaka jana nimefanya kampani saba na kuishi majimbo matatu. kufanya kazi marekani huwa nafanya tu kukaa bila kazi. nilichokifanya miaka minne ya marekani niliweka nguvu kuwekeza nyumbani jambo ambalo nilifanikiwa na kunipa huakika wa kuishi hapa bila kuwa na kazi.

Katika Harakati zangu za kucompare africa na marekani sehemu nzuri ya kuishi, niligundua africa kinachotufelisha ni uchumi ila ukiwa na pesa napendekeza kuishi afrca badala ya marekani. Marekani ni sehemu tu ya utafutaji ikiwa africa huna cha kupoteza(maono yangu)

MAZURI YA MAREKANI.
naipenda nchi ya marekani ni nchi ambayo inamuwesha kila mtu bila kujali nchi uliotokea kufanya lolote na ukafanikiwa, tofauti na nchi kama vile urusi, china. marekani ni nchi ya kila mtu kufanya anachoweza yaani nchi ya fursa. ukitaka kuwa doctoe, nurse nk.. hata kama umefeli elimu katika nchi yako marekani kuna njia nyingi za kukuwezesha ukarudi shule na ukatimiza ndoto zako.

Ikiwa ndo mara ya kwanza unaingia marekani, Kitu cha kwanza jifunze sana kingereza, kitu cha pili somea fani yeyote, cha tatu kuchuka Credit card. ukiwa na hayo matatu nchi ya marekani umemaliza mambo mengine yanakuja, na hayo yote inawezekana kufanyika kwa mtu yeyote anaishi marekani kihalali.

kazi na makazi, siwezi kushauri kuishi kwenye miji kama Chicago, New york, washington nk.. mara nyingi miji hii kazi zake ni professional. tena ina gharama kubwa ya rent. badala yake nenda kwenye majimbo kama dakota, kenctuky , mara nyingi ni kazi za viwanda au Entry job alafu rent iko chini.

Watu wengi kutoka nje ya marekani wanafanya ENRTY JOBS kutokana na lugha kuwa ngumu alafu pesa zinawachanganya hawataki kusoma.

Marekani kuna uraisi wa kumiliki nyumba gari na kufanya biashara unayotaka(biashara ya import chakula na kuuza kwenye maduka ya africa inalipa). hata kama huna huwezo huo. unaweza kutumia CREDIT yako na kupata nyumba, gari, au pesa baadae utalipa taratibu. kikubwa deal na Scores zako kuwa HIGH, na Credit ni kitu muhimu sana marekani.

Kazi ni nyingi na unaruhususiwa kufanya kazi masaa yote unayotaka hata kuwa na zaidi zaidi ya kumi, Mfano mimi nina ENTRY JOBS ndo always huwa nafanya kazi za aina hii, Kazi yangu ya Sasa Ni HMI CLASS tunatengenza class, nafanya kazi masaa 8 kila siku nalipwa $21 kwa saa na overtime $27, awali ilikuwa GE Appliance nilikuwa nalipwa $19, Before GE ilikuwa Fedex nilikuwa nalipwa $19.50, kabla ya Fedex ilikuwa Amazon $20.

Now kazi yangu ya sasa nafanya masaa ninayotaka nikisema kwamba nataka nipate $5000 mwezi huu inapatikana na gharama zangu za maisha ya marekani hazifiki hata $600(bills). So hapo nina kitu cha kufanya tayari africa. Imagine miez 12 ya kazi nikiruid africa huwez kusema tunarudi tumechoka.

Fursa nyingine ambayo kwangu huwa naona ni muhumu sana hapa marekani ni technology, Iphone ilipo marekani sio iliopo africa, chrome inavyofanya kazi marekani ni tofauti kabisa na africa, System za simu na Feature baadhi za Social Media ziko tofauti. kuna software kama vile Stripe huwezi kujiunga ikiwa unaishi africa, so mambo kama hayo ni muhimu sana na ni fursa kubwa.
Hat banl system ni tofauti kabisa zinavyotumika africa.

