Maisha halisi ya Watanzania waishio hapa Afrika Kusini

Ontan katika uhalisia wake...ushanidaka mkuu nikiona bandiko lako tu lazima nilipitie....makes clap!
 
Stippers ninao wakubali ni wale wa the summit,wengine wote tupa kule! Wabongo waliotusua wapo kibao pia ila ni wale wenye shughuli rasmi zinazofahamika.
Boss! Nakubaliana na wewe, sikatai kua hao wapo. Lkn tuwe wakweli SA si pa kuenda mzima mzima.

Mimi I'm being honest, kuna sehemu nilienda panaitwa White House hotel, mtaa wa Main street, Town. Kuna dogo ni mwafrika kusini pure, nilikutana nae ana degree ya metallurgy engineering na bado alikua ni bar waiter.

Alikua anatamani sana kuzamia kuja Bongo, alinambia ana rafiki zake wamekuja Bongo na wakala mashavu migodini. Sasa, nafikiria mwenyeji anahenya hivi, vipi kuhusu mgeni anayekuja huku hajui kuzungumza Tswana, Zulu, Khoxa, Ndebele, Swati wala Tshonga na hata kingereza chenyewe mtu hawezi kuongea dakika 3 bila kunywa maji.

Huko ni pagumu sana km hauna pa kuanzia.
 
KATIKA HILI HAKUTUTENDEA HAKI HUYU MHESHIMIWA, ALIYO YA ZUNGUMZA MENGI NI SAHIHI ILA SI KWAMBA WOTE TULIO HAPA TUPO HIVYO INAWEZA LIKAWA NI KOSA LA MWENYEJI WAKO AU NI MAKUSUDI TU! 0733318248 TUWASILIANE UJE NYUMBANI TAFADHALI.
Unaishi wapi boss, weekend nakuja Honey Dew kuna ishu nafata.
 
Salute!

Nakumbuka mara yangu ya kwanza kuingia Afrika Kusini ilikuwa mwaka 2015, nikiwa chuo mwaka wa 2. Kuanzia hapo safari za kwenda huko Bondeni zikawa ni za mara kwa mara. View attachment 510219

Lkn kwa bahati mbaya, mara nyingi nilivyokua naenda huko sikuwa na muda wa kutosha sana kuzunguka na kuiona Afrika kusini katika 3 dimensions. Mara kadhaa nilikua naenda Johannesburg na kuishi sehemu 1 bila kupata fursa ya kuzama downtown, na maeneo niliyokua nafikia ni yale ambayo hayana purukushani kama Sandton, Roodport, Midrand na Melrose Arch. Na hata muda ulikua very much limited.View attachment 510225Sandton City Shopping centre.

Tarehe 11 April nikaja hapa Afrika Kusini kwa ajili ya shughuli zangu kadhaa, safari hii ambapo nimemaliza chuo na nipo huru, basi nikaplan nikae hapa kwa muda mrefu zaidi hadi May 23. Na moja ya vitu vilivyonisukuma kukaa huku muda mrefu ni kujua hali ya maisha ya Watanzania wenzangu wa hapa, nikiamini kua kwa namna 1 ama nyingine ningeweza kujifunza mbinu kadhaa za kupambana na haya maisha.View attachment 510227Nikiwa safarini kuelekea Jozi.

[/B]Midrand

Siku niliyofika mwenyeji wangu alinichukua na kuniacha hotel hapo Midrand, kisha yeye akaelekea kwake Pretoria.View attachment 510231Mall of Africa - nahisi hii ni mall kubwa zaidi Afrika, maana nilipotea mara kadhaa humo ndani.

Nilivyosettle nikaenda restaurant ya jirani kupata dinner, sasa nilikua nimeingia instagram, nikawa natazama video ambayo ilikua ikiplay kwa kiswahili. Kuna jamaa kama meza 2 au 3 mbele yangu akawa ananitazama sana, nikagundua yule bwana anafahamu kiswahili, lkn sikuweza kuconfirm kama ni Mtanzania, Mkenya, Mkongo ama vipi. Akaondoka zake mimi nikabaki nakula, nilivyomaliza kula nikapata wazo la kubadili sim cards, hivyo nilihitaji kwenda kusajili line ya Telkom SA na Cell C.

Very coincidentally, nilivyoenda kusajili Cell C nikamkuta yule bwana pale. Hata alivyoona passport yangu bado Hakutaka kujitambulisha, lkn kadri alivyozidi kuongea kingereza cha kuunga unga ndipo nikagundua yule jamaa ni Mbongo. Sikukutana na Mtanzania mwingine hadi naondoka Midrand.

Pretoria

Muda wote nikiwa Midrand, trips zangu zilikua za kwenda Pretoria, sikuwahi kukutana na Mbongo yeyote hadi siku nilipoenda Tanzanian restaurant. Kwakeli hata watumiaji wa hile restaurant walikua ni waAfrika kusini, kuna mdingi mmoja alikuja na familia yake yeye na mkewe walikua wakiongea kiswahili, mzee alipaki E- class Mercedes benz na alikua na card nyeusi ya FNB Bank (hii card inamaanisha mtu ana zaidi ya Rand mil 1 kwa account).

Johannesburg

Baada ya siku kadhaa nikaenda kuishi Johannesburg maana hapo pia nilikua na shughuli nyingine ambayo inajitegemea tofauti na ile ya Pretoria, ikawa kuishi Jozi kungenirahisishia usafiri.View attachment 5102561 ya vivutio vya Jozi

Melrose Arch

View attachment 510246mtaa wa QwaQwa, Melrose.

Nilifika hapo Jozi hotel 1 inaitwa Blu Swan, siku ya Ijumaa jioni, nilikua nina weekend yote kurelax then j3 pilika pilika zianze. Nakumbuka siku ya Jumapili jioni, kukawa kama na majibizano, vyumba kadhaa kutoka chumbani kwangu. Sikutilia maanani sana.

Lkn baada km ya nusu saa majibizano yalizidi, nikasikia watu wakitembea kwa veranda, wakasimama karibu na mlango wangu. Nikategesha sikio vizuri, kuna mmoja alikua anajaribu kupiga simu, akaweka 'loud speaker'. Ile call ikaleta sauti ya mhudumu wa Voda "Namba unayoipigia haipatikani kwa sasa...". Nikajua fika huyu ni mbongo, nikatoka nje ya chumba changu ili nione nini kinaendelea.

Majibizano yale yalikua kati ya security wa hotel na huyo jamaa. Alikua kjn mdogo km wa miaka 25 hivi, kilichokua kikiendelea ni kua huyo dogo alikua anafukuzwa atoke pale kwa kushindwa kulipa pesa ya hotel.

Nikatumia uungwana, nikamuomba huyo security aachane nae mimi nitamlipia kwa siku hiyo. Nikaingia ndani nikachomoa Rand 780 nikamlipia huyo dogo. Baada ya kuSort out ile ishu, tukawa na majadiliano nae. Dogo alinambia vitu vya kusikitisha sana.

Ni kwamba, alikua ana siku 2 tangu aingie SA, alikua ametumwa na Boss wake. Kwa maelezo ya dogo ni kua Boss wake anaitwa Jumbe, ni mdau wa Ilala mtaa wa Arusha. Dogo alipewa mzigo aje nao, alikua na mabegi mawili. Kisha akifika SA atakutana na mwenyeji wake ambae atamwachia huo mzigo, baadae atapewa pesa ya kujikimu na nauli ya kurudi Bongo.

Dogo alivyokutana na mwenyeji wake, akamkabidhi mizigo, kisha akapelekwa hotel akalipiwa siku 1 then yule mwenyeji wake akaondoka mazima. Dogo wala hatambui nini kilikua kwenye hayo mabegi, ambayo alidai yalikua madogo ya mgongoni. Kutokana na njaa aliyokua nayo dogo, nikaamua tusile vyakula vya hotel, tukaenda kugonga vyakula local. Dereva akatuendesha hadi Carlton Centre.

Carlton Centre

Kusema kweli sijawahi kua na real experience ya Johannesburg hadi nilipofika hapa mitaa ya Carlton.View attachment 510254muonekano wa Carlton kutoka Jengo maarufu sana la Transet.

Tukafika Simmonds Street, tukapata mgahawa tukaagiza Pap (huu ni ugali) na manyama, ilikua km Rand 40 kwa sahani 1. Baada ya kumaliza kula tukarudi hotel. Keshowe yule dogo akasema kua ni bora akajichanganye kitaa, maana hata passport hakua nayo, ilikua kwenye mabegi aliyompa mwenyeji wake, mimi nikamtakia maisha mema nikamwachia Rand 500.

Wakati tupo hapo Carlton nikagundua kua pako busy sana, hivyo nikapenda nitumie muda kupaelewa zaidi. Baada ya kumaliza ishu zangu za Melrose, sasa nikahamia Carlton Hotel. Nilipofika huku ndio nikapata hali halisi, maisha halisi ya wabongo wengi wa SA.
Kuna muhudumu wa hapa hitelini akatokea kua jamaa yangu sn, hivyo kila alipomaliza zamu yake, alikua ananitembeza mitaa ya Carlton.

Mitaa ya Carlton ambayo sikumbuki majina

Huku kwa kweli nilikutana na wabongo wengi, japo nilikua naficha identity yangu, maana nilishatahadharishwa kua wahuni ni wengi.View attachment 510257Gandhi Square, eneo maarufu hapa mitaa ya Carlton Centre

Wabongo wengi niliwaona wapo kwenye kama vikundi, yani kuna sehemu katika mtaa unakuta watu wote wanaongea kiswahili. Haya yalikua maeneo duni sana, machafu, yananuka kila aina ya harufu. Wabongo wengi walikua ni vibaka, wanategeshea kwenye zebra cross ambayo msongamano wa watu ni mkubwa sana. Kisha wanawazonga watu, na kuwakwapulia mali zao kwa staili ya Chadema.