So kuishi marekani kuna fursa ya kuelimika pia, saivi ukimwabia banker maswala ya wallet pay, wireless pay, finger pay haya ni mambo mageni kwake au anasikiaga tu, ila wewe unaelimika kutoka na fursa ya mazingira unayoishi

ITAENDELEA.......
NO PM
 
Aisee..
Wewe unaishi Marekani au uliwahi kuishi........umetisha mkuu
Anawapanga na Mr sule na kuwajibu na Matola
Sijaona hawa wawili wakipishana........

Huyo anaongea kitu ambacho haelewi, na haipendezi kubishana na mtu, hope nimeongea sababu za mimi kubadili kazi, nimeongea kwanini naama sana makazi, na nimemuonyesha check yangu ikionyesha tax na take home,istoshe nimemwambia nimefanya kazi amazon, fedx na GE. nenda google alafu angalia namna wanavyoajiri na sheria zao za kazi,

Sijaoenda kubishana nae. haina maana
 
Unazidi kutengeza mada yako. Anzisha uzi wako basi. Kuwa na permanent employment haikuwa dhumuni la mtoa mada. Bado unajitengenezea maswali yako kwenye mtihani na kuyajibu. Na wala mtoa mada hakutaka kuonyesha watu kuwa amefika Marekani. Mtoa mada ana-share opportunities nje ya Tanzania na kufungua macho wanajukwaa. Wee kwa akili yako mbovu unamwonyesha eti anafanya blue collar job, kwa hiyo ana-toil. That was not the point of his/her post. White or blue collar, toil or not, ever been to the US or not, stable or not, permanent or temporary - are all irrelevant to the post.

Kama una white collar job, shukuru Mungu. Usijione wee mjanja sana kwa kuwa na white collar job. Dunia inawahitaji wote - white collar na blue collar workers, temporary or permanent. I have a white collar job (siyo lazima iwe Marekani, dunia ni kubwa, Marekani ni kasehemu kadogo tu kwenye planet hii). Dunia ina zaidi ya watu bil 7, wote hawawezi kuwa US na wote hawawezi kuwa white collar. I earn much higher than the median wages in the US lakini naheshimu watu wanaofanya blue collar jobs akiwemo mtoa mada hii.

Nimefanya kazi amazon, nimefanya kazi fedex, na nimefanya kazi GE, hizi ni kampuni kubwa na kazi yake huwa ni permanent.nenda google uangalie hili.

Alafu nimeandika sababu ya mimi kwanini nataka kuhama kazi na kuishi states tofauti.

Jamaa anaandika asichi kijua
 
Ukimaliza kuandika yote nitag.
Masuala ya kusoma nusu nusu sipendi
 
Mimi nina uzoefu wa marekani tu, so sijuwi unaowazungumzia wewe ni wa wapi?
Alichoongelea ni kweli, sijui kama uko karibu na jumuiya yoyote ya WaTz unavyoishi sehemu mbalimbali. Ajue tofauti na wewe, kuna wengi tu ambao hawaishi Marekani kihalali, hivyo hawawezi kutoka, au niseme wakitoka, hawataweza kurudi tena, hivyo misiba huko nyumbani kwao inawapita.
Na kusafirisha miili ni gharama vile vile, lazima watu wachangishane.
 
Kusafirisha maiti maana yake unasafirisha mzigo human remaining body, sasa milioni 40 mlikuwa mnasafirisha mzigo gani? Au kuna wajanja walipiga hizo ela?
Maiti huhifadhiwa Kwa kufanyia embalming, hasa sinazobidi kusafirisha umbali mrefu, ili zisiharibike. Hapo na pia usafiri wenyewe, ndio gharama inapokuja. Na ndio, katika ndege, jeneza linachukuliwa kama mzigo, ni gharama kubwa kusafirisha mzigo.
 
Back
Top Bottom