Nilijibanza sehemu ili niusome mchezo, kwakweli wadada na wamama walikua wanalizwa sana. Simu, hela, vipochi, wallet. Wengi wa hawa wabongo walikua kama mateja, wamechoka sana wanapolala ndio hapo hapo wanapokojoa.

Polly street na Marshall street

Hii mitaa nilikutana na wabongo wengi sana wanaunga unga maisha, wamekata tamaa kabisa.

>Kuna majamaa wawili walikua wanatembea mtaani wamebeba maboxi kama subwoofer wanazungumza. Jamaa mmoja akamuuliza mwenzie - hivi Ally umemuona hivi karibuni, yule mwenzie akajibu - alli si yupo kwa yule muhundi. Jamaa akamjibu tena - dah jamaa kaotea sana maisha. Wale majamaa ghafla wakaingia kwenye duka fulani na hile mizigo. Nahisi ilikua ni mali ya wizi sasa wanaenda kuuza.

>Hapo hapo polly street kuna jengo limechakaa kiasi, hata sikuweza kulitambua kwa jina. Pale wadada walikua wanajiuza kuanzia asubuhi, mchana, jioni hadi usiku, yale kuuza mbunye pale ni kama kuuza mtumba Karume. Na bei yao ni sawa na mahindi mawili ya kuchoma hapo mtaani, yani walikua wanajiuza short time kwa Rand 24 (hii ni sawa na 3,800 Tsh). Hapo wanapojiuza tulikaa kama dakika 15 hivi, nikiwa hapo nilisikia sauti ya mdada yupo ndani anaita "Fetiii fetii njoo mara 1". Nikajua wazi hayo maeneo yana wabongo wengi sana

>Kuna mtaa fulani wa Fox street iliyochoka kuna frame nyingi sana za saloon. Kule saloon inakuwa na huduma zote za kike na kiume. Jamaa yangu akanipitisha hayo maeneo, kuna sehemu tukasimama kununua matunda. Hapo nilimsikia kinyozi mmoja anamkaripia mwenzie "Oyah kula vichwa, kula vichwa. Changamka huoni wanakupita." Hapo nikajua kbs ni mtaa wa wabongo, nikaingia kama kuzuga kunyoa ndevu.

Mule niliwakuta masela wengi sana wamejazana wakiwa hawana mwelekeo, vinyozi ni wa 3 tu na wadada wa kusuka wawili na jamaa mmoja wa kuchora tatoo. Kunyoa pale bei ilikua R15.

Cheeky tiger, diplomatic hotel na patapata Cuisine

Tukiwa tunakatiza mitaa jamaa yangu akanipeleka hapo cheeky tiger. Tukapigwa search pale getini, kisha tukalipa R5 kila mmoja. Jamaa hakuniambia nini kinaendelea, tulipoingua ndani kidogo nikate kauli (hahaha hahaha).

Mimi sijawahi kuona strippers live, nilikua nawaona kwa movies tu, sasa hapa niliwaona live. Yani wadada wanasasambua uchiii, mtu anaenda anamtunza hela labda Rand 50 au 20 au hata 10, akifika hapo anashika shika mzigo anapima wese na kubambia pia.

Humo ndani kuna wadada wengi mno, wakiwa wamevaa nusu uchi, wengine bikini huku juu wakiwa wazi. Mwanzo nilikua nnina hofu sn, nikawa najihisi guilty mno, jamaa yangu akanituliza. Nakumbuka hii ndio ile weekend Arsenal alimchapa Man Utd 2-0. Game kipindi cha kwanza chote tulicheki hapo, baada ya kupata ujasiri nilimwita mdada mmoja hapo nikawa namdadisi. Alianza kuniongelesha Kizulu nikamkatisha haraka sana, tukaswitch into English. Pale short time ni Rand 60-70, yule dada nikampa 50 ili tupige story.

Alichonielezea pale wapo wadada kama 160, kila ukichukuliwa kwenda kusafisha rungu basi Rand 20 ni ya mwenye Cheeky Tiger afu Rand 50 ndio ya mwanamke, kwasiku anapata hadi wateja 50. Na alinieleza na kuniitia watanzania wawili, wengine hakuwaona. Ni wadada mashine haswa hawa wabongo, walipogundua mimi ni mbongo walinichangamkia sana.

Mechi ilivyoisha tukaenda tena sehemu inaitwa diplomatic hotel. Hapa sasa ni kama mara 2 ya cheeky tiger, wadada ni wengi mno humo ndani japo wao kidogo hawapo uchi sana, na bei zao ilikua ni Rand 50. Hapa sikuongea na mdada yoyote lkn nilisikia mdada mmoja mwenye lafudhi ya Zanzibar akisema "naomba unisogezee hiyo tishu". Yani haya maeneo kuna uchafu vibaya mno. Natamani ningeshare picha, lkn naheshimu ID yangu hapa JF na kwamba hili si jukwaa pendwa la chini kabisa.
View attachment 510258 Patapata

Baadae kabisa tukaelekea Pata Pata. Hapa kweli unapata vitu. Tulienda kula, vyakula vyao vilikua kiwango haswa, baadae nikagundua muhudumu mmoja pale ni Mkenya, akaniambia nibaki pale hadi pachangamke. Alinipromise kuniunganisha na Wabongo kadhaa.

Mida ilivyoanza kukata pakaanza kujaa, aloo yani hiki kijiwe ni balaa. Kulikua na wadada wengi wa Kibongo na Wakenya wanauza. Lkn hawa walikua tofauti na wa awali, hawa walikua very professional, na quality ya juu kidogo.

Kusema kweli Wabongo wengi niliowaona hawakua na maisha ambayo wengi hutegemea. Ni huruma sana kuona wenzetu wakiwa kwenye maisha ya namna hii katika nchi za ugenini. Wengi wamekata tamaa, hawana mbele wala nyuma, wapo hopeless sana.

Mpk happ nikawa nimejiridhisha ktk utafiti wangu, sasa nikaamua niende mitaa ya Soweto, kutokana na umaarufu wa Soweto.
View attachment 510259

Soweto

Siku zote mnasikia neno 'Chaf Pozi', hii kitu ipo Soweto, na hapa ndio Chaf Pozi penyewe achana na mambo ya Bill NassView attachment 510260Chaf Pozi, Orlando Towers.
Huku sasa ndio townships, au tuseme kama uswazi. Wabongo huku nilikutana nao wengi mno, na niseme wazi wengi shughuli zao zilikua ni hizi hizi za hapa na pale. Wengi ni vinyozi, wauza mayai, wauza matunda, waziba pancha. Kuna mmoja nilipata bahati ya kuongea nae, yeye alikua anaosha magari na alikua kijiweni kwake kwenye Taxi (daladala)
View attachment 510261

Mwisho

Siwezi nikahitimisha 1 kwa 1 kuwa watu wasizamie kwenda SA, lkn nachojaribu kusema ni kuwa kila mtu mwenye plans za kutafuta maisha SA ahakikishe kuwa kila kitu kipo well sorted out hata kabla hajatoka Bongo, sio kwenda kichwa kichwa na kukutana na mambo tofauti. Hapo Johannesburg kuna kila mwafrika, Botswana, Malawi, Zambia, Kenya, Nigeria nk nk. Tena hawa wanigeria ndio hatari, hua wakiotea mchongo wanahamisha wenzao wote kutoka Lagos na Abuja. So wabongo wengi wanaishia kwenye michongo isiyoeleweka. Sijui hata wakifa hua wanazikwa wapi.

Ontario
Duh hii movie Nilitamani isiishe nzuri sana sana sana booonge la documentary hongera sana Mdau,binafsi kwetu Green City aka Mby ni njia panda ya kwenda RSA,zamani ilikuwa ni ndoto yangu kwenda kuishi kule sababu Brothers wakipiga picha Wamenenpa na wamependeza kwa mavazi Nilijua maisha huko ni rahisi tu mpaka siku Moja Jamaa mmoja alisema siwezi kuruhusu ndugu yangu kuishi South kuuana ni dakika moja bora Nibaki sokomatola au Mbata kuliko RSA!
 
Pia ufike cape town. Na ukifika Johannesburg fanya mawasiliano tukukutanishe na watanzania wenye maisha yao. Mana kuwajumlisha wote kisa umeona maisha ya mateja. ... da!
Boss siwezi kugeneralize kuwa Wabongo wote ni mateja hahahaa. Pia weekend nakuja Jozi maeneo ya Honey Dew, from Rustenburg, ntakua nalala Home Stay Hotel hapo Roodpoort.

Boss nimefika Cape town. Huko si Africa, si Africa Kabisa. Nilifika Western Cape, kisha nikakaa V & A Waterfront. Huko sijawahi kuona hata dalili ya wabongo. Yani niseme mpaka Mbongo anafika Cape, basi huyo katoka Bongo anajua route yake mwanzo hadi mwisho. Maana ukiangalia hata flight distance tu kutoka O.R Tambo hadi Cape Town Airport bi sawa na O.R Tambo hadi Dar.
4978bf2d61ffb9edf532b9d4715f77f9.jpg
 
Natoka chafu pozii...asant sana mkuu.ila ntaisoma asbuh,ilo neno juu ndo nimeliona harak na pich y ilo eneo.
 
Ontan katika uhalisia wake...ushanidaka mkuu nikiona bandiko lako tu lazima nilipitie....makes clap!
Thanks my main man. Tupo pamoja sana askari wangu.
 
Mkuu mbona tupo wengi tu na wengine wametusua hapahapa wakasonga mbelembele huko na wanafanya vizuri tu spain, sweden, Belgium, Holland, Italy nk..

Karibu maeneo yetu sandton tuchome nyama Mandela square hapo.. ..
 
Unanikumbusha mbali sana mkuu enzi za kubandika stick za wachezaji kwenye madaftari yaliyoisha. Bring back those days of golden goal. I still have image ya David Trezeguet anawatungua wataliano Euro 2000. Dammmnn!! where are those days!!!

Well said mkuu, huyo mwalimu is a good reference kwa wale waliosoma na kutaka kwenda abroad kutafuta maisha. Lakini mbaya zaidi ndugu zetu hawa ambao hawana hata vyeti feki, wanapofika huko ndiyo haya anayoyaelezea mtoa mada. Wengi wanaenda wakiwa hawana dira, no money in their pockets, they just depends on lucky and at the end of the day wanakuwa "screwed up".

"If you don't know where you go, no way can take you there"

David Treziguet a.k.a Trezgoals hahaha... Huyu jamaa haki ya nani wataliano hawawezi msahau, umenifanya nikumbuke the luckiest France!! ilikuwaga ina bahati sana miaka hiyo, miss that golden era.

In blue, umeongea kitu cha msingi saaaana ambacho nilitaka nikiandike hata kwenye reply iliyopita ila nikaona nisubiri kwanza ni muone gani hasa ulio nao... Huyo mwalimu amekanyaga bondeni kwa mara ya kwanza 2009 nadhani ilikuwa ni baada tu ya Xenophobic attack ile ya kwanza, alikuwa ana kielimu chake kiana alichotoka nacho hapa bongo amefika kule amefanya kazi hizi hizi za hohe hahe ila upate kula tu, baadae akaona arudi class kwenye hiyo hiyo aridhi ya madiba... Amemaliza course kapata internship na internships za kule sio za kishamba kama huku eti hata nauli hupati, kule unapata allowance una sahau kama unajitolea.

Hakuchukua muda akapata shavu, sasa hivi nakula zake ZR20k+ ambozo ni zaidi ya Tsh.4.4m. Na maisha yanasonga.

Ukweli ni kwamba unapoenda kwenye nchi za watu kama hauna shule, hauna fani wala kipaji chochote hata cha kuendesha maringi yaani wewe ni bashite type na kibaya zaidi hata lugha nayo iwe ni tatizo ....haaaa hapo lazima usage meno na utajikuta umekuwa kibaka automatically.

If you don't know the way, then the way itself will take you anywhere.
 
Salute!

Nakumbuka mara yangu ya kwanza kuingia Afrika Kusini ilikuwa mwaka 2015, nikiwa chuo mwaka wa 2. Kuanzia hapo safari za kwenda huko Bondeni zikawa ni za mara kwa mara. View attachment 510219

Lkn kwa bahati mbaya, mara nyingi nilivyokua naenda huko sikuwa na muda wa kutosha sana kuzunguka na kuiona Afrika kusini katika 3 dimensions. Mara kadhaa nilikua naenda Johannesburg na kuishi sehemu 1 bila kupata fursa ya kuzama downtown, na maeneo niliyokua nafikia ni yale ambayo hayana purukushani kama Sandton, Roodport, Midrand na Melrose Arch. Na hata muda ulikua very much limited.View attachment 510225Sandton City Shopping centre.

Tarehe 11 April nikaja hapa Afrika Kusini kwa ajili ya shughuli zangu kadhaa, safari hii ambapo nimemaliza chuo na nipo huru, basi nikaplan nikae hapa kwa muda mrefu zaidi hadi May 23. Na moja ya vitu vilivyonisukuma kukaa huku muda mrefu ni kujua hali ya maisha ya Watanzania wenzangu wa hapa, nikiamini kua kwa namna 1 ama nyingine ningeweza kujifunza mbinu kadhaa za kupambana na haya maisha.View attachment 510227Nikiwa safarini kuelekea Jozi.

[/B]Midrand

Siku niliyofika mwenyeji wangu alinichukua na kuniacha hotel hapo Midrand, kisha yeye akaelekea kwake Pretoria.View attachment 510231Mall of Africa - nahisi hii ni mall kubwa zaidi Afrika, maana nilipotea mara kadhaa humo ndani.

Nilivyosettle nikaenda restaurant ya jirani kupata dinner, sasa nilikua nimeingia instagram, nikawa natazama video ambayo ilikua ikiplay kwa kiswahili. Kuna jamaa kama meza 2 au 3 mbele yangu akawa ananitazama sana, nikagundua yule bwana anafahamu kiswahili, lkn sikuweza kuconfirm kama ni Mtanzania, Mkenya, Mkongo ama vipi. Akaondoka zake mimi nikabaki nakula, nilivyomaliza kula nikapata wazo la kubadili sim cards, hivyo nilihitaji kwenda kusajili line ya Telkom SA na Cell C.

Very coincidentally, nilivyoenda kusajili Cell C nikamkuta yule bwana pale. Hata alivyoona passport yangu bado Hakutaka kujitambulisha, lkn kadri alivyozidi kuongea kingereza cha kuunga unga ndipo nikagundua yule jamaa ni Mbongo. Sikukutana na Mtanzania mwingine hadi naondoka Midrand.

Pretoria

Muda wote nikiwa Midrand, trips zangu zilikua za kwenda Pretoria, sikuwahi kukutana na Mbongo yeyote hadi siku nilipoenda Tanzanian restaurant. Kwakeli hata watumiaji wa hile restaurant walikua ni waAfrika kusini, kuna mdingi mmoja alikuja na familia yake yeye na mkewe walikua wakiongea kiswahili, mzee alipaki E- class Mercedes benz na alikua na card nyeusi ya FNB Bank (hii card inamaanisha mtu ana zaidi ya Rand mil 1 kwa account).

Johannesburg

Baada ya siku kadhaa nikaenda kuishi Johannesburg maana hapo pia nilikua na shughuli nyingine ambayo inajitegemea tofauti na ile ya Pretoria, ikawa kuishi Jozi kungenirahisishia usafiri.View attachment 5102561 ya vivutio vya Jozi

Melrose Arch

View attachment 510246mtaa wa QwaQwa, Melrose.

Nilifika hapo Jozi hotel 1 inaitwa Blu Swan, siku ya Ijumaa jioni, nilikua nina weekend yote kurelax then j3 pilika pilika zianze. Nakumbuka siku ya Jumapili jioni, kukawa kama na majibizano, vyumba kadhaa kutoka chumbani kwangu. Sikutilia maanani sana.

Lkn baada km ya nusu saa majibizano yalizidi, nikasikia watu wakitembea kwa veranda, wakasimama karibu na mlango wangu. Nikategesha sikio vizuri, kuna mmoja alikua anajaribu kupiga simu, akaweka 'loud speaker'. Ile call ikaleta sauti ya mhudumu wa Voda "Namba unayoipigia haipatikani kwa sasa...". Nikajua fika huyu ni mbongo, nikatoka nje ya chumba changu ili nione nini kinaendelea.

Majibizano yale yalikua kati ya security wa hotel na huyo jamaa. Alikua kjn mdogo km wa miaka 25 hivi, kilichokua kikiendelea ni kua huyo dogo alikua anafukuzwa atoke pale kwa kushindwa kulipa pesa ya hotel.

Nikatumia uungwana, nikamuomba huyo security aachane nae mimi nitamlipia kwa siku hiyo. Nikaingia ndani nikachomoa Rand 780 nikamlipia huyo dogo. Baada ya kuSort out ile ishu, tukawa na majadiliano nae. Dogo alinambia vitu vya kusikitisha sana.

Ni kwamba, alikua ana siku 2 tangu aingie SA, alikua ametumwa na Boss wake. Kwa maelezo ya dogo ni kua Boss wake anaitwa Jumbe, ni mdau wa Ilala mtaa wa Arusha. Dogo alipewa mzigo aje nao, alikua na mabegi mawili. Kisha akifika SA atakutana na mwenyeji wake ambae atamwachia huo mzigo, baadae atapewa pesa ya kujikimu na nauli ya kurudi Bongo.

Dogo alivyokutana na mwenyeji wake, akamkabidhi mizigo, kisha akapelekwa hotel akalipiwa siku 1 then yule mwenyeji wake akaondoka mazima. Dogo wala hatambui nini kilikua kwenye hayo mabegi, ambayo alidai yalikua madogo ya mgongoni. Kutokana na njaa aliyokua nayo dogo, nikaamua tusile vyakula vya hotel, tukaenda kugonga vyakula local. Dereva akatuendesha hadi Carlton Centre.

Carlton Centre

Kusema kweli sijawahi kua na real experience ya Johannesburg hadi nilipofika hapa mitaa ya Carlton.View attachment 510254muonekano wa Carlton kutoka Jengo maarufu sana la Transet.

Tukafika Simmonds Street, tukapata mgahawa tukaagiza Pap (huu ni ugali) na manyama, ilikua km Rand 40 kwa sahani 1. Baada ya kumaliza kula tukarudi hotel. Keshowe yule dogo akasema kua ni bora akajichanganye kitaa, maana hata passport hakua nayo, ilikua kwenye mabegi aliyompa mwenyeji wake, mimi nikamtakia maisha mema nikamwachia Rand 500.

Wakati tupo hapo Carlton nikagundua kua pako busy sana, hivyo nikapenda nitumie muda kupaelewa zaidi. Baada ya kumaliza ishu zangu za Melrose, sasa nikahamia Carlton Hotel. Nilipofika huku ndio nikapata hali halisi, maisha halisi ya wabongo wengi wa SA.
Kuna muhudumu wa hapa hitelini akatokea kua jamaa yangu sn, hivyo kila alipomaliza zamu yake, alikua ananitembeza mitaa ya Carlton.

Mitaa ya Carlton ambayo sikumbuki majina

Huku kwa kweli nilikutana na wabongo wengi, japo nilikua naficha identity yangu, maana nilishatahadharishwa kua wahuni ni wengi.View attachment 510257Gandhi Square, eneo maarufu hapa mitaa ya Carlton Centre

Wabongo wengi niliwaona wapo kwenye kama vikundi, yani kuna sehemu katika mtaa unakuta watu wote wanaongea kiswahili. Haya yalikua maeneo duni sana, machafu, yananuka kila aina ya harufu. Wabongo wengi walikua ni vibaka, wanategeshea kwenye zebra cross ambayo msongamano wa watu ni mkubwa sana. Kisha wanawazonga watu, na kuwakwapulia mali zao kwa staili ya Chadema.

Nilijibanza sehemu ili niusome mchezo, kwakweli wadada na wamama walikua wanalizwa sana. Simu, hela, vipochi, wallet. Wengi wa hawa wabongo walikua kama mateja, wamechoka sana wanapolala ndio hapo hapo wanapokojoa.

Polly street na Marshall street

Hii mitaa nilikutana na wabongo wengi sana wanaunga unga maisha, wamekata tamaa kabisa.

>Kuna majamaa wawili walikua wanatembea mtaani wamebeba maboxi kama subwoofer wanazungumza. Jamaa mmoja akamuuliza mwenzie - hivi Ally umemuona hivi karibuni, yule mwenzie akajibu - alli si yupo kwa yule muhundi. Jamaa akamjibu tena - dah jamaa kaotea sana maisha. Wale majamaa ghafla wakaingia kwenye duka fulani na hile mizigo. Nahisi ilikua ni mali ya wizi sasa wanaenda kuuza.

>Hapo hapo polly street kuna jengo limechakaa kiasi, hata sikuweza kulitambua kwa jina. Pale wadada walikua wanajiuza kuanzia asubuhi, mchana, jioni hadi usiku, yale kuuza mbunye pale ni kama kuuza mtumba Karume. Na bei yao ni sawa na mahindi mawili ya kuchoma hapo mtaani, yani walikua wanajiuza short time kwa Rand 24 (hii ni sawa na 3,800 Tsh). Hapo wanapojiuza tulikaa kama dakika 15 hivi, nikiwa hapo nilisikia sauti ya mdada yupo ndani anaita "Fetiii fetii njoo mara 1". Nikajua wazi hayo maeneo yana wabongo wengi sana

>Kuna mtaa fulani wa Fox street iliyochoka kuna frame nyingi sana za saloon. Kule saloon inakuwa na huduma zote za kike na kiume. Jamaa yangu akanipitisha hayo maeneo, kuna sehemu tukasimama kununua matunda. Hapo nilimsikia kinyozi mmoja anamkaripia mwenzie "Oyah kula vichwa, kula vichwa. Changamka huoni wanakupita." Hapo nikajua kbs ni mtaa wa wabongo, nikaingia kama kuzuga kunyoa ndevu.

Mule niliwakuta masela wengi sana wamejazana wakiwa hawana mwelekeo, vinyozi ni wa 3 tu na wadada wa kusuka wawili na jamaa mmoja wa kuchora tatoo. Kunyoa pale bei ilikua R15.

Cheeky tiger, diplomatic hotel na patapata Cuisine

Tukiwa tunakatiza mitaa jamaa yangu akanipeleka hapo cheeky tiger. Tukapigwa search pale getini, kisha tukalipa R5 kila mmoja. Jamaa hakuniambia nini kinaendelea, tulipoingua ndani kidogo nikate kauli (hahaha hahaha).

Mimi sijawahi kuona strippers live, nilikua nawaona kwa movies tu, sasa hapa niliwaona live. Yani wadada wanasasambua uchiii, mtu anaenda anamtunza hela labda Rand 50 au 20 au hata 10, akifika hapo anashika shika mzigo anapima wese na kubambia pia.

Humo ndani kuna wadada wengi mno, wakiwa wamevaa nusu uchi, wengine bikini huku juu wakiwa wazi. Mwanzo nilikua nnina hofu sn, nikawa najihisi guilty mno, jamaa yangu akanituliza. Nakumbuka hii ndio ile weekend Arsenal alimchapa Man Utd 2-0. Game kipindi cha kwanza chote tulicheki hapo, baada ya kupata ujasiri nilimwita mdada mmoja hapo nikawa namdadisi. Alianza kuniongelesha Kizulu nikamkatisha haraka sana, tukaswitch into English. Pale short time ni Rand 60-70, yule dada nikampa 50 ili tupige story.

Alichonielezea pale wapo wadada kama 160, kila ukichukuliwa kwenda kusafisha rungu basi Rand 20 ni ya mwenye Cheeky Tiger afu Rand 50 ndio ya mwanamke, kwasiku anapata hadi wateja 50. Na alinieleza na kuniitia watanzania wawili, wengine hakuwaona. Ni wadada mashine haswa hawa wabongo, walipogundua mimi ni mbongo walinichangamkia sana.

Mechi ilivyoisha tukaenda tena sehemu inaitwa diplomatic hotel. Hapa sasa ni kama mara 2 ya cheeky tiger, wadada ni wengi mno humo ndani japo wao kidogo hawapo uchi sana, na bei zao ilikua ni Rand 50. Hapa sikuongea na mdada yoyote lkn nilisikia mdada mmoja mwenye lafudhi ya Zanzibar akisema "naomba unisogezee hiyo tishu". Yani haya maeneo kuna uchafu vibaya mno. Natamani ningeshare picha, lkn naheshimu ID yangu hapa JF na kwamba hili si jukwaa pendwa la chini kabisa.
View attachment 510258 Patapata

Baadae kabisa tukaelekea Pata Pata. Hapa kweli unapata vitu. Tulienda kula, vyakula vyao vilikua kiwango haswa, baadae nikagundua muhudumu mmoja pale ni Mkenya, akaniambia nibaki pale hadi pachangamke. Alinipromise kuniunganisha na Wabongo kadhaa.

Mida ilivyoanza kukata pakaanza kujaa, aloo yani hiki kijiwe ni balaa. Kulikua na wadada wengi wa Kibongo na Wakenya wanauza. Lkn hawa walikua tofauti na wa awali, hawa walikua very professional, na quality ya juu kidogo.

Kusema kweli Wabongo wengi niliowaona hawakua na maisha ambayo wengi hutegemea. Ni huruma sana kuona wenzetu wakiwa kwenye maisha ya namna hii katika nchi za ugenini. Wengi wamekata tamaa, hawana mbele wala nyuma, wapo hopeless sana.

Mpk happ nikawa nimejiridhisha ktk utafiti wangu, sasa nikaamua niende mitaa ya Soweto, kutokana na umaarufu wa Soweto.
View attachment 510259

Soweto

Siku zote mnasikia neno 'Chaf Pozi', hii kitu ipo Soweto, na hapa ndio Chaf Pozi penyewe achana na mambo ya Bill NassView attachment 510260Chaf Pozi, Orlando Towers.
Huku sasa ndio townships, au tuseme kama uswazi. Wabongo huku nilikutana nao wengi mno, na niseme wazi wengi shughuli zao zilikua ni hizi hizi za hapa na pale. Wengi ni vinyozi, wauza mayai, wauza matunda, waziba pancha. Kuna mmoja nilipata bahati ya kuongea nae, yeye alikua anaosha magari na alikua kijiweni kwake kwenye Taxi (daladala)
View attachment 510261

Mwisho

Siwezi nikahitimisha 1 kwa 1 kuwa watu wasizamie kwenda SA, lkn nachojaribu kusema ni kuwa kila mtu mwenye plans za kutafuta maisha SA ahakikishe kuwa kila kitu kipo well sorted out hata kabla hajatoka Bongo, sio kwenda kichwa kichwa na kukutana na mambo tofauti. Hapo Johannesburg kuna kila mwafrika, Botswana, Malawi, Zambia, Kenya, Nigeria nk nk. Tena hawa wanigeria ndio hatari, hua wakiotea mchongo wanahamisha wenzao wote kutoka Lagos na Abuja. So wabongo wengi wanaishia kwenye michongo isiyoeleweka. Sijui hata wakifa hua wanazikwa wapi.

Ontario
Kiongozi Ongera sna karibu sna kifupi maisha uliozungumzia hata nyumbani bongo yko kupanga ni kuchagua hao uliwakuta wanaishi maisha hayo ndio maisha walio chagua ila tupo tunao jielewa na maisha yanakwenda...
 
Thanks my main man. Tupo pamoja sana askari wangu.
HATA BONGO WAPO<br />Mi nampongeza sana mtoa mada. Nafikiri ni muandishi. Na nimuandishi mzuri kwa kweli. <br /> Ameeleza kwa ufasaha sana Yale aliyoyaona. Na amejitahid kuyapigia rangi inayompendeza. Lakin kamlipia mtu hotel ambae aliachwa hotel na mtu asiejulikana (kama kweli) mtanzania alieachwa kwenye mataa hotel, simkazi wa afrika kusini. Ni mtu alietumwa Afrika kusini akaachwa solemba. Je mtu aliemtuma kutoka bongo hakumpa japo pesa kidogo ya kijikwimu? Shida imeanzia bongo.<br /> Mana nadhani kama aliondoka bila kuchukua walau nusu ya malipo yake ya kazi yake kazi ipo hapo. Sijui kama Hilo lina uhusiano wowote na maisha ya south Africa au ni tabia tu ya hao watu alofanya nao biahara. <br /> Kisha akaenda mjini. Cbd. Kama nimesoma vizuri akaona vibaka wa ndole. Tena mateja. Je ndo utapima maisha ya watanzania wanaoishi Afrika kusini kwa kiwaangalia hao. <br /> Alienda kunyoa. Akaona vinyozi na baadhi ya watanzania wasio na kazi wamekaa hapo. Je ni maisha ya watanzania wote afrika kusini. <br /> Maisha yote uliyafanikiwa kuyaona Afrika kisini. HATA bongo yapo. Wapo watanzania wanaoishi maisha hayo ndani ya Tanzania. Ila si maisha ya watanzania wote. <br /> Maisha ya watanzania ndani ya afrika kusini hayana tofauti maisha ya watanzania ndani ya Tanzania. Wapo wanaoishi vizuri sana. Wapo wanaoishi maisha ya kati. Wapo wanaoishi maisha ya kawaida. Wapo wanaoishi maisha dhalili sana. Na aina yote hii ya watu, Hata bongo wapo. Nimesema.
 
Back
Top Bottom